Apitaye cheo ni mtu wa namna gani?

Apitaye cheo ni mtu wa namna gani?

Jibu: Turejee..

2Yohana 1:9 “KILA APITAYE CHEO, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia”.

“Cheo” ni neno lenye maana ya “Kipimo”..

> Kwamfano Mtu mwenye kipimo kikubwa cha heshima katika kazi/shughuli fulani maana yake huyo mtu ana cheo kikubwa  katika kazi hiyo…

> Au mtu mwenye kipimo kikubwa che heshima kuliko wenzake katika Serikali/mamlaka, maana yake mtu huyo ana cheo kikubwa..

Marko 6:21 “Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya”

> Vile vile mtu mwenye kipimo kikubwa cha umri, ni sawa na kusema ana cheo kikubwa cha umri..

Mwanzo 43:33 “Wakaketi mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa cheo cha kuzaliwa kwake, na mdogo kwa udogo wake; watu hao wakastaajabu wao kwa wao”.

Sasa tukirudi kwenye swali, mtu apitaye cheo ni mtu wa namna gani?

Mtu “apitaye cheo” kulingana na andiko hilo, ni mtu avukaye kipimo au mipaka ya Mafundisho ya KRISTO.

Maana yake kama neno la Mungu linasema “Usiibe”  au “Usizini” yeye atatafuta namna ya kuhalalisha wizi au uzinzi au ushoga kwa namna yoyote ile (ambapo hapo kwanza tayari alikuwa amekwisha kuamini kuwa wizi na uzinzi ni dhambi) lakini sasa anataka kuhalalisha zinaa au wizi anaoufanya au anaoutamani.

Mtu wa namna hiyo ni mtu aliyevuka cheo cha mafundisho ya Kristo, (maana yake alikuwa katika mafundisho sahihi lakini sasa amevuka mipaka)..na mtu wa hivyo biblia inasema hana Mungu ndani yake.

Hivyo hatuna budi daima kudumu na kusimama katika Neno la Mungu.. Kwasababu biblia inasema limehakikiwa na halina kasoro, na hivyo hatuhitaji sisi kulirekebisha..

Mithali 30:5 “Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.

6 Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo”.

Tukivuka kipimo (cheo) kwasababu aidha ya kiburi au tamaa ya kuhalalisha mambo mabaya na tukalipindisha Neno la lake (mafundisho yake), basi tutaangukia katika hukumu ile iliyotajwa katika Ufunuo 22:18…

Ufunuo 22:18 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki”.

Bwana atusaidie tufikie cheo na si tuvuke cheo. (Waefeso 4:13).

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

USIKWEPE CHUO CHA UTAKATIFU.

UAMINIFU NI KIGEZO KIKUBWA CHA KUTUMIWA NA MUNGU.

Fahamu Namna ya Kuomba.

Je shetani ana uwezo wa kujua mawazo ya mtu?

MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments