Nini maana ya “Atamwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”. (2Wathesalonike 2:8).

Nini maana ya “Atamwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”. (2Wathesalonike 2:8).

Jibu: Tusome,

2 Wathesalonike 2:8 “Hapo ndipo atakapofunuliwa yule ASI ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza KWA UFUNUO WA KUWAPO KWAKE

Andiko hili linamhusu Mpinga Kristo ambaye maandiko yanasema katika siku ya mwisho Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kwa ufunuo wa kuwapo kwake (vitu hivyo viwili).

Sasa ufunuo wa kuwapo kwake unaozungumziwa hapo, sio ufunuo wa kuwepo kwa mpinga Kristo.. La! Bali sentensi hiyo inamaanisha kuwa mpinga-Kristo ataangamizwa kwa  kule kudhihirishwa (au kufunuliwa) kwa Bwana Yesu katika utukufu wake, au kwa lugha nyingine rahisi ni kwamba ule Mwako wa utukufu Kristo atakaokuja nao, utamwangamiza mpinga Kristo. Hiyo ndio maana ya (ufunuo wa kuwapo kwake).

Sasa ni wakati gani ambapo Bwana Yesu atamwua kwa kinywa chake na kwa kufunuliwa kwake?.

Tusome Ufunuo 1:13-16

Ufunuo 1:13 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

12 NA MACHO YAKE YALIKUWA KAMA MWALI WA MOTO, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

15 NA UPANGA MKALI HUTOKA KINYWANJ MWAKE ILI AWAPIGE MATAIFA KWA HUO. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA”.

Umeona hapo?..

Kwa huo utukufu Bwana atakaokuja nao wa macho kama miali ya moto na upanga unaotoka katika kinywa chake (kwa mfano wa pumzi) hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kusimama mbele yake, akiwemo mpinga Kristo…kwasababu yeye (Bwana Yesu) ni Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.

Je umeokoka?..kwa kutubu dhambi zako na kumaanisha kuziacha?. Kama bado unasubiri nini?..Huyu Yesu anayekuja leo kwako kwa sauti ya upole, fahamu kuwa hatakuwa hivyo siku zote..

Kuna wakati utafika atakuwa ni hakimu, na mhukumu, na atayapiga mataifa na kuyaadhibu.

Si jambo jema kuifikia hiyo siku, kwasababu ni siku ya hasira ya Mungu, ni heri tuyasalimishe maisha yetu kwake ili tuwe salama katika siku za mwisgo.

Maran atha!.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NI VIZURI SISI KUWAPO HAPA.

HIZO NDIZO ROHO ZA MASHETANI.

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

USIISHIE TU KUPATA HAKI, BALI PATA NA WOKOVU.

YESU HAYUPO KATIKA MAZINGIRA YALEYALE TU SIKUZOTE, USIJISAHAU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments