SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.

Nyuma kidogo nilikuwa nadhani mtu mwenye mapepo, ni lazima yalipuke, na ikiwa hayalipuka, basi hana mapepo ndani yake. Kumbe mtazamo huu sio sahihi. Tunapaswa tujue kuwa mtu yeyote ambaye hayupo ndani ya Kristo kwa namna moja au nyingine lipo pepo ambalo linaishi ndani yake, aidha kwa kujua au kwa kutokujua, haijalishi kuwa litamlipuka au halimtalipuka.

Biblia inatufundisha hivyo, Si wakati wote Mapepo yote yaliyokutana na Yesu yalilipuka, au yalitolewa kwa kukumewa kama tunavyodhani.. Embu tusome habari hii pengine ulishawahi kuisoma mara nyingine lakini jambo hili hukulijua..tusome.

Luka 13:10 “Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo.

11 Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa NA PEPO WA UDHAIFU muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.

12 Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako.

13 Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu”.  

Kwa mistari hiyo michache tunaweza kusema, Yesu alijua kabisa huyu mama kilichokaa nyuma yake si kingine zaidi ya Pepo, na hilo pepo nalo lilijua kabisa aliyesimama mbele yake ni Yesu mkuu wa uzima. Lakini pepo hili limekaa nyuma ya kivuli cha udhaifu, nyuma ugonjwa wa kibiongo, wala halipigi kilele, wala halijidhihirishi kama ilivyo desturi yao. Ndipo Yesu akamwita, akamwekea mikono yake, na hilo pepo likaondoka saa ile ile, na mama yule akawa mzima.

Lilipotoka Mama huyu hakujua chochote, kwasababu hakugarara chini, au hakupiga kelele, kilichomfanya ajue kuwa pepo limeondoka na mabadiliko ya ghafla aliyoanza kuyaona katika mwili wake baada ya pale.

Nachotaka kusema ni kuwa, nguvu za giza hazichagui wa kumwingia, maadamu upo nje ya “himaya ya Kristo Yesu” hayatakosa mahali popote tu pa kukaa, panaweza pasiwe katika ugonjwa, panaweza pasiwe katika mwili, utaenda kanisani kama kawaida, mtafanya maombi ya nguvu pengine, na wala lisilipuke pepo lolote. Lakini linaweza likakukaa katika ulevi, likakukaa katika uzinzi, likakukaa katika wizi, likakaa katika usengenyaji  n.k. Au katika tabia fulani ambayo wewe mwenyewe inakushinda. Na hayo yote hutajua kama yalikuwa ndani yako mpaka utakapookolewa na Yesu.

Lakini kama upo ndani ya wokovu Pepo haliwezi kuwa na nafasi ndani yako.

Hivyo wewe unayeusoma ujumbe huu, na hujaokoka pengine ulikuwa hujui kuwa kuna maroho ya giza yamekuzunguka kwenye maisha yako. Na leo umejua, basi fahamu kuwa njia pekee ya kuzishinda roho hizo, ni kwa kujikabidhi kwa Bwana Yesu.  Yeye pekee kwa damu yake iliyomwagika pale msalabani ndiyo yenye nguvu ya kuweza kuondoa na anayeweza Kufuta laana yote ya dhambi iliyokuwa juu yako, pamoja na kufukuza miungu yote migeni inayoishi humo nafsini mwako. Ikiwa tu utakubali leo hii kutubu, na kuyasalimisha maisha yako kwake kikamilifu, kwa kumaanisha kabisa kutoka katika moyo wako, kwamba hutorudi nyuma tena. Basi leo hii anaweza kukusamehe kabisa.

Hivyo Kama upo tayari kwa hilo hii, basi fuatisha sala hii fupi kwa imani, ukijua kuwa Mungu anakusikia, na kwa kufanya hivyo Bwana ataanza kuunda jambo jipya katika maisha yako, kuanzia leo. Fungua tu moyo wako.

Mahali ulipo jitenge kasha piga magoti sehemu ya utulivu kisha Sema maneno haya;

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE IONDOE UOVU WANGU WOTE SASA NDANI YANGU, NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa sala hiyo imetoka moyoni mwako, ujue kuwa hiyo ni hatua ya kwanza, kuelekea kufanywa huru kweli kweli na Bwana Yesu. hatua inayofuata kwako ni kupokea Ubatizo sahihi, ambao ni ule wa kuzamishwa katika maji tele (Yohana 3:23) na uwe katika jina la BWANA YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38,8:16,10:48,19:5.  Na ukilikamilisha hilo kuanzia hapo Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.

Hivyo kama utakuwa tayari kwa ajili ya Tendo hili la ubatizo ambalo ni maagizo la msingi tuliyopewa na Bwana wetu Yesu Kristo kwamba kila aaminiye na kubatizwa ataokoka.(Luka 16:16), itakuwa ni vema sana. Hivyo wewe tayari umeshaamini, hatua iliyobaki kwako ni kubatizwa. Usipuuzie agizo hilo. Tafuta ubatizo sahihi kwa ajili ya kuukamilisha wokovu wako.

Kama utakuwa tayari kwa tendo hilo, basi wasiliana na sisi, inbox au kwa namba hizi hapa chini, tujue pa kukusaidia kwa mahali ulipo. +255693036618 / +255789001312,

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hapo juu.

Mada Nyinginezo:

YESU MPONYAJI.

FAHAMU JINSI KRISTO ANAVYOPONYA WATU ROHO.

NYAYO TUNAZOPASWA KUZIFUATA.

RABI, UNAKAA WAPI?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 6

TUMEPEWA AMRI YA KUKANYAGA NGE NA NYOKA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Rowland Asante Robert
Rowland Asante Robert
2 years ago

Naelewa Sana! Pepo SI lazima apige kelele. Blessings