KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

Wakati ambapo Israeli inapitia manyanyaso makali kutoka kwa wakaanani kwa miaka 20, mpaka yakawafanya wamlilie Mungu kwa nguvu ili awaokoe..Tunasoma kwenye biblia Mungu alisikia kilio chao akawanyanyulia mwamuzi Debora pamoja na baraka..

Hivyo Mungu akawaagiza wana wa Israeli wapange majeshi, ili wakapigane na adui zao, na hakika Bwana atawashindia..makabila mengi yalikubali kupeleka majeshi yao, lakini yapo makabila mengine hayakutaka kujishughulisha na jambo hilo..na hayo si mengine zaidi ya  Dani, Asheri, na nusu ya kabila la Manase na Gadi. Haya yote yalikuwa mbali kidogo na eneo la vita, Yaliona kama vile vita haviwahusu wao, hivyo yakawa bize kuendelea na mambo yao..

Waamuzi 5:17

[17]Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani, 

Na Dani, mbona alikaa katika merikebu? 

Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari, 

Alikaa katika hori zake.

Kwamfano kama hapo maandiko yanasema Dani alikaa katika merikebu, maana yake ni kuwa alikuwa ni mfanya biashara, aliona kuacha biashara zake za melini, za uchukuzi, na kwenda kujishughulisha na vita, ni upotezaji wa muda, kupigania taifa la Mungu ni kazi kichaa, wacha niendelee na biashara zangu..Na ndivyo hata hayo mataifa mengine yalivyokuwa, yalichowaza ni biashara, na mahangaiko ya hii dunia mpaka Agizo la Mungu likawa halina maana tena kwao, hata utumwa wa taifa lao hawakuuona, mateso na dhihaka taifa lao lilipokuwa linapitia hawakuona kama ni kitu zaidi ya biashara.

Ndipo Debora akaongozwa na Roho kutunga wimbo huo wa kuwashutumu ambao mpaka sasa tunausoma..

Hata sasa, tabia za makabila haya kama Dani zipo miongoni mwa wakristo wengi, ni mara ngapi utamwambia mkristo twende tukashuhudie, kwasababu tumeamuriwa kufanya hivyo na Kristo..lakini atakuambia sina muda, nipo buzy, sina mtu wa kumuacha kwenye biashara yangu…

Anaona biashara yake ni bora kuliko kuokoa roho za watu wanaopotea, huyu ni Dani anayekaa merikebuni..kipaumbele chake ni shughuli za huu ulimwengu, kazi, pesa, ndizo anazozitaabikia kutoka Januari mpaka Disemba, mwaka kwa mwaka, hana rekodi ya kufanya chochote kizuri  kwa ajili ya ufalme wa Mungu, lakini yupo tayari kujenga majumba, na mahoteli, na ma-meli ili kutanua wigo wake wa kibiashara..

Ni kweli Mungu anaweza kuokoa watu wake pasipo wewe, lakini vilevile kumbuka Mungu anaweza kubaki na mbingu yake pasipo wewe..usipokwenda mbinguni hakumpunguzii yeye kitu.

Hatushangai hata ni kwanini hili kabila la Dani halionekani miongoni mwa makabila ya Israeli yatakayookolewa siku za mwisho (Ufunuo 7:1-8). Sababu mojawapo ni hii..Na sisi tujichunguze tutambue kipaumbele chetu kwa kwanza ni kipi. Je siku ile tutakuwa na ujasiri wa kusimama mbele ya Kristo?

Bwana atupe kuliona hili.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.

Hori ni nini kibiblia (Waamuzi 5:17, Luka 2:7)?

Tarshishi ni mji gani kwasasa?

NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?.

NYOTA ZIPOTEAZO.

Kuna tofauti gani kati ya ‘Mungu’ na ‘Mola’?

NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments