Elewa maana ya Mithali 18:23 Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali. 

Elewa maana ya Mithali 18:23 Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali. 

Mstari huu unaeleza uhalisia wa mambo kwa ujumla wake katika maisha ya wanadamu hapa duniani.

Tunafahamu kwamba maskini wengi hutumia maombi kupata kitu, huwa wanyenyekevu pale wanapotaka kupewa kitu, kwasababu hawana. 

Lakini matajiri hawawezi kujishusha (japo si wote) kauli zao huwa ni za lazima na zenye amri. Kwani mali zake humpa kiburi. Hivyo waombe ya nini?

Sasa biblia haitufundishi tuwe matajiri ili tuwe wakali (wenye sauti) hapana, bali inatutahadharisha matokeo ya mafanikio yoyote. Jinsi yanavyoweza kumpotezea mtu unyenyekevu wake.

Bwana akunyanyuapo, ndio uwe wakati wako wa kujishusha. Kwasababu mali, fedha, mafanikio visipowekewa mipaka yake vinaweza kuyaharibu maisha ya mwaminio kwa sehemu kubwa. (1Timotheo 16:10)

Lakini pia katika eneo la kiroho. Kuna maneno haya Bwana Yesu aliyasema.

Mathayo 5:3

[3]Heri walio maskini wa roho;  Maana ufalme wa mbinguni ni wao. 

Ikiwa na maana watu walio maskini rohoni, ni wale wanaojiona kila siku wana haja na Mungu, bado hawajafika. Na hivyo humlilia Mungu sikuzote kwa unyenyekevu ili Bwana ayaongoze maisha yao.

Lakini wale wanaojiona wamefika wanajua kila kitu hawawezi kufanya hivyo. Ndio wale mafarisayo enzi za Bwana Yesu ambao hata kuomba kwao kulikuwa ni kwa majivuno (Luka 18:9-14). Hawawezi kujishusha, maneno yao ni ya ukali, wala hawaoni shida kumwita hata  Bwana wao Beelzebuli.

Hata kama tutakuwa tumepiga hatua kubwa kiasi gani rohoni, Bwana hataki tujidhani kuwa sisi tumefika, sisi ni matajiri, bali tumtegemee yeye sikuzote haijalishi wewe ni mtumishi mkubwa au uliyeokoka leo. 

Unyenyekevu kwa Bwana unapaswa uwe ni uleule. Usiende mbele za Mungu kama mtumishi wa Mungu, nenda kama mtoto wa Mungu mfano tu wa yule ambaye kaokoka leo. Jinyenyekeze kama vile ndio umeokoka leo. Kwasababu kumjua Bwana itatuchukua milele.

Lakini tukijiona ni matajiri tutaishia katika anguko hili alilolisema katika..

Ufunuo 3:17-19

[17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. 

[18]Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 

[19]Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 

Hivyo katika utajri wowote (wa kiroho /kimwili). Bwana atupe unyenyekevu kama wa maskini. Ndio kiini cha mstari huo.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Tajiri na maskini hukutana pamoja; BWANA ndiye aliyewaumba wote wawili.

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

Mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?

JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments