Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?

Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?

SWALI: Kikombe cha maji ya baridi ni  kipi Bwana alichokitaja katika;

Mathayo 10:42  Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake


JIBU: Ni kawaida mtu anayetoka kufanya kazi ngumu, labda ya shamba, au wanaoshiriki katika michezo labda riadha au mipira, utaona huduma ya kwanza wanayoihitaji, sio chakula, bali ni maji, kwasababu mwili huwa unapoteza maji mengi sana pale jasho linapotoka. Na gharama ya maji sikuzote ni ndogo kuliko chakula. Hivyo mtu yeyote huwa ni rahisi kupata huduma hiyo, kwani mtu anaweza kumtolea ndani mwake kwenye pipa lake la kutunzia maji masafi, au kuchota kisimani, na kumpa n.k. Na pale anapompa ya baridi kabisa basi humfanya mtu yule ayanywe yale maji sio tu kwa kukata kiu lakini pia kwa burudiko.

Vivyo hivyo na Bwana naye anawafananisha watu wake, na watenda kazi waliotoka kufanya kazi ya kuchosha, hivyo na wenyewe huwa wanakuwa na kiu chao, wanahitaji maji yao. Lakini zaidi sana maji baridi. Na mtu anayefanya hivyo Mungu amemuahidia kumpa thawabu yake.

Maji ya mwaminio ni yapi?

Yanaweza kuwa ni vyakula: Kwamfano umuonapo, mtumishi wa Mungu labda anahudumu au anahubiri pengine kwenye masoko, au mahali fulani kwa muda mrefu, na wewe ukathamini kumpatia chakula au hata chupa ya maji. Akanywa au akala ashiba akamshukuru Mungu. Hiyo ni thawabu kwako kwa Mungu.

Yaweza pia kuwa sadaka yako: Kile kidogo, kinachoweza kumtunza hata kwa siku hiyo, kwa ajili ya usafiri, au sabuni, au vocha kwa ajili ya mahitaji yake madogo madogo. Bwana amekuahidia pia thawabu yako hata kama utakiona ni kidogo, si zaidi  ukampa vya ziada? Kinabadilika kuwa kikombe cha maji ya baridi.

Yaweza kuwa pia ni “vitu”: Mfano mwingine hana fedha au chakula, lakini ana kitu Fulani cha kumpa, labda nguo, au kiatu, au simu, au huduma n.k. Hicho nacho Bwana anakihesabu kama kikombe cha maji ya baridi.

Hivyo kwa hitimisho ni kuwa zipo thawabu mbalimbali ambazo Bwana anatoa, kwa kutenda mema, zipo thawabu za kuwasaidia maskini, zipo thawabu za kuwasaidia ndugu, lakini zaidi pia Bwana ameahidi thawabu kwa wale wote wanaowajali watumishi wake.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mafundisho mengine:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA.

JE NI KIKOMBE KIPI UTAKINYWEA SIKU ILE?

YESU ANA KIU NA WEWE.

UWE KIKOMBE SAFI 

AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.

MAJI YA UZIMA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments