Maandiko hayaelezi moja kwa moja kifo cha Farao. Lakini baadhi ya hivi vifungu vinatuonyesha Farao alizama na jeshi lake katika bahari ya shamu.
Zaburi 136:15
[15]Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Kuonyesha kwamba sio tu jeshi lake, lakini pia pamoja na yeye..walizamishwa baharini.
Pia vifungu hivi…
Kutoka 14:28
[28]Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.
Maandiko hayo, hapo mwishoni yanasema hakusalia hata “mtu mmoja”. Ikiwa na maana hata Farao mwenyewe alikwenda na maji.
Lakini pia andiko linaendelea kusema zaidi…
Kutoka 15:19
[19]Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, BWANA akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.
Maana yake ikiwa kama magari yake mwenyewe yalizama baharini, ni uthibitisho kuwa hata na yeye mwenyewe alikuwa juu ya gari lake. Haiwezekani yeye kama mfalme aruhusu gari lake liende halafu abakie kwa miguu.
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba Farao alikufa katika bahari ile, pamoja na jeshi lake. Na Mungu ilimpasa awahakikishie wokovu kamili watu wake. Kwa kumwangamiza aliye kichwa cha adui zao. Kwasababu tangu mwanzo, masumbufu yote yalishinikizwa na Farao, hivyo alikuwa hana budi kuondolewa na yeye. Ili Israeli waufurahie wokovu mkuu wa Mungu.
Bwana akubariki.
Kutufundisha nini?
Mungu huwa anawahakikishia wokovu kamili watu wake, hata sasa tunao ukombozi mkamilifu ndani ya Yesu Kristo kwa kumwimini yeye, adui yetu shetani na mapepo yake yanafukuzwa,mbali na sisi. Lakini yatupasa tusiwe watu wa kutokuamini kama wana wa Israeli jangwani kwa kuishi kama wapagani, kwasababu ijapokuwa Mungu aliwaahidia nchi nzuri iliyobubujika maziwa na asali, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kuiingia isipokuwa wawili. Vivyo hivyo na sisi hatuna budi kuishindania Imani yetu. Ili tusionekane tumekosa kuingia kwenye ufalme wa Mungu wetu.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.
YONA: Mlango 1
Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?
USIMWABUDU SHETANI!
Rudi nyumbani
Print this post