Kuna tofauti gani kati ya ‘Mungu’ na ‘Mola’?

Kuna tofauti gani kati ya ‘Mungu’ na ‘Mola’?

Swali: Je kuna tofauti gani ya Mola na Mungu, na je sisi wakristo ni sahihi kutumia Jina Mola badala ya Mungu?

Jibu: Neno Mola, limeonekana mara kadhaa katika biblia…

Matendo 4:24 “Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, MOLA, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo”

Yuda 1:4 “Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake MOLA, na Bwana wetu Yesu Kristo”.

Ufunuo 6:10 “Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, EE MOLA, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi”.

Maana ya MOLA ni  “Mungu-Mtawala”

Neno ‘Mungu’ maana yake ni “Muumbaji”, yaani aliyeumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.. lakini jina Mola limeingia ndani zaidi, kumtaja Mungu kama Mtawala,  Ni sawa na mtu anayesema “Mungu mwenyezi” badala ya “Mungu” au Mtu anayesema “Mungu mwenye Nguvu” badala ya “Mungu tu”. Mtu anayeomba kwa kumtaja Mungu pamoja na na sifa yake nyingine, hoja zake zinakuwa na Nguvu zaidi kuliko Yule anayetaja Mungu tu.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba, sisi wakristo ni sahihi kabisa kutumia neno Mola katika maombi yetu, kwasababu ni jina linaloelezea zaidi uweza wa Mungu, Ndio maana Wanafunzi walipokusanyika na kuomba baada ya Petro na Yohana kufunguliwa kutoka gerezani, maandiko yanasema pale walipokuwepo palitikiswa na wote wakajazwa Roho Mtakatifu na wakanena Neno la Mungu kwa ujasiri.

Matendo 4:24 “Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;

25 nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?………………..

31 HATA WALIPOKWISHA KUMWOMBA MUNGU, MAHALI PALE WALIPOKUSANYIKA PAKATIKISWA, WOTE WAKAJAA ROHO MTAKATIFU, WAKANENA NENO LA MUNGU KWA UJASIRI”.

Bwana Yesu akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MILANGO YA KUZIMU.

USIMLAANI KIZIWI, WALA USITIE KWAZO MBELE YA KIPOFU.

Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?

MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.

Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments