USIOGOPE KUMWADHIBU MWANAO.

USIOGOPE KUMWADHIBU MWANAO.

Tunaishi katika ulimwengu ambao, maadili yameporomoka sana, na bado yanaendelea kuporomoka kwa vijana na watoto..Na hiyo inatufanya tuelekeze lawama kwa watoto; tukisema watoto wa siku hizi wamebadilika sana, lakini ukweli ni kwamba wazazi ndio wamebadilika, watoto ni walewale.

Malezo ya mzazi kwa mtoto ni muhimu sana, mtoto si kama nyau, ambaye kitu pekee anachohitaji ni chakula tu na sehemu ya kulala, hata ukimwacha mwaka mzima bila kumjali kwa vingine, hakuna hasara yoyote, bado ataendelea kuwa paka..

Lakini kwa mwanadamu sivyo..yeye hafugwi, bali analelewa..na malezi ni zaidi ya chakula na nguo na mahali pa kulala.. Hapo ndipo wazazi wengi wanashindwa kuelewa.

Kwasababu mtoto atahitaji kuwa na maarifa, nidhamu, uadilifu, hekima, busara, upendo, utiifu, upambanuzi n.k. Ili aweze kuishi vema katika huu ulimwengu.

Hivi vyote hazaliwi navyo, bali anajifunza anapokuwa duniani..hivyo akikosa msaada sahihi, basi ibilisi atatumia fursa hiyo kumfundisha elimu yake na nidhamu yake hapa ulimwenguni.

Hivyo wewe kama mzazi au mlezi una jukumu kubwa sana zaidi ya lile la kumlisha na kumvisha na kumsomesha..hizo ni hatua 3 katika ya 1000, anazopaswa azijue.

Ikiwa hukupata masomo yaliyotangulia ya malezi ya watoto, basi waweza kututumia ujumbe kwa namba hii, ili tuweze kukutumia chambuzi za nyuma. Au tembelea website yetu hii www.wingulamashahidi.org. au tutumie ujumbe kwa namba hizi +255693036618

Leo tutaona njia nyingine ya kumlea mtoto vema.

Na njia yenyewe si nyingine zaidi ya kutumia KIBOKO.

Lugha hii inaweza isiwe nzuri masikioni mwa wazazi lakini ni tiba nzuri kwa malezo yao. Hata ‘panadol’ haina ladha nzuri mdomoni, lakini pale inapotutibu tunaishukuru, ndio maana tunayo siku zote majumbani kwetu.

Lakini ni kwanini utumie kiboko kwa mtoto?

Sababu zipo mbili.

1) Ni kwasababu ujinga umefungwa moyoni mwake

2) Mungu naye huwa anatuadhibu sisi.

  1. Tukianzana na sababu ya kwanza biblia inatuambia..

Mithali 22:15

[15]Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.

Ni vizuri ukafahamu kuwa mtoto kama mtoto huwa ana ujinga mwingi ndani yake..yule si kama wewe, unapoona anang’ang’ania kitu fulani kisichopendeza halafu wewe kama mzazi unaamua tu kumwachia kisa anakililia, usidhani kuwa anaelewa matokeo ya kile anachokitaka..

Kumbuka yule hatafakari, wewe unatafakari, hivyo basi ukimsikia anatukana, usisubiri apumzike bali hapo hapo shika kiboko chapa. Ukiona unamwagiza kitu hatii, chapa..ukiona hawaheshimu watu wazima hata baada ya kuonywa mara nyingi..chapa..usiogope labda atakufa…biblia inasema kiboko cha adili hakiui..

Mithali 23:13

[13]Usimnyime mtoto wako mapigo; [14] Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.

Hiyo itamsaidia sana kuundoa ujinga mwingi wa kipepo ambao mwingine kwa maneno tu, peke yake au kwa kufundishwa hauwezi kutoka..

  • 2) Mungu naye anatuadhibu.

Na sababu ya pili kwanini tuwaadhibu watoto wetu kwa kiboko pale wanapokosea..ni kwasababu Mungu naye anatuadhibu sisi watoto wake.

Biblia inasema hivyo..

Waebrania 12:6-7

[6]Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.

[7]Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?

Umeona..Sisi hatuna hekima ya kumzidi Mungu, tengeneza picha Bwana angekuwa anatuona tunatukana wengine halafu hachukui hatua yoyote anacheka tu..si tungaangamia..Mungu alipomuona Daudi anamchukua mke wa Huria halafu anaendelea kusema wewe ni mtumishi wangu unayeupendeza moyo wangu..Daudi leo angekuwa wapi kama sio kuzimu? Lakini Mungu alimuadhibu vikali…na baadaye akatubu akapona..

Nasi pia biblia inatuambia tutakuwa wakamilifu kama Baba yetu wa mbinguni alivyomkamilifu..(Mathayo 5:48)

Mzazi unayemtazama mwanao, anafanya ujinga, unaogopa kumchapa atalia..bado hujawa mkamilifu kama Mungu.

Hivyo anza sasa kutimiza huduma hii, ili kesho mtoto huyo afanyike baraka na neema kwa ulimwengu.

Lakini zingatia: Haimaanishi kuwa umpige pige mtoto ovyo kila saa anapokosea..hapana zipo sehemu zinastahili kiboko, zipo zinazostahili maonyo, zipo zinazostahili kuelimishwa..Zote zina umuhimu wake mkubwa bila kupuuzia hata moja.

Bwana akubariki

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.

KILEMBA CHA NEEMA, JE! UMEMVIKA MWANAO?

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?

NI NINI KINATOKA KINYWANI MWA MTOTO WAKO?

MALEZI YA MTOTO MCHANGA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments