Kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.

Kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.

SWALI: Je? Daudi na Yonathani walikua wanashiriki mapenzi ya jinsia moja?

Kufuatana na vifungu hivi;

1 Samweli 20:30

[30]Basi hasira yake Sauli ikawaka juu ya Yonathani, akamwambia, Wewe, mwana wa mke mkaidi, asi, je! Mimi sijui ya kuwa umemchagua huyo mwana wa Yese, kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.


JIBU: Andiko hilo halina uhusiano wowote wa Yonathani na Daudi kuwa na mahusiano ya jinsia moja..

Wazo kama hilo linakuja kichwani mwa watu kufuatana na lile andiko linalosema upendo wa Jonathan kwa Daudi ulikuwa zaidi ya upendo wa mwanamke (2Samweli 1:26).Ambalo nalo halihusiani na jambo hilo kabisa.

Katika andiko hilo tunaona Sauli alipoona kwamba mwanawe Jonathani anashikamana sana na Daudi na kwamba yupo tayari hata kumwachia ufalme wake ambao alistahili yeye kuumiliki..ilimfanya Sauli aghadhibike sana juu yake ndipo akamwambia maneno hayo..

1 Samweli 20:30 “… je! Mimi sijui ya kuwa umemchagua huyo mwana wa Yese, kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako”.

“Aibu ya uchi wa mama yake”..Akiwa na maana “aibu ya mama yake aliyemzaa” na si vinginevyo .

Yaani kwa tendo lile la kumruhusu Daudi aje kuwa mfalme wa Israeli badala yake italeta aibu kubwa na fedheha kwa mama yake, kwa kuzaa mtoto ambaye haendelezi ufalme katika familia

Na ikumbukwe kuwa wa-mama wa wafalme enzi zile walikuwa wanapewa heshima kubwa kiasi cha kuwekewa kiti cha enzi pembezoni mwa wafalme . Na ndio maana utaona sehemu nyingi mfalme mpya atajwapo huwa anaambatanishwa na jina la mama yake, na sio mke au mtoto kwasababu walipewa heshima yao, kipekee. ( soma 2Wafalme 21:19, 22:1).

Sasa hapa inapotokea Yonathani hapiganii kiti chake cha ufalme kinyume chake ndio yupo tayari kumpa Daudi ufalme wote..Ndio maana Sauli akamwambia tendo analolifanya ni aibu kubwa sana kwa mama yake.

Hii inatufundisha nini?

Upendo usio wa kinafki unakuwa tayari kujishusha pale panapostahili kufanya hivyo.

Hautafuti mambo yake wenyewe..sawasawa na 1Wakorintho 13:5

Unawatanguliza wengine mbele..

Si ajabu ni kwanini Daudi hakuufananisha upendo ule na wa mwanamke yeyote duniani.

Na sisi pia tupendane, kwa kuwa tayari kutangulizana. Kumuhesabu mwingine ni bora zaidi yetu sisi wenyewe, Hiyo itatupa kibali kikubwa sana kwa Mungu. Kama vile Yonathani ambaye hadi leo hii tunazisoma habari zake kwa mema.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MAMA, TAZAMA, MWANAO.

HERI WAPATANISHI, MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU

Upole ni nini?

Unyenyekevu ni nini?

MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI.

Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1).

Kiyama ni nini?

YESU NDIYE ATAKAYEKURUSHIA MAWE, USIPOTUBU.

Wakati wakina Shadraka wanatupwa katika tanuru la moto, Danieli alikuwa wapi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments