SWALI: Naomba kufahamu maombolezo ya Hadadrimoni tunayoyasoma katika Zekaria 12:11 ni maombolezo gani hayo?
Zekaria 12:11 “Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido”.
JIBU: Hadadrimoni ni eneo lililokuwa sehemu ya bonde lijulikanalo kama Megido huko Israeli. Bonde hili lilisifika kwa vita, na Zaidi sana kuuawa kwa baadhi ya viongozi wakubwa. Hivyo kupelekea maombolezo makubwa sana kwa watu waliouliwa viongozi wao.
Mfano katika Habari hii, inamlenga mfalme Yosia, ambaye ndiye aliyekuwa tumaini la mwisho la Taifa la Israeli. Kama wewe ni msomaji wa biblia utakumbuka, Yosia alikuwa mfalme aliyemcha Mungu sana kuliko wafalme wote wa Israeli,tukimwondoa Daudi, na yeye ndiye aliyefanikiwa kuondoa sanamu zote Israeli kipindi kile, Na ndiye mfalme ambaye kuzaliwa kwake kulitabiriwa miaka mingi sana kabla hajazaliwa.
Hivyo waisraeli walimwona kama ndiye tumaini pekee waliobakiwa nalo.
Lakini siku moja alitoka kwenda kupigana vita na mfalme wa Misri aliyeitwa Neko. Na kinyume na matazamio yake, aliuliwa, na mahali alipouliwa palikuwa ni hapo Hadadrimoni katika bonde la Megido.
Israeli nzima iliposikia, ilimwombolezea maombolezo makubwa sana, taa ya Israeli kuzima ghafla, mpaka wakamwekea kumbukumbuku lake la kila mwaka akumbukwe.
2Wafalme 23:29 “Katika siku zake, Farao-neko, mfalme wa Misri, akakwea ili kupigana na mfalme wa Ashuru, akafika mto Frati; naye mfalme Yosia akaenda kupigana naye; naye mfalme wa Misri akamwua huko Megido, hapo alipoonana naye”.
2Nyakati 35:25 “Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote waume kwa wake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hata leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika maombolezo”.
Hivyo Mungu akatumia kivuli hicho kueleza jinsi taifa la Israeli litakavyokuja kuomboleza huko mbeleni, siku watakapopewa neema ya kumtambua Kristo. Biblia inasema wayahudi watamwombolezea Yesu waliyemchoma, watalia kama vile mtu aliyefiwa na mwana wake wa pekee, mfano wa pigo la wamisri la kuuliwa wazaliwa wao wa kwanza, jinsi walivyokuwa na maombolezo makuu.
Kama vile, maombolezo ya Yosia katika bonde la Hadadrimoni, Waisraeli walivyombolezea mfalme wao, kwa uchungu mwingi, ndivyo itakavyokuwa siku hiyo watakapomwagiwa neema ya kumtambua Kristo..
Zekaria 12:10 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza. 11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, KAMA MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI KATIKA BONDE LA MEGIDO. 12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao; 13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao. 14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.
Zekaria 12:10 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, KAMA MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI KATIKA BONDE LA MEGIDO.
12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;
13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.
14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.
Ndugu, Kipindi si kirefu hii neema inayochezewa leo hii, itageuka na kuwarudia wayahudi. Kipindi hicho unyakuo utakuwa umeshapita, na Roho Mtakatifu hayupo tena kwetu sisi watu wa mataifa, bali kwa watu wake Israeli. Dunia itastaajabia, kuona watu hawa wametolea wapi moyo huo wa kujuta kwa ajili ya Yesu ambaye leo hii wanamkataa.
Kwani wayahudi hawa wakati huo, biblia inasema watajitenga, familia kwa familia, ukoo kwa ukoo, kila moja atakuwa na maombolezo yake makuu sana haradharani na sirini, kudhihirisha kazi ya Roho Mtakatifu juu yao. Sasa wakati huo ndio Mungu atakuwa anawaandaa ili kuwarudishia ufalme ambao waliutazamia kutoka kwa masihi wao, sawasawa na lile ulizo la mitume (Matendo 1:6)
Ndugu, ukishaona mabadiliko haya kwa wayahudi, ujue umeshaachwa katika unyakuo, vilevile hii dunia itakuwa na kipindi kifupi sana kisichozidi miaka 7 hadi iishe. Leo hii tumeshaona Israeli imekuwa taifa, wote wamesharudi kwao. Unadhani wanachosubiria ni nini kama sio kurudiwa wakati wowote.
Bwana Yesu alisema,
Mathayo 24:32 “Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu”;
Mtini unawakilisha taifa la Israeli (Yer 24), Hivyo tuonapo Israeli leo hii inachipuka, tujue kuwa wakati wa mavuno umeshafika.
Je!, unalitambua hilo? Bado unaipuuzia hii neema ambayo hatuna nayo muda mrefu?. Una Habari kuwa unyakuo ni wakati wowote, na hatua zake tayari zimeshaanza?. Wakati tulionao sasa si wakati wa kubembelezewa wokovu, Injili imeshazagaa kila mahali, watu wote wameshasikia, ni wakati wa kujitakasa, wewe ambaye tayari umeshaokoka. Lakini kama bado upo nje ya neema kipindi hichi? Utakuwa ni wa ajabu kweli.
Unasubiria siku Fulani, neema ikufikie? wakati neema ya wokovu ipo tayari kila mahali, unasubiria ikufikieje tena? Tambua kuwa njia imeshasonga, na wengi wanatamani waingie wanashindwa, kwasababu upotofu mwingi upo duniani, na wewe bado tu unaisubiri.. Ni kuwa makini sana. Neema inakimbilia Israeli sasa, jicho la Bwana linaelekea kule sasa, kwani muda wetu umeshakwisha.
Bwana atusaidie.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
SIKU YA TAABU YA YAKOBO.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita.
Uru wa Ukaldayo ni nini?
Rudi nyumbani
Print this post
Ubarikiwe Mtumishi. Bwana azidi kukupaka mafuta ya Ufunuo wa Neno lake!!
Amen nawe pia Bwana azidi kukubariki. Tafadhali share na wengine whatsapp/facebook kwa icon iliyopo mwisho wa kila somo..