JINSI YA KUISHINDA DHAMBI INAYONITESA.

JINSI YA KUISHINDA DHAMBI INAYONITESA.

SWALI: Shalom. Naomba kufahamu nifanye nini ili niweze kuishinda ile dhambi inayonitesa.?


JIBU: Dhambi inayomtesa mtu kwa jina lingine inaitwa “dhambi izingayo kwa upesi”, ambayo tunaisoma katika;

Waebrania 12:1

[1]Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

Si kila dhambi, huwa inaondoka kirahisi ndani ya mtu pindi anapookoka..

Ni kweli asilimia kubwa ya dhambi mtu anajaliwa na Roho Mtakatifu kuziacha wakati ule anapotubu, na na kudhamiria kumfuata Yesu kwa moyo wake wote, kwamfano mwingine alikuwa ni mwizi, mwongo, mshirikina, mzinzi n.k.

Lakini alipookoka hivi vyote akaviacha kiwepesi kabisa..Lakini ndani yake kukawa na shinikizo kubwa la kuendelea kufanya punyeto, au mawazo machafu kumtawala..hivyo hiyo hali ikawa inamtesa  kwa kipindi kirefu na kumfanya akose raha, wakati mwingine amejaribu kuomba sana lakini hali ipo vilevile.

Mwingine hayo yote ameweza  kuyashinda lakini dhambi ya usengenyaji imekuwa ni mzigo mzito sana kwake kuutua, mwingine ulevi, mwingine kutazama picha za ngono n.k.

Ndugu ikiwa umeokoka na unaona hiyo dhambi ni kikwazo kikubwa  kwako, nataka nikuambie huna budi kushindana nayo hadi uishinde..kwasababu usipoishinda itakupeleka jehanamu.

Kaini alikuwa na dhambi ya hasira na wivu, akaipuuzia, lakini  Mungu akamwambia, unapaswa uishinde

Mwanzo 4:6-7

[6]BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?

[7]Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.

Dhambi kama hizi huwa zilishatia mizizi mrefu ndani ya mtu tofauti na nyingine, hivyo kuziondoa inahitaji nguvu ya zaida..

Na njia pekee ya kuzishinda hizi ni moja tu nayo ni “kwa Kuua vichocheo vyote vinavyokupelea kuitenda dhambi hiyo”..

Mithali 26:20 Inasema;

“Moto hufa kwa kukosa kuni;..”

Moto hauwezi kuendelea muda mrefu mahali ambapo hapana kichocheo chake kama kuni au mafuta..haijalishi utakuwa na nguvu kiasi gani, mwishowe utazima tu.

Hakuna dhambi yoyote iliyo ngumu kuishinda hapa duniani endapo vichocheo vyake vitauliwa kikamilifu.

Kwa mfano kufahamu ni jinsi gani utaweza kuishinda dhambi ya uzinzi fungua hapa..>>> MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO

Kwa siku za mwanzo, utaona ni shida lakini kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda Mungu anakutia nguvu na hatimaye inakuwa ni dhambi nyepesi sana kuishinda kuliko hata zote…

Ni kawaida hata hata gari lililo katika mwendo kasi likichuna breki kwa ghafla, haliwezi kusimama hapo hapo…litasogea mbele kidogo, ndipo litulie japokuwa tairi tayari zilishaacha kuzunguka, kitambo kidogo.

Vivyo hivyo na wewe katika hiyo dhambi inayokuzinga kwa upesi, inayokufanya usipige mbio kwa wepesi, katika safari yako ya ukristo, kwa siku za mwanzoni itaonyesha  kama kuleta ukinzani lakini kwa jinsi unavyokaa mbali na vichocheo vyake hatimaye itakufa tu ndani ndani yako…ni kitendo cha muda.

Kwamfano kama wewe ni mvuta sigara, kiu ya kuvuta ikija, ondoka mazingira ya upatikanaji wake, vilevile wale marafiki uliokuwa unavuta nao jitenge nao waone kama kaburi, hicho kiu kitakutesa tu kwa muda mfupi, lakini uking’ang’ana utakuja kushangaa kimetoweka tu ghafla..hapo ndio tayari kimekufa..

Shindana, hadi ushinde…usikubali kusema mimi nimeshindwa kuacha hiki au kile, usikubali hiyo hali, usiwe mnyonge wa dhambi, kwasababu wanyonge wote hawataurithi uzima wa milele biblia inasema hivyo katika Ufunuo 21:27

Ikiwa ni fashion, wewe kama mwanamke ni lazima uishinde, ikiwa ni kamari, ikiwa ni miziki ya kidunia kanuni ni hiyo hiyo…Ua vichocheo vyote. Kaa mbali nayo, ulizoea kutazama picha za ngono mitandaoni, na ulipookoka mawazo yale yanajirudia rudia kwenye fahamu zako, endelea kukaa mbali na vichocheo hivyo, acha mazungumzo mabaya, left magroup masiyokuwa na msingi kwako, epuke kutazama au kusikiliza kitu chochote chenye maudhui ya uzinzi, marafiki wazinzi waepuke, marafiki wasiokuwa na maana wa jinsi tofauti wapeuke, utafika wakati hayo mawazo machafu yatakukimbia..

Zingatia hayo, na matokeo utayaona.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JINSI YA KUSOMA BIBLIA.

MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)

YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.

CHUKIZO LA UHARIBIFU.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita.

JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
MOHERE ERICK CHACHA
MOHERE ERICK CHACHA
1 year ago

Na barikiwa Sana na mafundisho ya neno la Mungu