MILANGO YA KUZIMU.

MILANGO YA KUZIMU.

Milango ni wingi wa neno “mlango”..( Malango na Milango), ni neno moja. Katika biblia tunasoma Neno hilo likitajwa na Bwana Yesu..

Mathayo 16:18 “ Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; WALA MILANGO YA KUZIMU HAITALISHINDA.

19  Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”.

Tunasoma Mamlaka hayo alipewa Mtume Petro,  na Mitume wengine pia walipewa mamlaka kama hayo (soma Yohana 20:23).

Sasa Mlango maana yake ni maingilio ya mahali, Vitu au watu wanaingia ndani ya nyumba au ndani ya mji kupitia milango yake, hakuna namna wanaweza kupitia kwingine.

Kwahiyo Kristo aliposema atalijenga kanisa ambalo milango ya kuzimu haitalishinda, Maana yake ni kwamba kanisa Bwana Yesu atakalolijenga, litakuwa na nguvu dhidi ya Milango yote ya kuzimu.

Sasa Milango ya kuzimu ni ipi?

Milango ya kuzimu ni mambo yote ambayo yanayompa mtu tiketi ya moja kwa moja kuingia kuzimu. Ifuatayo ni baadhi tu!

1Wakorintho 6:9  “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? MSIDANGANYIKE; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,

10  wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi”

Kwahiyo Ibada za sanamu: Ni lango la kuzimu…Uasherani: ni lango la kuzimu!. Mtu anayefanya uasherati kajifungulia mlango wa kwenda kuzimu, Uuaji ni lango la kuzimu, Wizi ni lango la kuzimu, Anasa ni lango la kuzimu, Ulevi ni lango la kuzimu. Na mengine mengi yanayofanana na hayo!.. ndio maana Bwana Yesu kaitaja kama “Milango”..maana yake ipo mingi… Maana yake hata ukitenda mojawapo kati ya hayo bado utaingia kuzimu tu! Hata kama hutafanya hayo mengine yaliyosalia.. Ukiwa mzinzi tu, hata kama huibi, au sio mlevi, tayari utaenda kuzimu tu!..Kwasababu uzinzi, ni moja wapo ya lango la kuzimu..utafika kule kule tu, alipo mlevi na muuaji. Kwasababu kuzimu ina milango mingi.

Yakobo 2:10  “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.

11  Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria”.

Kwahiyo Kanisa Bwana atakalolitengeneza Maana yake litakuwa ni Kanisa Takatifu lisilo na kunyanzi wala hila, Kanisa ambalo litaliendea LANGO MOJA TU LA MBINGUNI (Yaani Yesu), na wala halivutwa na Malango ya kuzimu!. Kanisa la namna hiyo ndio Bwana aliahidi kulijenga.

Na alianza kulijenga siku ile ya Pentekoste, Roho Mtakatifu aliposhuka juu watu wake, akawajaza Roho Mtakatifu, na kuwapa nguvu za kushinda milango yote ya kuzimu.

Roho Mtakatifu ndio Muhuri wa Mungu, anaposhuka juu ya mtu, anaondoa ile kiu yote ya kufanya dhambi, kiasi kwamba dunia inamshangaa mtu huyo anawezaje kuishi bila kufanya zinaa katika kizazi hiki, anawezaje kuishi bila kuvuta sigara wala kunywa pombe, na hata hatumii nguvu kujizuia, anawezaje kuishi bila kutukana, bila kuiba, anawezaje kuishi maisha ya ustaarabu kiasi hicho, anawezaje kuwa na amani na huku hana kitu mfukoni, anawezaje kuwa na amani na huku kila mtu yupo kinyume naye, anawezaje kuishi bila kumkana huyo Yesu, anawezaje kuishi bila kuvutwa na anasa na starehe za dunia?..n.k pasipo kujua kuwa ipo nguvu waliyopewa ya kuishinda MILANGO YA KUZIMU.

Je na wewe unayo hiyo nguvu?. Au malango ya kuzimu yana nguvu juu yako?.

Kwa ufunuo Petro aliopewa ndio Bwana aliosema atalijenga kanisa lake juu yake, na  milango ya kuzimu haitalishinda…na ufunuo huo si mwingine zaidi ya YESU NDIYE MWANA WA MUNGU.

Mathayo 16:15  “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?

16  Simoni Petro akajibu akasema, WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.

17  Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

18  Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda”

Hivyo ukitaka milango ya kuzimu uishinde, njia ni moja tu, nayo ni KUMWAMINI YESU KUWA NDIYE MWANA WA MUNGU, Huo ndio Msingi, ambao kanisa la Mungu linajengwa juu yake. Ukitafuta msingi mwingine kamwe hutaweza kupata nguvu ya kuishinda milango ya kuzimu.

Na kumwamini Yesu, ni kutubu kwa kudhamiria kuacha kabisa dhambi zote, na baada ya hapo ubatizo, na mwisho kupokea Roho Mtakatifu, kama muhuri wa Mungu, ambaye huyo ndio ukamilifu wa kazi ya Mungu juu ya Mtu, ndiye anayetoa nguvu za kuyashinda malango ya kuzimu.

Kumbuka biblia inasema kuzimu haishibi..(Mithali 30:16), wanaoshuka huko ni wengi kila siku.Na ina milango mingi.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Je! kuna maombi yoyote ya kumtoa mtu aliyekufa kwenye mateso ya kuzimu?

LANGO LIMEBADILIKA.

WAOMBEENI WANAOWAUDHI.

UFUNUO: Mlango wa 3 part 3

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Julius chacha
Julius chacha
1 year ago

Nimebarikiwa na ujumbe Huu wa lango