Unyenyekevu ni nini, kibiblia, ili mtu awe ni mnyenyekevu anapaswa aweje?
Tafsiri ya Unyenyekevu ni Kujishusha. Pale unapokuwa na uwezo wa kutumia nguvu, au sauti, au mamlaka,kuhimiza jambo, lakini unajishusha chini, kana kwamba wewe si kitu, huo ndio unaitwa unyenyekevu.
Unyenyekevu sio kushushwa, bali kujishusha. Na kinyume cha Unyenyekevu ni kiburi, yaani kujipandisha juu, kujiona wewe unaweza yote, wewe ni bora kuliko vyote, wewe una nguvu kuliko wote, wewe una sauti zaidi ya wote.
Unyenyekevu ni mgumu sana kuufikia, kwasababu asili ya mwanadamu ni kutaka kujipandisha juu. Lakini ukiupata unyenyekevu basi umepata mpenyo mkubwa sana wa kumfikia Mungu.
Kiwango cha unyenyekevu kinatofautiana, kwa jinsi mtu unavyoterekema ngazi moja chini, ndivyo kiwango chake cha unyenyekevu kinavyokuja juu, na pale anapoongeza ngazi nyingine na nyingine ndivyo unyenyekevu wake unavyofikia kilele cha juu sana.
Wafilipi 2:6 “ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba”.
Wafilipi 2:6 “ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba”.
2) Kwasababu Mungu anawapinga wenye kiburi
Yakobo 4:6 “Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu”.
Mungu ni adui mkubwa kwa kiburi, hivyo tukilijua hilo ni kujitahidi sana tuwe mbali na kitu hicho.
Mungu alikuwa karibu na Bwana Yesu, kuliko mtu mwingine yeyote, na hiyo yote ni kwasababu ya unyenyekevu wake:
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
2) Mungu anatukweza juu;
Utaona baada ya Bwana Yesu kujishusha, Mungu alimkweza juu Zaidi ya vitu vyote ulimwenguni.
Wafilipi 2:8 “tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba”.
Wafilipi 2:8 “tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba”.
Wafilipi 2:3 “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake”.
2) Kuuzuia ulimi:
Kuwa wa mwisho kunena, na kuzuia hasira zako, usiotoe maneno ya majigambo;
Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum”.
Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum”.
3) Kutojihesabia haki, mbele za Mungu:
Luka 18:9 “Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi”.14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Luka 18:9 “Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.
10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi”.
14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
4) Kukubali kujishughulisha na mambo manyonge
Warumi 12:16 “Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili”.
Si lazima, kila jambo la juu tung’ang’anie kulifanya. Bwana Yesu alikuwa ni Mungu, lakini akaona kule kuwa sawa naye sio kitu cha kushikamana nacho. Akawa kama mtumwa..Vivyo hivyo na sisi tupende utumwa kuliko ukubwa.
Mwisho kabisa tukumbuke kuwa Unyenyekevu kibiblia, upo kwa namna mbili; Unyenyekevu wa sisi kwa sisi, na unyenyekevu kwa Mungu. Vyote viwili vinakamilisha Unyenyekevu wa ki-Mungu. Kama vile ulivyo upendo. Ili tukamilike katika huo ni sharti, tupendane sisi kwa sisi, na vilevile tumpende Mungu.
Ndio maana Bwana Yesu aliwatawaza miguu watakatifu wake, akatupa na sisi kielelezo kuwa tunyenyekeane sisi kwa sisi, kama yeye alivyofanya.
Hivyo tuizingatie sana nguzo hii muhimu katika ukristo wetu. Ili tumfurahie Mungu wetu.
Bwana akubariki.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Upole ni nini?
Furaha ni nini?
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
TUMAINI NI NINI?
Jehanamu ni nini?
Rudi nyumbani
Print this post
Barikiwa sana
Amen, Ubarikiwe
Ameni,,
Bwana Yesu asifiwe mwali Denis Nina swali Sasa itakuwaje kwa mtu anayetumia cheo chako kukuhukum maan kunajambo lilitokea unakuta mtu unafanya kitu cha haki lakini unakuta mtu ana kuambia we si kiongoz fulani ?