Wakati wakina Shadraka wanatupwa katika tanuru la moto, Danieli alikuwa wapi?

Wakati wakina Shadraka wanatupwa katika tanuru la moto, Danieli alikuwa wapi?

SWALI: Je Wakati Mfalme Nebukadreza anawatupa Shadraka, Meshaki na Abednego kwenye tanuru la Moto, Danieli alikuwa wapi?


JIBU: Kwasababu biblia haiandiki kila habari, bali inachagua yale matukio muhimu tu, yatakayotusaidia, ndivyo ilivyo katika habari hii, haielezi habari za Danieli kwa wakati huo, alikuwepo wapi, lakini katika sintofahamu hiyo, tuna la kujifunza.
Hivyo hapo mambo matatu yanawezekana,

La kwanza ni aidha Danieli hakuwepo, wakati huo, ambapo Nebudreza, anatoa amri, kwasababu utakumbuka kuwa yeye aliyewekwa juu ya waganga wote, na wenye hekima (Danieli 5:11). Hivyo kuna uwezekano, alipewa jukumu lingine la kwenda kulifanya nje ya Babeli kwa wakati huo , na mbio ilipopigwa yeye hakuwepo.

La pili, ni aidha, watu waliokuwa pamoja na mfalme agizo hilo halikuwahusu, kwasababu ukichunguza utaona, Nebukadreza, aliwaita wakuu wake wote waliokuwa katika majimbo yake yote ulimwenguni. Na lengo la kuwaita, lilikuwa ni kuwapima utiifu wao kwa serikali yake moja ya ulimwengu. Ndio maana akawalazimisha wakuu wote ambao wapo mbali naye waje kuisujudia sanamu yake. Hivyo kwasababu Danieli alikuwa katika jumba la mfalme agizo hilo halikumuhusu.

Danieli 2:49 “Tena, Danielii akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danielii alikuwa akiketi katika lango la mfalme”.

Na mwisho, ni kwamba Danieli, tangu mwanzo alisimama katika misingi ya Imani yake, utakumbuka, walipoitwa na kutaka kulishwa Divai, pamoja na vyakula najisi, moja kwa moja walivikataa yeye pamoja na hao wenzake watatu. (Danieli 1:8-16) Hivyo uwezekano pia wa Danieli kumweleza mfalme misimamo wake, ulikuwepo, na mfalme akamwelewa, akamwacha peke yake asiisujudie miungu yake.

Lakini kusema kwamba alitii amri ya mfalme, hilo jambo halipo, wala lisingewezekana kwa Danieli, kwasababu utakumbuka, hata baadaye sana, jaribio kama hilo lilitaka kufanyika, la kumzuia asimwabudu Mungu wake, lakini alikaidi amri yao bila kujali nani kasema, au adhabu gani imetolewa.

Lakini habari hii ya kutokuwepo kwa Danieli inatufundisha nini?
Ni kwamba, upo wakati Mungu atakuepusha na majaribu ambayo nafasi ya kuyakwepa ni ndogo sana, lakini pia upo wakati Mungu atakupitisha katika majaribu ya adui. Mwanzoni kikombe kile hakikumuhusu Danieli, lakini mwishoni, alishiriki kikombe cha kutupwa katika tundu la Simba.

Nasi pia, kuna nyakati ngumu zitapita mbele yetu katika eneo la imani yetu, na Mungu atatuvusha salama bila hata ugumu wowote, lakini pia zipo nyakati ataziacha zipite juu yetu. Lakini yote katika yote, tunapaswa tuwe katika msimamo wetu kama vile Danieli.

Nyakati zote za mvua, na joto, misingi ya imani yetu isitikiswe.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

DANIELI: Mlango wa 1

UMEDI NA UAJEMI ZILITAWALAJE?

Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)

Nini maana ya kuutia moyo ufahamu? (Danieli 10:12)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments