SWALI: Nini maana ya Mithali 25:13
Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.
JIBU: Kwa wanaoishi maeneo ambayo kuna misimu ya theluji, wanafahamu kuwa vipindi hivyo vya baridi vinapofika, huwa kunakuwa na upepo-baridi unaovuma.
Sasa kwa mujibu wa vifungu hivyo, anasema, Kama upepo huo ukivuma kipindi cha mavuno, ambacho kimsingi ni wakati wa kiangazi,na sio baridi, kingekuwa ni shangwe kubwa sana kwa wavunaji.
Kwa namna gani?
Kazi ya uvunaji inafanyika wakati wa jua kali, kwasababu mazao pia wakati huo yanakuwa yamekauka. Lakini pia mfano jua lile likapoozwa na upepo wa baridi, huuburudisha sana moyo wa mvunaji.
Vivyo hivyo anafananisha na wajumbe waaminifu wanaotumwa kupeleka habari fulani anasema;
“Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao”.
Mjumbe wa kwanza mwaminifu aliyetumwa ni Bwana wetu Yesu Kristo. Alimburudisha Baba moyo wake, kwasababu yote, na kusudi alilopewa kulifanya la kutukomboa sisi alilitimiza lote.
Vivyo hivyo na sisi, tumewekwa kuwa wajumbe wa Bwana, wa kuenenda kuihubiri injili ya Kristo kwa kila kiumbe, ulimwenguni kote. Yatupasa tuwe waaminifu, mfano wa Bwana na mitume wake, ili moyo wa Kristo wetu ufurahi.
Na thawabu ya kuuburudisha moyo wa Bwana ni sisi kupewa mamlaka kubwa kule ng’ambo tufikapo, kwa mfano ambao Bwana Yesu aliutoa katika vifungu hivi;
Luka 19:12-26
[12]Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi. [13]Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja. [14]Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale. [15]Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. [16]Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. [17]Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. [18]Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida. [19]Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano. [20]Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso. [21]Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. [22]Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda; [23]basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake? [24]Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi. [25]Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi. [26]Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho.
[12]Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
[13]Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.
[14]Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.
[15]Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.
[16]Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.
[17]Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.
[18]Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.
[19]Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.
[20]Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.
[21]Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.
[22]Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
[23]basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?
[24]Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.
[25]Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.
[26]Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho.
Je na sisi tunaweza kuwa mbele za Bwana Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; ?
Bwana atusaidie.
Je! Umeokoka?
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?
WALIYATWAA MAVAZI YAKE, WAKAFANYA MAFUNGU MANNE,
Tofauti kati ya zaka na sadaka ni ipi?
AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.
Rudi nyumbani
Print this post