Kwanini Bwana Yesu alivikwa taji ya miiba?

Kwanini Bwana Yesu alivikwa taji ya miiba?

Taji ya miiba juu ya kichwa cha Bwana Yesu, iliashiria nini kiroho?..

Tusome,

Mathayo 27:27 “Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio, wakamkusanyikia kikosi kizima.

28 WAKAMVUA NGUO, WAKAMVIKA VAZI JEKUNDU.

29 WAKASOKOTA TAJI YA MIIBA, WAKAIWEKA JUU YA KICHWA CHAKE, NA MWANZI KATIKA MKONO WAKE WA KUUME; WAKAPIGA MAGOTI MBELE YAKE, WAKAMDHIHAKI, WAKISEMA, SALAMU, MFALME WA WAYAHUDI!

30 Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampiga-piga kichwani.

31 Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulibisha”.

Kumbuka Pilato alipomuuliza Bwana Yesu kama yeye ni mfalme wa Wayahudi, Bwana hakukanusha… alimwambia “wewe wasema” maana yake “mimi ndiye”.

Hivyo wale Askari waliposikia Bwana Yesu kakiri kuwa ndiye  mfalme wa wayahudi, walicheka sana.. na kwasababu askari wa kirumi walikuwa wanawadharau wayahudi.. Hivyo ili kuwadhalilisha wayahudi.. ndio wakamvua zile nguo za thamani Bwana Yesu na kumvika vazi la jekundu, na kisha kumpa mwanzi (yaani fimbo)..na kumvika taji ya miiba…na mwisho kuinama kama vile wanamsujudia..

Lengo la kufanya vile ni kumweka katika mazingira kama ya kifalme… kwasababu kikawaida Mfalme anakuwa anavaa mavazi mekundu, pia anakuwa ameshika/anatembea na mwanzi wa thamani, na vile vile kichwani anakuwa na taji la thamani sana.. Lakini kwasababu hawa askari lengo lao lilikuwa ni kufanya dhihaka kwa wayahudi…ndio wakafanya hayo kwa Bwana Yesu, ili aonekane kama mfalme lakini asiye na utukufu, ambaye asiyejielewa.

Lakini walifanya vile kwa lengo la kufanya dhihaka tu!, (na kuwadhalilisha wayahudi) na si vinginevyo!…Na walifanya hivyo kwasababu hawakumjua yeye ni nani?.. kwasababu laiti kama wangemjua kuwa huyo wanayemfanyia dhihaka ndiye Mfalme wa kweli wa mbinguni na duniani, na pia ni Mungu mwenyewe katika mwili, wasingelimsulubisha zaidi ya yote wangemwabudu.

1Wakorintho 2:7 “bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;

8 ambayo wenye kuitawala dunia hii HAWAIJUI HATA MMOJA; MAANA KAMA WANGALIIJUA, WASINGALIMSULIBISHA BWANA WA UTUKUFU”.

Sasa swali ni kwanini Bwana Yesu asingezuia hayo yatokee na ilihali alikuwa na uwezo huo?

Sababu zipo kuu (2).

 1. ILI SISI TUPATE WOKOVU.

Bwana Yesu asingelisulubiwa maana yake sisi tusingelipata wokovu…

 2. ILI AINULIWE JUU.

Bwana Yesu mwenyewe alisema… ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.. Maana yake siri ya kuinuliwa juu, wakati mwingine ni kujishusha…Ili uwe mkubwa kuliko wote sharti uwe mdogo kuliko wote, ili upate heshima kuliko wote, sharti ukubali kukosa heshima kuliko wote, hiyo  ni kanuni kubwa sana, ambayo Bwana Yesu aliijua..

Alifahamu kuwa ili anyanyuliwe juu kuliko vitu vyote, hana budi kukubali kuonekana si kitu sasa.

Wafilipi 2:5 “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;

6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;

7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;

8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba”.

3. KUTUPA SISI KIELELEZO.

Sababu ya mwisho ni ili kutufundisha sisi kuwa wema, kama yeye!… kama yeye mwenyewe alivyosema.. “mtu akupigaye shavu hili mgeuzie na la pili” au mtu akulazimishaye mwendo wa maili moja, nenda naye mbili..Kwasababu kwa kufanya hivyo, ataiona haki yako na mwisho atavutiwa na imani yako, na hata kumbadilisha kabisa… (Umeona askari hao hao waliomfanyia dhihaka, masaa machache tu mbele walikiri kuwa yeye kweli alikuwa Mwana wa Mungu, Marko 15:39).

Na sisi hatuna budi kuwa kama Bwana Yesu, tunapotukanwa tunapaswa tustahimili, tunapoudhiwa na kudhalilishwa tunapaswa tustahimili kama Bwana Yesu, kwasababu mwisho wake ni mzuri..

1Petro 2:19 “Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki.

20 Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.

21 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.

22 Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.

23 Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.

24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

25 Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu”.

Waebrania 12:3 “Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.

4 Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi”.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

MJUE SANA YESU KRISTO.

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

Kwanini hatuirithi neema kama tunavyoirithi dhambi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Devis Julius administrator

Subscribe
Notify of
guest
7 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Célestin
Célestin
2 years ago

Asante kwa somo hili

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Asante kwa masomo, yananijenga sana.

lucas mhula
lucas mhula
2 years ago

Kiukweli nabarikiwa sana naona nazidi kujenga katika kweli ya Mungu siku hadi siku..🙏🙏🙏🤝

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Asantee sana kwa mafundisho haha mbarikiwe🙏

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Ahsante Sana barikiwe🙏🙏

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Asante kwa somo zuri, nimejifunza na kukumbushiwa