Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)

Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)

Swali: Wenye kutia Kalafati ni watu gani?

Jibu: Neno “Kalafati” limeonekana mara mbili tu katika biblia, katika Ezekieli 27:9 na Ezekieli 27:27.

Na maana yake ni “Kamba nyembamba iliyotengenezwa kwa pamba” ambayo inawekwa katikati ya mianya ya mbao za merikebu, ili kuzuia maji yasipenye katika ile miunganiko. (Tazama picha juu)

Hivyo watu wanaofanya hiyo kazi ndio waliotajwa hapo katika Ezekieli 27:9,

Ezekieli 27:9 “Wazee wa Gebali na wenye akili wake walikuwa ndani yako, WENYE KUTIA KALAFATI; merikebu zote za bahari na mabaharia wao walikuwa ndani yako, ili kubadiliana biashara yako”.

Lakini habari hii inahusu nini?

Ukisoma kitabu hicho cha Ezekieli mlango wa 27 kuanzia mstari wa kwanza, utaona ni unabii unamhusu mfalme wa Tiro. (Kwa urefu kuhusu Taifa la Tiro fungua hapa >>>Miji ya Tiro na Sidoni ni miji gani kwasasa? 

Lakini hapa ni unabii wa Mfalme wa Tiro, Kwamba kwa kiburi chake na biashara zake nyingi alizozifanya juu ya nchi na katika bahari kupitia merikebu zake, siku inakuja ambapo ataanguka na kushuka chini kwasababu ya dhambi zake nyingi.

Na biashara za baharini alizokuwa anazifanya kupitia merikebu zake kubwa ambazo ndani yake kulikuwa na wana-maji, na “watiao Kalafati” na manahodha, zitaanguka na shughuli zao hizo zitaisha!

Ezekieli 27:27 “Mali zako, na bidhaa yako, na utajiri wako, wana-maji wako, na rubani zako, na WENYE KUTIA KALAFATI WAKO, na wafanya biashara wako, na watu wako wa vita wote, walio ndani yako, pamoja na jeshi lako lote lililo ndani yako, wataanguka katika moyo wa bahari katika siku ya kuangamia kwako”.

Ufunuo kamili pia kwa anguko la ulimwengu pamoja na dini zake za uongo katika siku za mwisho..

Ufunuo Ufunuo 18:2  “Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;

3  kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake………………..

9  Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake;

10  wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.

11  Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;

12  bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;

13  na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.

14  Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe.

15  Na wafanya biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza”

Je Umeokoka kwa kumwamini Bwana Yesu Kristo na kubatizwa, sawasawa na Marko 16:16?. Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho na Kristo amekaribia kurudi.

Kwa msaada Zaidi katika kumpokea Kristo fuatiliza sala hii ya Toba >>KUONGOZWA SALA YA TOBA  au wasiliana nasi kwa namba zetu zilizoanishwa mwisho wa somo hili.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

EZEKIELI, ITABIRIE MIFUPA MIKAVU.

Tarshishi ni mji gani kwasasa?

Mashonde ni nini? (Ezekieli 4:15).

Kuna tofauti gani kati ya  “Edeni” na “Adeni”?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments