Neno hori lina maana mbili, maana ya kwanza ni ile inayofahamika na wengi, kuwa eneo la kulishia mifugo.
Biblia inatuambia Bwana Yesu alipozaliwa, alilazwa katika hori la kulia ng’ombe, hivyo maana ya kwanza ya neno hili ndio hiyo.
Luka 2:7 “akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni”.
Maana ya pili ya neno hori ni mkono wa bahari. Yaani eneo la bahari au ziwa lililoingia nchi kavu, tazama picha juu.
Neno hilo utalipata katika vifungu hivi;
Yoshua 15:4 “kisha ukaendelea hata Azmoni, na kutokea hapo penye kijito cha Misri; na matokeo ya huo mpaka yalikuwa baharini; huu ndio mpaka wenu wa upande wa kusini. 5 Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hata mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani; 6 na huo mpaka ukaendelea hata Beth-hogla, kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Beth-araba; kisha mpaka ukaendelea hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni”;
Yoshua 15:4 “kisha ukaendelea hata Azmoni, na kutokea hapo penye kijito cha Misri; na matokeo ya huo mpaka yalikuwa baharini; huu ndio mpaka wenu wa upande wa kusini.
5 Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hata mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani;
6 na huo mpaka ukaendelea hata Beth-hogla, kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Beth-araba; kisha mpaka ukaendelea hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni”;
Yoshua 18:19 “kisha mpaka ukaendelea mbele ubavuni mwa Beth-hogla upande wa kaskazini; na matokeo ya mpaka yalikuwa katika ile hori ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, mwisho wa kusini wa mto wa Yordani; huo ndio mpaka wa upande wa kusini”.
Waamuzi 5:17 “Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani, Na Dani, mbona alikaa katika merikebu? Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari, Alikaa katika hori zake”.
Matendo 27:38 “Walipokwisha kushiba wakaipunguza shehena ya merikebu, wakiitupa ngano baharini. 39 Kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana”.
Matendo 27:38 “Walipokwisha kushiba wakaipunguza shehena ya merikebu, wakiitupa ngano baharini.
39 Kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana”.
Lakini tukirudi kwenye ile maana ya kwanza.
Ni kwanini Yesu alizaliwa katika hori la kulishia ng’ombe na si kwenye majumba ya kifahari? Ni kwasababu alikuwa ni sadaka iliyoandaliwa kuja kuchinjwa kwa ajili ya upatanisho wa dhambi za watu mbeleni, mfano wa ng’ombe au kondoo, hivyo ilimpasa na yeye azaliwe kule, kama ishara ya utumishi wake duniani.
Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. 6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. 7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake”.
Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake”.
Shalom.
Tazama maana za maneno mengine ya biblia.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Baghala ni nini katika maandiko?(2Wafalme 5:16).
Konzi ni nini?(Mhubiri 4:6)
Shokoa ni nini katika biblia?
https://wingulamashahidi.org/2020/09/24/rangi-ya-kaharabu-ni-ipi-kibiblia/https://wingulamashahidi.org/2020/09/24/rangi-ya-kaharabu-ni-ipi-kibiblia/
Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Jambo WATUMISHI.nimefurahiya haya masomo ya kuhusu maneno ya Mungu.ndio maana penda kama itawezekana tuwe natumiana masomo mengine ya kibinlia. Asante sana naishi Congo DRC