Je! kuna maombi yoyote ya kumtoa mtu aliyekufa kwenye mateso ya kuzimu?

Je! kuna maombi yoyote ya kumtoa mtu aliyekufa kwenye mateso ya kuzimu?

JIBU: Kama yatakuwepo maombi ya kumtoa mtu aliyekufa katika dhambi kuzimu …basi yatakuwepo pia maombi..au itakuwepo namna ya kumtoa mtu aliyekufa katika haki paradiso.

Lakini kama hakuna maombi yoyote au namna yoyote ya kumtoa mtu paradiso na kumpeleka kuzimu..kadhalika hakutakuwepo na maombi yoyote ya kumtoa mtu jehanum na kumpeleka paradiso.

Biblia inasema katika…

Luka 16: 22 “ Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

26 Na zaidi ya hayo, KATI YETU SISI NA NINYI KUMEWEKWA SHIMO KUBWA, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu”.

Hapo inasema kumewekwa shimo kubwa…SHIMO Ni lugha ya kuonyesha kwamba haiwezekani kwa namna yoyote mtu aliyeko jehanamu kuvuka kuingia paradiso…wala aliyeko paradiso kwenda kuzimu..Ikifunua kwamba hata maombi hayawezi kumvusha mtu katika shimo hilo…

Nafasi ya kuvuka kutoka mautini kuingia uzimani tunayo tukiwa hapa hapa duniani. Tukishindwa kutengeneza mambo yetu tukiwa hapa duniani tukifika kule hakuna hiyo nafasi…Ibrahimu ambaye sisi sote tunamwita Baba wa Imani, ambaye ni mtakatifu na aliyekubaliwa na Mungu pengine kuliko mimi na wewe ameshindwa kumtoa huyo Tajiri kuzimu na kumwingiza paradiso…Je wewe au mimi ambaye tuna dhambi tutawezea wapi?…Ibrahimu ambaye sasa yupo utukufuni ambaye kashashinda vita vya ulimwengu huu, kashindwa kumtoa tajiri kuzimu… sisi ambao hata hatujui kinachoendelea ng’ambo..maombi yatu yatamtoaje mtu aliyekufa kutoka kuzimu kumpeleka peponi?.

Hivyo hiyo inatutahadharisha kuyaangalia Maisha yetu..Tujihakiki kila siku je tunampendeza Mungu?..Je tunastahili kuingia mbinguni?..Kama bado basi tutengeneze mambo yetu kabla siku zetu za kuishi hazijakwisha. Tusidanganywe na uongo wa shetani, ambao unakuja kwa kivuli cha faraja kwa ndugu zetu waliotangulia lakini kumbe nyuma yake kumejaa roho ya uongo na upotevu..Tuishi maisha masafi na ya kuwahubiria ndugu zetu kabla hawajaondoka duniani..Kwasababu hakuna nafasi ya pili baada ya kifo.

Hakuna kupitia kwanza ‘Toharani’ kisha ndio tuende mbinguni kama baadhi ya madhehebu yanavyoamini mfano wa Katoliki..Tukishakufa habari yetu ndio inakuwa imeisha hapo. kama tumeangukia upande wa uzima, basi tutabakia huko uzimani daima, kama tuliangukia upande wa mauti basi tutaishi mautini milele.

Tubu ikiwa bado hujatubu, angali nafasi ipo.

Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?

DUNIANI MNAYO DHIKI.

USIFE NA DHAMBI ZAKO!

ALIJARIBIWA SAWASAWA NA SISI KATIKA MAMBO YOTE.

Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Raphael Maiko Leboy
Raphael Maiko Leboy
1 year ago

Daima twayaweza yote katika MUNGU MWENYEZI mwingi wa rehema aliyeumba vitu vyote duniani na mbinguni