Jina la Bwana wetu YESU KRISTO na MKUU wa Dunia yote libarikiwe,
Karibu katika kujifunza kitabu cha Danieli, leo tukianza na ile Sura ya kwanza, Kwa ufupi tunasoma mlango huu wa kwanza kama wengi tunavyofahamu unaeleza jinsi wana wa Israeli walivyochukuliwa utumwani mpaka Babeli kutokana na wingi wa maovu yao, na Mungu kwa kupitia kinywa cha Nabii wake Yeremia alishawatabiria kuwa wangekaa huko kwa muda wa miaka 70 mpaka watakaporudi tena katika nchi yao wenyewe. Lakini mara tu ya kwenda utumwani tunasoma mfalme Nebukadneza alitamani kuwa na watu ambao watamsaidia katika Elimu za utafiti pamoja na utabiri wa mambo yanayokuja katika ufalme wake, hivyo akaazimu kwenda kuwatafuta watu wenye ujuzi mwingi na maarifa pamoja na wanajimu na wachawi wote waliosifikia, kutoka katika majimbo yote ya dunia aliyokauwa anayatawala.
Lakini taunaona walipofika kwa watu walioamishwa wa kabila la Yuda, walionekana huko vijana wanne, wenye sifa ya kuwa na ujuzi na hekima zilizotoka kwa Mungu nao ni Shedraki, Meshaki, Abednego pamoja na Danieli ambaye alikuwa na ujuzi katika ndoto na Maono yote.
Hivyo tunasoma walipopelekwa katika jumba la kifalme kwa mafunzo ya lugha na Elimu za wakaldayo, kama tunavyojua maeneo kama hayo havikosekani vyakula vya kila namna, vinono vyote kama nguruwe, nyama za wanyama wasiopasuka miguu kama bata, divai, na ng’ombe, kuku n.k vilikuwepo ambavyo vingi kati ya hivyo vilikuwa ni Najisi kwa Taifa la Israeli.
Kwahiyo Danieli na wenzake kwa kuwa walikuwa wanamcha Mungu hawakudhubutu kuvunja torati ya Mungu kwasababu ya vyakula, Hivyo wakaazimu kumuomba mkuu wa Matowashi wasivitumie vile vyakula, ndipo wakajaribiwa kwa mtama na maji kwa muda siku 10, na tunaona licha ya kwamba MTAMA na MAJI ni vyakula visivyokuwa na virutubisho kamili lakini tunaona waliweza kunona na kunawiri kuliko wale wengine wote waliokuwa wanajishibisha na vyakula vyote vya kifalme.
Na yule mkuu wa Matowashi alipouona muujiza ule na ujasiri wao, moja kwa moja aliwatolea ile posho ya vyakula najisi na kuwalisha vyakula walivyokuwa wanataka wao. Na baada ya ile miaka 3 kuisha ya mafunzo, walipowasilishwa mbele ya MFALME ili kuzungumza nao, hawakuonekana waliokuwa mfano wa Danieli, Meshaki, Shedraki na Abednego watakaomfaa katika baraza lake la washauri.
Amen.
TUNAJIFUNZA NINI KATIKA MAMBO HAYA?.
Tunapomuweka Mungu nyuma kwasababu ya fursa fulani au mazingira fulani yaliyopo mbele yetu, tukidhani kuwa ndio tutafanikiwa ukweli ni kwamba hatutafanikiwa tutakwama tu!!, Inawezekana mazingira yanayokuzunguka kama nyumbani au kazini au popote pale yanakulazimisha wewe mwanamke uvae vimini au suruali, au kuweka makeup, angali ukifahamu kuwa sheria ya Mungu hairuhusu hayo mambo, ni najisi, kwakuwa unaogopa kutengwa, au kufukuzwa kazi, au kuonekana wewe ni mshamba sio mzuri, unajitia unajisi kwa kufanya vitu ambavyo Mungu hakukuagiza ufanye ukidhani kuwa ndio utafanikiwa au utaonekana mzuri au utapandishwa cheo n.k., ukweli ni kwamba hautafanikiwa kwa lolote, safari yako ni fupi.
Danieli na wenzake, waliazimu kula mtama na maji tu, lakini ndani ya siku 10 tu walinawiri kuliko wale wengine wote, kuonyesha kuwa vyakula vya unajisi havimfanyi mtu kunawiri badala yake ndio vinamfanya mtu KUFUBAA.
Na sisi leo vyakula vyetu najisi ni nini??..Sio nguruwe, wala bata, bali ni Uasherati, ibada za sanamu,Ulevi, sigara, Ufisadi, usengenyaji,utukanaji,wizi, Rushwa, Fashion{vimini, suruali, makeup, wiggy}, ushoga, pornoghaphy, musterbation,disco, kamari,anasa, n.k. Hivi vyote vitakupelekea UFUBAE rohoni na mwilini,kwamaana vinatoka rohoni Bwana Yesu alisema..
Mathayo 15:16-20″ Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?
17 Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni? 18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. 19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
17 Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi;… “
Hivyo usidhani kwamba kwa kufanya hivyo utakubalika, au utaonekana mzuri, au utafanikiwa, la!! bali itakuwa ni kunyume chake.”
Kumcha Mungu ndio chanzo cha mafanikio yote na Hekima yote, kwa kadiri tutakavyozidi kuendelea kutazama sura zinazofuata tutaona jinsi Danieli alivyokuwa mwaminifu mpaka Mungu akampa kujua SIRI ya mambo yatakayokuja kutokea mpaka mwisho wa dunia, na kupewa cheo cha kuwa mkuu wa maliwali na waganga wote wa dunia.
Ni maombi yangu leo katika nafasi uliyopo, USIJITIE UNAJISI NA VITU VYA ULIMWENGU HUU, Bali uwe na msimamo kama Danieli na wenzake walivyokuwa, na watakapouona msimamo wako, watakuacha uendelee nao, lakini usipoonyesha msimamo wako, shetani atakuchezea kama anavyotaka.
Ubarikiwe na Bwana YESU
Kwa mwendelezo >>MLANGO WA PILI.
Mada Nyinginezo:
NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!
BIBLIA INAPOSEMA”VILIVYOTAKASWA NA MUNGU, USIVIITE WEWE NAJISI”. JE KAULI HIYO INATUPA UHALALI WA KULA KILA KITU?
JE! INAWEZEKANA MTU AKAWA ANAONA MAONO NA KUFANYA MIUJIZA NA BADO ASINYAKULIWE?
NINI MAANA YA KUBATIZWA KWA AJILI YA WAFU? (1WAKORINTHO 15:29)
Rudi Nyumbani:
Print this post