Swali: Je kuna ubani katika biblia?.. Na kazi ya Ubani ni nini?
Jibu: Ubani ni moja ya viungo vilivyotumika zamani kutengenezea manukato matakatifu yaliyoitwa “Uvumba”..
Viungo hivi (ubani) vinatokana na utomvu unaozalishwa na mmea ujulikanao kama “Boswelia” (Tazama picha juu). Mti wa Boswelia unaanza kutoa utomvu kati ya miaka 8 mpaka 10 baada ya kupandwa kwake, miti hii pia inastawi Zaidi sehemu zenye ukame.
Katika biblia “ubani” ulichanganywa pamoja na viungo vingine vitatu (3) ambavyo ni NATAFI, SHEKELETHI na KELBENA, kutengeneza Manukato matakatifu yaliyoitwa Uvumba ambapo Kuhani mkuu aliyachoma pamoja na kisha kuvukiza moshi ndani ya ile Hema kabla ya kufanya shughuli za upatanisho.
Na uvumba wa aina hiyo, haukuruhusiwa kutengenezwa mfano wa huo kwa matumizi yoyote yale tofauti na hayo ya nyumba ya Mungu.. (maana yake haikuruhusiwa mtu kutengeneza kwa fomula hiyo na kufanya kama marashi nyumbani kwake, au ibada nyumbani kwake, ilikuwa ni kosa).
Kutoka 30:34 “Bwana akamwambia Musa, Jitwalie manukato mazuri, yaani, natafi, na shekelethi, na kelbena; viungo vya manukato vizuri pamoja na ubani safi; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja; 35 nawe utafanya uvumba wa vitu hivyo, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenazaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu; 36 nawe baadhi yake utayaponda sana, na kuyaweka mbele ya ushuhuda ndani ya hema ya kukutania, hapo nitakapokutana nawe; nayo yatakuwa kwenu matakatifu sana. 37 Na uvumba utakaofanya, hamtajifanyia uvumba wenye viungo sawasawa na uvumba huo; utakuwa kwenu mtakatifu kwa ajili ya Bwana. 38 Mtu ye yote atakayefanya mfano wa huo, ili kuunusa, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake”
Kutoka 30:34 “Bwana akamwambia Musa, Jitwalie manukato mazuri, yaani, natafi, na shekelethi, na kelbena; viungo vya manukato vizuri pamoja na ubani safi; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja;
35 nawe utafanya uvumba wa vitu hivyo, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenazaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu;
36 nawe baadhi yake utayaponda sana, na kuyaweka mbele ya ushuhuda ndani ya hema ya kukutania, hapo nitakapokutana nawe; nayo yatakuwa kwenu matakatifu sana.
37 Na uvumba utakaofanya, hamtajifanyia uvumba wenye viungo sawasawa na uvumba huo; utakuwa kwenu mtakatifu kwa ajili ya Bwana.
38 Mtu ye yote atakayefanya mfano wa huo, ili kuunusa, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake”
Sasa kuelewa kwa upana Zaidi kuhusu “Uvumba” na maana yake kiroho basi fungua hapa >>KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?
Lakini swali ni je! Sisi wakristo tunaruhusiwa kuchoma Ubani katika ibada au manyumbani mwetu?
Jibu ni La!.. Wakristo hatujapewa maagizo yoyote ya kuchoma ubani wala kujishughulisha nao. Manukato ya Ubani yalitumika katika agano la kale katika hema ya kukutania, na baada ya agano jipya kuanza, mambo hayo yakawa ni ya KIROHO na si ya kimwili tena, hivyo hakuna Uvumba, wala ubani wala hivyo viungo vingine unaopaswa kuhusishwa na ibada yoyote katika agano hili jipya.
Kwanini Ibada hizo za Kuvukiza uvumba na ubani hazipo tena sasa?
Ni kwasababu ile ile za kuondoka ibada za kafara za wanyama.. Hatuwezi sasa kutumia Ng’ombe au kondoo kwaajili ya utakaso wa dhambi zetu, na wakati kuna damu ya YESU, ambayo inatusafisha sasa katika ulimwengu wa roho.
Vile vile hatuwezi kuchoma ubani, na kuvukiza uvumba kama njia ya kuvuta uwepo wa Mungu na wakati tunaweza kufanya hivyo kwa njia ya sala na maombi.
Zaburi 141:2 “Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni”
Sasa Kafara za wanyama (Ng’ombe, mbuzi, kondoo na njiwa) na kuchoma ubani zimebaki kuwa ibada za miungu!… Wote wanaofanya hizo, wanavuta uwepo wa mapepo na si wa Mungu! Hivyo ni muhimu kuwa makini.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
SISI TU MANUKATO YA KRISTO.
MADHABAHU NI NINI?
Chetezo ni nini katika biblia? (Walawi 10:1)
NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?
Rudi nyumbani
Print this post