Mlima wa Mizeituni  unaumuhimu gani kwetu?

Mlima wa Mizeituni  unaumuhimu gani kwetu?

Mlima wa Mizeituni ni moja ya milima saba ambayo inauzunguka mji wa Yerusalemu kule Israeli . Mlima huu upo upande  wa Mshariki mwa mji huo,  umbali usiozidi kilometa moja, mpaka kuuingia mjini Yerusalemu. Hivyo haupo mbali sana.

Umeitwa mlima wa Mizeituni, kutokana na kuwa na sifa ya kuzungukwa na miti mingi ya mizeituni pembezoni mwa mlima huo.

Mlima huu umetajwa mara mbili katika agano la kale, mara ya kwanza ni siku ile Daudi alipokuwa anafukuzwa na mwanawe Absalomu, biblia inatuambia aliupanda mlima huu akiwa analia peku, akiambatana na wale watu aliokuwa nao kwenye ufalme.(2Samweli 15:30).

Sehemu nyingine ni katika kitabu cha Zekaria ambacho kinaeleza unabii wa masihi siku atakaposhuka mara ya pili hapa duniani, kwamba atashukia kwanza juu ya mlima huu;

Zekaria 14:3 “Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita.

4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini”.

Lakini katika agano jipya mlima huu umetajwa mara nyingi kidogo;

Lakini cha kufahamu zaidi ni kuwa habari zote ambazo  Yesu Kristo alizitaja kuhusiana na siku za mwisho na kurudi kwake mara ya pili duniani, alizizungumzia juu ya mlima huu wa mizeituni. Utasoma hayo katika (Mathayo 24, Marko 13, Luka 21)

Hata  siku ile Yesu alipoulilia mji wa Yerusalemu, juu ya maangamizi yake yaliyo mbeleni, alikuwa amesimama juu ya mlima huu.(Luka 19:37-44)

Na juu ya mlima huu, ndio aliopaa kutoka ulimwenguni, mara ya mwisho  alipokutana na wanafunzi wake baada ya siku zile 40 na kuwapa maagizo ya kuhubiri injili, na kuingojea ahadi ya Roho Mtakatifu..

Matendo 1:9 “Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.

10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,

11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni”.

JE! MLIMA HUU UNAO UMUHIMU WOWOTE KWETU? NA JE! NI SAHIHI KWENDA KUOMBA JUU YA MLIMA HUU?.

mizeituni, mlima,

Ni wajibu wetu kujua kuwa huu ndio mlima ambao Kristo atashukia siku ile atakaporudi mara ya pili kuuhukumu ulimwengu na kutawala kama mfalme. Na kama tulivyosoma katika unabii wa Zekaria ni kwamba siku hiyo atakapokuja, mlima huu utagawanyika katikati, upande wa Mashariki, na Upande wa Magharibi, na hapo katikati kutakuwa na bonde kubwa sana. Siku hiyo  atauwa waovu wote watakaokuwepo duniani kwa wakati huo.. Kipindi hichi ndio kile biblia inasema  kila jicho litamwona, na mataifa yote watamwombolezea, watu watatamani milima iwaungukie kwasababu watauliwa na Kristo mwenyewe. (Mambo hayo watakutana nao wale watakaoukosa unyakuo)

Kwa urefu wa somo hilo fungua hapa >>WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA;

Na baadaye akishawamaliza waovu wote ataingia  mji wa Yerusalemu, na kisha atatawala kama Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana, juu ya dunia nzima kwa muda wa miaka 1000,

Ataitengeneza upya hii dunia, kutakuwa na amani ya milele isiyoelezeka. Dunia itakuwa kama paradiso. Na wakati huo upo karibuni sana. Hivyo ni wajibu wetu sisi sote kujua mambo yatakayoendelea Israeli katika siku za mwisho, ikiwemo juu ya mlima huu wa mizeituni, ili tujue  leo hii tunasimama wapi. Tusiishi tu kama watu wengine wa ulimwengu, wasioona mambo ya mbeleni.

Lakini sasa tukirudi kwenye sehemu ya pili ya swali letu  je! Ni Sahihi kwenda kuomba juu ya mlima huu?

Watu wengi wamekuwa wakienda Yerusalemu, kupeleka maombi yao, wakidhania kuwa mahali pale ndipo Mungu atawasikia vizuri zaidi kuliko huku walipo, wengine wamekuwa wakikesha kwenye ule ukuta wa maombolezo, wengine juu ya mlima huu wa Mizetuni, wengine kwenye mto Yordani n.k..

Lakini ukweli ni kwamba kufanya hivyo ni kukosa maarifa ya kutosha juu ya agano tulilo nalo leo hii. Bwana Yesu alimwambia Yule mwanamke;..

Yohana 4:21 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu….

4.23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.

Agano la Damu ya Yesu, ni agano la kimbinguni, kiasi kwamba mtu yeyote mahali popote atasikiwa na Mungu ikiwa tu ataingizwa katika agano hilo lililo bora. Na Mtu ataingia ndani ya agano hilo, kwanza kwa kumwamini Yesu Kristo, kisha kutubu dhambi zake, na baada ya hapo kuwa tayari kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. Akikamilisha hatua hizo anakuwa ameshaokoka.

Na mtu kama huyo maombi yake yanasikiwa, ziadi hata mtu aliyekwenda kuomba juu ya mlima huu.

Je! Wewe umeingizwa kwenye agano hili?. Je! Una habari kuwa Yesu Kristo yupo mlangoni kurudi? Na unabii huo upo mlangoni kutimia? Unasubiri nini usimkaribishe Kristo moyoni mwako. Bado unatangatanga na ulimwengu ili siku ile ikujie ghafla?.  Mambo yatakayoendelea huku duniani kwa watakaoukosa unyakuo hayaelezeki ndugu yangu, Ni heri leo ukayakabidhi maisha yako kwa Yesu. Kama moyo wako leo hii upo tayari kufanya hivyo. Basi uamuzi huo ni wa busara sana. Hivyo fungua hapa kwa ajili ya kupata maelekezo ya sala ya Toba.  >>> SALA YA TOBA

Na Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

UFUNUO: Mlango wa 20

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

UTAWALA WA MIAKA 1000.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Manase Gaspar
Manase Gaspar
1 year ago

Nimebariliwa sana na fundisho Hili. MUNGU azidi kuwafanikisha na kuwatumia kwa utukufu wake