Rubani ni nani katika biblia? (Ezekieli 27:8)

Rubani ni nani katika biblia? (Ezekieli 27:8)

Swali: Je zamani marubani wanaoendesha ndege walikuwepo kama tunavyosoma katika Ezekieli 27:8?


Jibu: Turejee mstari huo..

Ezekieli 27:8 “Wakaao Sidoni na Arvadi ndio waliovuta makasia yako; wana wako wenye akili, Ee Tiro, walikuwa ndani yako, ndio WALIOKUWA RUBANI ZAKE”.

“Marubani” wanaozungumziwa hapo si Marubani wanaorusha ndege kwamaana kipindi hicho ndege zilikuwa hazijavumbuliwa…bali marubani wanaozungumziwa hapo ni wana-maji (manahodha)..Kwasababu asili ya neno hilo rubani si mwana-anga, bali ni mwana-maji.

Isipokuwa kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda na kumavumbuzi mengi kuibuka, basi maneno mengi yanakuwa yanapata maana Zaidi ya moja.

Kwamfano katika biblia yametajwa magari (Mwanzo 45:21)..sasa magari ya zamani si sawa na haya sasahivi, ingawa yote ni magari… vile vile katika biblia kuna mahali pametajwa “Risasi” (Kutoka 15:10) lakini Risasi hiyo si sawa na hii inayojulikana sasa.. Vile vile pametajwa neno “Ufisadi“ (2Petro 2:7).. Lakini ufisadi huo wa biblia ni tofauti kabisa na huu unaofahamika sasa. N.k

Kwahiyo tukirudi katika Rubani, anayetajwa hapo katika Ezekieli 27:8, ni rubani mwana-maji, na si mwana-anga. Ndio maana ukiendelea mbele Zaidi katika mstari wa 29 utaona biblia imeweka sawa…

Ezekieli 27:29 “Na wote wavutao kasia, wana-maji, na RUBANI ZOTE WA BAHARINI, watashuka katika merikebu zao, na kusimama katika nchi kavu”.

Hapo anasema “Rubani zote za baharini” ikiashiria kuwa ni wana-maji na si wana-anga.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Risasi inayotajwa kwenye Ezekieli 27:12 ni ya namna gani?

Ufisadi una maanisha nini katika biblia?

EZEKIELI, ITABIRIE MIFUPA MIKAVU.

Mashonde ni nini? (Ezekieli 4:15).

Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments