Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu (Zekaria 13:7-9)

Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu (Zekaria 13:7-9)

SWALI: Nini maana ya hivi vifungu?

Zekaria 13:7-9

[7]Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema BWANA wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo.

[8]Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao watakufa, asema BWANA; lakini fungu la tatu litabaki humo.

[9]Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.


JIBU: Unabii huu ulimtabiri Yesu, wakati wa kukamatwa kwake na wayahudi ili auawe, ukisoma Mathayo 26:31 utaona Bwana alinukuu yeye mwenyewe maneno hayo kwa kusema..

“Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika”.

Na kweli tunaona baada ya Yesu kukamatwa mwanafunzi wake wote wakamkimbia.

Kama mstari wa nane unavyosema mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao watakufa, lakini fungu la tatu litabaki humo.

Ni kuonyesha kwa lugha ya mifano kuwa ni idadi ndogo tu ya wanafunzi ambao hawakumuacha kabisa kabisa, mfano wa “theluthi moja”, lakini theluthi mbili zote zilirejea nyuma moja kwa moja. Na ndio maana utaona siku ile ya pentekoste ni watu 120 tu waliokuwepo pale kuingojea ahadi ya roho. Lakini yale maelfu ya makutano yaliyokuwa yakimfuata yalitawanyika.

Lakini katika mstari wa 9, anasema;

“Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.”

na hao ndio waliopitishwa katika moto, wakabatizwa na Roho, wakawa vyombo vikamilifu vimfaavyo Mungu kwa kazi ya uvuvi.

Lakini adui hakujua ulikuwa ni mpango wa Mungu iwe vile kwamba mchungaji afe, ili wokovu mkuu zaidi ya ule wa kwanza uje kwa kupitia kifo chake.Angelijua hilo hata asingedhubutu kumgusa.

Ndio hapo shetani hakuamini alipoona wale wachache waliojazwa Roho, wakivuta maelfu kwa mamilioni ya watu  kwa kipindi kifupi mpaka dunia nzima ikawa imepinduliwa. Shetani hakujua misheni ya mchungaji ilikuwa ni kuingia ndani ya kondoo, sio kuwachunga tena kwa nje, kama hapo mwanzo.

Je nini tunajifunza?

Je! Wewe ni kundi lipi? Lile la tatu, au yale mawili ya kwanza. Ambayo yanapoona mtikisiko kidogo tu wa kimaisha hurudi nyuma, yanapoona kuyumba kidogo tu kwa kanisa hutoroka, yanapoona kutetereka kidogo kwa kiongozi wao yanarudi Misri? Kumbuka ni kusudi la Kristo wote tupitishwe katika moto, ili tuimarishwe tufae kwa ajili ya kazi njema ya utumishi wake.

Aliwapitisha wana wa Israeli jangwani, ili kuwaimarisha kabla ya kwenda kuwaangusha maadui zao kule Kaanani. Aliwapitishwa mitume wako, kwanini na wewe usipitishwe?

Vivyo hivyo ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, ambaye utapenda Bwana akutumie, basi liweke kichwani kwamba kuna mahali fulani utapitishwa ili kuimarishwa, huo ndio ubatizo wa Moto ulio wa Roho Mtakatifu. Wakati huo usimwache Bwana, kuwa fungu la tatu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KWANINI KRISTO AFE?

Tofauti kati ya zaka na sadaka ni ipi?

(Opens in a new browser tab)MWANAMKE ULIYEKOMAA KI-UMRI, ITAMBUE HUDUMA YAKO.(Opens in a new browser tab)

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments