Nini maana ya Mithali 6:30 Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha

Nini maana ya Mithali 6:30 Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha

SWALI: Je!  Mithali 6:30 inamaana gani?

Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa;  31 Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake.

JIBU: Chukulia mfano mtu hajala siku tatu, halafu akaona kuna duka lipo wazi pale jirani, na mwenyewe ametoka, akashawishika kuingia haraka  na kubeba mkate, ili akale. Lakini mwenye duka aliporudi na kuona mkate umeibiwa, alianza kumfuatilia, mwishowe akamkuta amejificha mahali Fulani anakula akiwa katika hali mbaya.

Kibinadamu, atakapoona hali halisi ya mwizi, huwenda ataishia kukasirika tu, au kumgombeza, au kwenda kumwajibisha, kwa mambo madogo madogo. Kwasababu anaona alichokifanya ni kwa ajili ya kusalimu maisha yake tu, ale asife, lakini sio kwa lengo la kuchukua vya watu, akauze, au kuleta hasara kwa wengine.

Lakini sehemu ya pili ya mstari huo anaendelea kusema kama “akipatikana atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake”.

Maana yake ni kuwa kama “atapatikana na kosa”, basi atalipa mara saba. Atagharimikia vyote alivyoviiba mara saba. Sasa kauli hiyo haimaanishi kwamba mwizi huyo huyo aliyeiba kwa ajili ya kujishibisha tumbo lake ndio atalipa mara saba, hapana, vinginevyo mstari huo ungekuwa unajipinga unaposema “watu hawamdharau mwizi akiiba kwa kujishibisha”, bali  anamaanisha kama akipatikana na hatia tofauti na hiyo..mfano aliiba vitu ili akauze, aliiba fedha ili akajiendeleze kwenye mambo yake, alete hasara kwa wengine. Huyo atalipa gharama zote mara saba.

Ndio maana utaona adhabu nyingi za wezi huwa ni kubwa sana zaidi ya vile walivyoviiba, wanapigwa faini kubwa, wengine mpaka wanauliwa, kwa wizi tu mdogo. Hapo ni sawa na wamelipa mara saba.

Je! Hili linafunua nini rohoni?

Kama njaa ya mwilini, inaweza kumfanya mwizi asihesabiwe kosa. Kwasababu watu wanaelewa umuhimu wa kunusuru uhai kwa chakula, vipi kuhusu rohoni. Hata kuna wakati Daudi alikula mikate ya makuhani ambayo  hawakupaswa watu wengine kula, lakini kwasababu alikuwa na njaa yeye na wenzake haikuhesabiwa kwake kuwa ni kosa (1Samweli 21).

Vivyo hivyo rohoni, Mungu anatufundisha sio kwamba tuwe wezi, hapana, lakini anataka tuthamini sana roho zetu, pale zinapokuwa hazina kitu, zina njaa. Iweje mtu unakaa hadi unakufa kiroho halafu unaona ni sawa kuwa hivyo hivyo kila siku. Hufanyi jambo Fulani la kujinasua katika hiyo hali yako mbaya rohoni, unaendelea tu hivyo hivyo. Tafuta kwa bidii chakula cha kiroho usife ndugu. Jibidiishe.

Iba muda wako wa kufanya mambo mengine ili ukipate chakula cha kiroho. Ni kweli ulipaswa kuwepo mahali Fulani pa muhimu, embu ghahiri muda huo, nenda kasome biblia, nenda kaombe, nenda kasikilize mahubiri yatakayokujenga. Ulipaswa uwepo kazini, lakini kwasababu ibada ile ni muhimu embu usione shida kughahiri.

Huna biblia Iba hata pesa yako ya matumizi ya muhimu kanunue, acha uonekane mjinga nenda kanunue biblia au vitabu vya rohoni vikujenge. Tafuta ile MANA iliyofichwa.

Siku hizi ni za mwisho. Na Bwana alishatabiri duniani kutakuwa na njaa, sio ya kukosa chakula au maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Mungu ya kweli. Usipojiongeza katika eneo la ukuaji wako kiroho.  Ni ngumu kuvuka hizi nyakati mbaya  za manabii wengi wa uongo, na mafundisho ya mashetani. Usipoyajenga maisha yako ya kiroho, shetani akusaidie kuyajenga kwake.

Amosi 8:11 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana”

Penda biblia, penda kujifunza, penda maombi zaidi ya vingine.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

YEYE ALIYEUWASHA HUO MOTO LAZIMA ATALIPA.

NJAA ILIYOPO SASA.

(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.

(Opens in a new browser tab)KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.(Opens in a new browser tab)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments