Jibu: Turejee..
Kutoka 5:14 “Na WANYAPARA wa wana wa Israeli, ambao wasimamizi wa Farao wamewaweka juu yao, wakapigwa, wakiambiwa, Kwa nini hamkutimiza kazi yenu jana na leo; kwa kufanya matofali kama hapo kwanza? 15 Basi WANYAPARA wa wana wa Israeli wakaenda, wakamlilia Farao, wakisema, Mbona umetutendea hivi, sisi watumwa wako? 16 Watumwa wako hawapewi majani, nao wanatuambia, Fanyeni matofali; na tazama, watumwa wako wapigwa; lakini kosa hilo ni la watu wako mwenyewe”.
Kutoka 5:14 “Na WANYAPARA wa wana wa Israeli, ambao wasimamizi wa Farao wamewaweka juu yao, wakapigwa, wakiambiwa, Kwa nini hamkutimiza kazi yenu jana na leo; kwa kufanya matofali kama hapo kwanza?
15 Basi WANYAPARA wa wana wa Israeli wakaenda, wakamlilia Farao, wakisema, Mbona umetutendea hivi, sisi watumwa wako?
16 Watumwa wako hawapewi majani, nao wanatuambia, Fanyeni matofali; na tazama, watumwa wako wapigwa; lakini kosa hilo ni la watu wako mwenyewe”.
“Wanyapara” ni wasimamizi wa wafungwa au watumwa.
Katika magereza, wale wafungwa wanaoteuliwa kuwa kama viongozi wa wafungwa wenzao ndio wanaoitwa “wanyapara”. Hivyo yule askari ambaye ni mkuu wa gereza anapotoa agizo basi yule Nyapara ndiye anayelichukua na kuliwasilisha kwa wafungwa wenzake na yeye mwenyewe anakuwa ni msimamizi juu yao, ingawa naye pia ni mfungwa.
Sasa kipindi wana wa Israeli wapo Misri utumwani, wale wasimamizi wa Farao (Maaskari) waliwachagua baadhi ya wafungwa na kuwafanya wanyapara kwa wafungwa wenzao.
Na Wasimamizi hao walipotoa amri ya kazi Fulani, basi waliwaangalia hao wanyapara na hao wanyapara ndio waliowaongoza watumwa wenzao, na ikitokea watumwa (wana wa Israeli) wamekaidi au wanafanya kazi kwa ulegevu basi wanaoathirika wa kwanza ni wanyapara wao, kwani wale wasimamizi wa Farao walikuwa wanashughulika kwanza na hao wanyapara kabla ya watumwa wenyewe.
Kutoka 5:14 “Na wanyapara wa wana wa Israeli, ambao wasimamizi wa Farao wamewaweka juu yao, wakapigwa, wakiambiwa, Kwa nini hamkutimiza kazi yenu jana na leo; kwa kufanya matofali kama hapo kwanza?”
Shetani naye anao wanyapara wake aliowaweka juu ya wote wanaotumikishwa na dhambi!.. kwasababu biblia inasema atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi, na kama ni mtumwa basi ni lazima atakuwa na nyapara wake.
Kama unaishi katika uzinzi na uasherati, yule unayeishi naye kama mume/mke ni nyapara wa ibilisi kwako, ndio maana dhambi inakutesa na huyo naye anakutesa, kwasababu wote mpo katika dhambi na ni hivyo hivyo katika dhambi nyingine zote…ni lazima shetani akupe nyapara juu yako.
Leo hii mkatae shetani na manyapara wake,..mkubali Bwana YESU upate uzima wa milele.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Ni kosa gani lililowafanya wana wa israeli wawe watumwa miaka 400 Misri?.
VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA
USIMWABUDU SHETANI!
Je Farao alikufa kwenye maji pamoja na jeshi lake au alipona?
Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu.
Rudi Nyumbani
Print this post