MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.

MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.

Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze Biblia.

Je!, wewe ni Mwanamke?..kama ndio! basi fahamu kuwa upo katika hatari kubwa ya kuingiwa na roho za mapepo kuliko mwanaume!.

Hebu tutafakari mstari ufuatao, na kisha tujiulize maswali machache!.

1Timotheo 2.11 “Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.

12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.

14 WALA ADAMU HAKUDANGANYWA, ILA MWANAMKE ALIDANGANYWA KABISA AKAINGIA KATIKA HALI YA KUKOSA”.

Hapo katika mstari wa 14, anasema “ADAMU HAKUDANGANYWA, ILA HAWA ALIDANGANYWA KABISA AKAINGIA KATIKA HALI YA KUKOSA”.

Maana yake pale Edeni, “Adamu hakudanganywa kabisa”…Adamu alikuwa anajua anachokifanya, alikubali kula lile tunda alilolipokea kutoka kwa mke wake, akiwa na akili timamu na..akijua kabisa lile ni kosa!..lakini Hawa alikuwa hajui chochote, yeye aliamini kile alichoambiwa na Nyoka ni ukweli mtupu!.hivyo alidanganywa na shetani..

Hiyo ikifunua kuwa kuna “KUNA UDHAIFU MKUBWA SANA KATIKA JINSIA YA KIKE”.

Utakumbuka tena, kipindi mfalme Sauli, alipoachwa na Mungu, kitu cha kwanza alichofikiria kukifanya ni kumtafuta mwanamke mwenye pepo la utambuzi katika nchi yake ile?

1Samweli 28:6 “Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.

7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, NITAFUTIENI MWANAMKE MWENYE PEPO WA UTAMBUZI, NIPATE KUMWENDEA NA KUULIZA KWAKE. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.

8 Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako”.

Jiulize hapo ni kwanini aseme “NITAFUTIENI MWANAMKE MWENYE PEPO, NA SI MWANAUME mwenye pepo la utambuzi”?.. Si kwamba wanaume wachawi hawakuwepo, walikuwepo!… Lakini Sauli alijua kuna utofauti wa Mwanaume mwenye pepo, na Mwanamke mwenye pepo!… Alijua mwanamke mwenye pepo, anakuwa na pepo kweli kweli!..tofauti na mwanaume!.

Utaona tena kipindi akina Paulo wapo kule Filipi, walikutana na Mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, ambaye alikuwa anawatabiria watu na kuwapatia faida mabwana zake..

Matendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, KIJAKAZI MMOJA ALIYEKUWA NA PEPO WA UAGUZI AKATUKUTA, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.

17 Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.

18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.

19 Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji”.

Umeona?.. Ukizidi kujifunza biblia utakutana na maandiko yanayosema “Usimwache mwanamke mchawi kuishi (Kutoka 22:18)”… Jiulize ni kwanini inataja mwanamke na si mwanaume?…Sio kwamba haijawaona wanaume ambao ni wachawi!.. walikuwepo wanaume wachawi wengi, lakini kundi la wanawake ndilo lililokuwa limezama zaidi na ndilo lilikuwa hatari..

Sio ajabu kwanini unaona  hata leo hii,..Wanawake ndio wanaoongoza  kulipuka mapepo!. Hiyo ni kutokana na kwamba, ni rahisi kufungua milango ya roho zao zaidi ya wanaume!.

Maana yake ni kwamba…Kila kitu chochote kinachokuja mbele wanawake wengi ni rahisi kukiamini, pasipo kukifanyia uchunguzi wa kutosha, kila wazo linalokuja ni rahisi kulipokea bila kulifanyia uchunguzi wa kutosha, kila fundisho linalokuja ni rahisi kuliamini pasipo kulifanyia uchunguzi wa kutosha…mwisho wa siku wanajikuta wanaingiwa na roho nyingi zidanganyazo, na wanatumika na roho nyingi, pasipo wao wenyewe kujijua..

Mwanamke, si kila wazo linalotoka kwa Mume wako ni la kulipokea pasipo kulitafakari kwa kina, si kila fundisho ni la kuliamini pasipo kulichunguza mara mbili mbili.. Fahamu kuwa wewe ni lango kubwa na la kwanza dhaifu, ambalo shetani analitazama zaidi ya wanaume. Wanawake wengi wa siku hizi za mwisho ni wavivu wa kuyatafakari maandiko kwa kina.. ingawa sio wote!, lakini asilimia kubwa wapo hivyo, na pasipo kujijua kuwa wao ndio ndio windo kubwa na la kwanza la mapepo na roho zote za mashetani zaidi ya wanaume!..

Asilimia kubwa ya wanapenda kufuata mambo au kuamini mambo kwa kusikia tu!.. Kwa mfano kukizuka jambo Fulani ambalo linawafuasi wengi, wanawake wengi ni rahisi kuamini jambo hilo na kulifuata, pasipo kulichunguza kwa kina, au kulifuatilia..na huko huko ndiko wanakojikuta wameshafungua milango ya maroho ya mapepo ndani yao, bila wao wenyewe kujijua.

Baada ya kujijua kuwa wewe ni windo la roho za mapepo zaidi ya jinsia nyingine basi huna budi kuchukua tahadhari kubwa sana juu ya maisha yako, kwa kufanya jambo lifuatalo!.

JARIBU MAMBO YOTE.

Maandiko yanasema  katika kitabu cha 1Wathesalonike 5:21 “ jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema”.. Hapo anasema “jaribuni” pasipo kuonyesha jinsia,.. ikiwa na maana kuwa ni jukumu la jinsia zote “kujaribu mambo”.. Na sio kujaribu jambo moja tu bali “ kujaribu yote”.. Hata ushauri unaopewa na mtu wa kazini kwako, huna budi kuujaribu, hata habari unayoletewa na rafiki yako, huna budi kuijaribu!!..Hata habari unayoisikia katika redio au Tv, ijaribu..

1Yohana 4:1 “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”.

Kwanini tunajaribu kila kitu tunachokisikia?? Kwasababu “MANENO” ni “roho”..kila maneno tunayoyasikia yana roho ndani yake.. Hata Neno la Mungu ni Roho wa Mungu..tunaposikia maneno ya Mungu, maana yake tunampa nafasi Roho wa Mungu kusema ndani yetu. Sasa Utasema hilo tunalithibitisha vipi?..

Yohana 6:63 “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; MANENO HAYO NILIYOWAAMBIA NI ROHO, tena ni uzima”.

Umeona?.. Bwana Yesu anasema, maeneno ninayowaambia ni ROHO..  kadhalika tunaposikiliza mambo mengine nayo pia ni roho. Ndio maana hatuna budi kujaribu kila kitu tunachokisikia.. kama Bwana alivyosema katika..Luka 8:18 “Jiangalieni basi jinsi msikiavyo….”

Na tunayajaribu mambo kupitia nini?… Si kingine zaidi ya NENO LA MUNGU.

Biblia ndio Hadubini ya maisha yetu.. ndio kipimo cha mambo yote..Maana yake kama hupendi kujifunza biblia, kamwe hutaweza kuzipima roho, kama hujizoezi kujifunza biblia mwenyewe bila kusubiria kufundisha fundisha kila mara, kamwe hutaweza kuzijaribu roho kama zinatokana na Mungu au la!..Kama wewe ni wa kusubiria tu makala Fulani iachiwe usome, au mahubiri Fulani uyasikilize, ni wa kupenda kuletewa letewa tu!…wewe mwenyewe biblia unaiona ngumu fahamu kuwa wewe ni windo bora la mapepo!.

Mwanafunzi anayeona masomo ni magumu, siku zote ni Yule ambaye hapendi kusoma, bali yule anayependa kusoma anapoona mada ni ngumu, basi anafanya bidii kupambana mpaka aielewe…na kamwe hawezi kuona masomo ni magumu… vile vile na wewe kama unaona biblia ni NGUMU miaka nenda rudi!.. Basi huo ni uthibitisho kuwa wewe si mwanafunzi wa biblia, hujawa serious!!.. ndio maana inakuwa ni ngumu kwako!.. miaka na miaka.

Hivyo kama wewe ni mwanamke, kumbuka haya, na fahamu kuwa mapepo yanakutafuta wewe zaidi zaidi ya jinsia nyingine, hivyo huna budi kuongeza umakini katika kujilinda na hizo roho.. lakini kama hutaongeza umakini kwa kuamua kujifunza BIBLIA kwa kina!!, na kupima mambo yote!!! Basi jua kuwa roho za mapepo zitakusumbua daima..na mapepo mengine yatakuingia pasipo wewe kujua, lakini utakuja kuona madhara yake baadaye sana.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.

NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.

ONDOKA YESU, TUACHIE MAPEPO.

NI KIPI KINAMZUIA MUNGU KUZUNGUMZA NA SISI?

MFANYE BWANA YESU MWENYEJI MAISHANI MWAKO.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments