Je! Unaona Fahari juu ya nini? Ni kitu gani unachokionea Fahari?.. Je ni mali?, ni vyeo?, au uwezo ulio nao?..
Kama Bwana amekujali kukupa hivyo vyote, basi mshukuru lakini usijionee fahari juu ya hivyo, kwasababu vyote hivyo ni “UBATILI”….bali ona FAHARI juu ya BWANA YESU kama umeshamjua!.
Kwasababu kumjua YESU ni UTAJIRI mkubwa, na CHEO kikubwa na UWEZO mkubwa.. kuliko utajiri wowote wa kiduni, wala cheo chochote cha kidunia wala uwezo wowote wa kidunia.
Maana yake Kama ni kuringa, au kutamba…basi tamba kwa kuwa UMEMJUA YESU!. (Furahia kwa kuwa umekipata kitu kikubwa na cha thamani, furahi kwa kuwa umelenga shabaha)..ndivyo maandiko yanavyotufundisha..
1Wakorintho 1:30 “Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu HEKIMA itokayo kwa Mungu, na HAKI, na UTAKATIFU, na UKOMBOZI; 31 kusudi, kama ilivyoandikwa, YEYE AONAYE FAHARI NA AONE FAHARI JUU YA BWANA”.
1Wakorintho 1:30 “Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu HEKIMA itokayo kwa Mungu, na HAKI, na UTAKATIFU, na UKOMBOZI;
31 kusudi, kama ilivyoandikwa, YEYE AONAYE FAHARI NA AONE FAHARI JUU YA BWANA”.
Hapo anasema YESU KRISTO amefanyika kuwa HEKIMA itokayo kwa Mungu, maana yake kama yeye yupo ndani yetu, basi ni hekima ya Mungu imeingia ndani yetu. (sasa kwanini usione fahari juu yake kama yupo ndani yako)
Na tena amefanyika kuwa “HAKI”, Maana yake ni kwamba kama yeye yupo ndani yetu, basi tumepata haki ya kuishi milele, na kupata yote tunayoyahitaji ambayo ni mapenzi ya Mungu, (sasa kwanini usione fahari juu yake huyo kama yupo ndani yako?).
Na tena amefanyika “UTAKATIFU”.. Maana yake akiingia ndani yetu, tunahesabika na kuitwa watakatifu, (Kwanini usione fahari juu ya huyo).
Zaidi sana amefanyika “UKOMBOZI”. Maana yake anapoingia ndani yetu, tunapata ukombozi wa Laana, na zaidi sana tunapata Kuokoka na hukumu ya milele ijayo, ya ziwa la moto aliloandaliwa shetani na malaika zake (Ufunuo 12:9)… Kwanini usione fahari juu ya huyo aliyekupa ukombozi..
Aibu inatoka wapi!!!, ikiwa YESU KRISTO, aliye hekima ya Mungu yupo ndani yako?… Aibu ya kubeba kitabu chake (biblia) na kutembea nacho kikiwa wazi inatoka wapi? Ikiwa yeye ni mwokozi wako?
Aibu ya kuzungumza habari zake mbele za watu inatoka wapi? Ikiwa yeye ni Haki yako?… Aibu ya kushika amri zake inatoka wapi ikiwa yeye amekupa wokovu kutoka katika hukumu ya milele?.
ONA FAHARI JUU YAKE!.. wala usimwonee haya (aibu), maana alisema mtu akimwonea haya katika kizazi hiki yeye naye atamwonea haya mbele za malaika zake wa mbinguni.. Maana yake ni kwamba kama tukimwonea fahari, naye pia atatuonea fahari mbinguni (Marko 8:38)
ONA FAHARI JUU YAKE,…MTANGAZE KWA KUJITAMBA KABISA!.. MDHIHIRISHE KWA WATU, WAONE KUWA ULIYE NAYE NI KILA KITU KATIKA MAISHA YAKO!… Na itakuwa baraka kubwa kwako.
Wagalatia 6:14 “Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu”.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Maana ya Mithali 19:11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake.
Kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.
KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?
VAZI KUU AMBALO MUNGU AMETUANDALIA KILA MMOJA WETU.
Rudi nyumbani
Print this post