KWANINI KRISTO AFE?

KWANINI KRISTO AFE?

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Swali la msingi: Kwanini Kristo afe, si angekuja tu kuhubiri na kufundisha njia ya wokovu na kisha apae zake kurudi juu alipotoka, kulikuwa na sababu gani ya kufa?. Leo tutajifunza sababu chache za kifo cha Bwana Yesu. Kwa kuchunguza vitu vya asili, kumbuka vitu vingi vya asili vinahubiri injili, Ndio maana sehemu kadhaa Bwana Yesu alikuwa anasema maneno haya..

Luka 13:18ย  โ€œKisha alisema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? NAMI NIUFANANISHE NA NINI?ย 

19ย  Umefanana na punje ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake; ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake.ย 

20ย  Akasema mara ya pili, NIUFANANISHE NA NINI UFALME WA MUNGU?โ€.

Maana yake ufalme wa mbinguni, umeandikwa katika vitu vya asili, umeandikwa katika Maisha ya kawaida tunayoishi, katika shughuli tunazozifanya n.k

Sasa Umuhimu wa Kifo cha Bwana Yesu, pia tunaweza kuupata kwa kupitia vitu hivi hivi vya asili, kama tukivitafakari kwa hekima.

Zifuatazo ni sababu chache za Umuhimu wa Kifo cha Bwana Yesu.

  1. Sababu ya kwanza, Ile Bwana Yesu aliyoitoa mwenyewe katika kitabu cha Yohana.

Yohana 12:24ย  โ€œAmin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengiโ€.

Hapo Bwana alikifananisha kifo chake na jinsi chembe ya ngano, inavyopandwa…Siku zote ukichukua mbegu yeyote, ile ya mahindi, au maharage, ukiifunga ndani ya gunia mahali ambapo haitaingiliwa na wadudu, ile mbegu inaweza kukaa hata miaka 5, bila kuharibika, na bila kumea chochote… Lakini utakapoichukua na kuitupa ardhini, ikazama chini ya udongo, ikapatwa na umande wa ardhini, ikaoza, wadudu wakaitembelea kidogo, wakala gamba lake la nje, ikanuka kidogo..Ndipo hapo itaanza kumea, na mwishoni kuwa mche mkubwa au hata mti, na kuzaa matunda mengi, yenye mbegu nyingi…Lakini isipopitia hizo hatua haitazaa chochote.

Na hiyo ndio sababu ya Kristo kufa..Kristo asingekufa na kufufuka, Injili isingefika duniani kote, Mataifa tusingepata wokovu…Lakini baada ya kufa, akatuletea nguvu ya Roho Mtakatifu juu yetu, kwa uweza na nguvu..Neno lake likasambaa duniani kote mpaka leo. Hivyo ilikuwa ni muhimu sana Kristo afe.

  1. Sababu nyingine ya kufa kwa Yesu, ni ili azizike dhambi zetu.

Kumbuka kuwa Kristo alibeba dhambi zetu, laumu zetu alizibeba, kwaufupi mbele za Mungu alikuwa ni mwenye hatia kwaajili yetu. Kutokana na dhambi zetu kuwa nyingi, Baba yake (ambaye ndio Baba yetu) aliuficha uso wake kwa muda ule alipokuwa pale msalabani, ndio maana akalia..Mungu wangu..Mungu wangu mbona umeniacha?..

Wagalatia 3:13 โ€œ Kristo alitukomboa katika laana ya torati, KWA KUWA ALIFANYWA LAANA KWA AJILI YETU; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mtiโ€.

Kwahiyo suluhisho pekee ya kuitoa hiyo laana juu yake ilikuwa ni KUFA, Asingekufa ile laana ingeendelea kukaa juu yake, Mungu angeendelea kujitenga naye vile vile siku zote.. Hivyo pale alifanyika najisi/laana kwaajili yetu.. Kwa dhambi zetu, ikasababisha Mungu kujitenga naye..

Sasa kifo kimefananishwa na usingizi, Siku zote mtu akiwa amechoka sana, hata uumpe pesa kiasi gani, hawezi kuundoa ule uchovu, hata umpe chakula cha aina gani hawezi kuundoa ule uchovu, suluhisho la kumfanya mtu arudie ukakamavu wake ni kulala..Akishalala akiamka, ule uchovu wote utakuwa umetoweka, na atarudi ukakamavu upya.

Na kifo kazi yake ni hiyo hiyo, ilikuwa haina budi Kristo, afe ili azike uchovu wa dhambi zetu, na afufuke akiwa katika upya.

Pia tunaweza kujifunza kwa vifaa vichache tunavyovitumia kama simu au computer… Simu ikileta usumbufu (imeganda, au imekuwa slow sana)..mara nyingi suluhisho ni kuizima na kuiwasha (kui-restart).

  1. Faida ya tatu ya kifo cha Bwana Yesu, ni ili azipokee baraka (Yaani apokee urithi).

Kristo alipokufa na kufufuka ndipo akaenda kuketi mkono wa kuume wa Mungu Baba, mamlaka yote na urithi wote akawa amekabidhiwa rasmi…

Waebrania 9:16ย  โ€œMaana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya.

17ย  Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanyaโ€

Sasa ni kwa namna gani kifo kihusiane na urithi?

Turudi kwenye mfano ule ule wa kifaa kinachoitwa simu au computer..kama wewe ni mtumiaji wa simu, zinazojulikana kama simu-jacha (smartphone) au computer.. Utakuwa unajua kwamba ili kila unapotaka kuongeza program nyingine, ili ifanye kazi, inakuambia ukizime na kukiwasha kifaa chako..ili kile ulichokiongeza kiweze kufanya kazi.

Ukitaka simu yako iwe na uwezo kutumia internet, huna budi kutumiwa zile settings na shirika la huo mtandao, na kisha wakishakutumia watakuambia zima simu yako na kuiwasha. Sasa unaweza kujiuliza ni kwanini wakwambie uzime na kuiwasha..Kwanini wasikwambie tu, endelea kuitumia hivyo hivyo.

Na Kristo, ni hivyo hivyo, alikabidhiwa mamlaka na Baba akiwa hapa duniani sawasawa na Marko 28:18, lakini Mamlaka hayo ili yaweze kuwa na nguvu zaidi, hana budi Bwana Yesu, kufa na kufufuka.

Kwahivyo kwa hayo machache, Ilikuwa ni lazima Kristo afe, na kufufuka ili Mamlaka yake iwe na nguvu. (Kwa urefu wa habari hiyo fungua hapa >>ย FAHAMU KINACHOMGHARIMU MUNGU, KUTOA URITHI WAKE.

Bwana atusaidie Mauti ya Yesu iwe na nguvu kwetu pia. Biblia inasema tunapomwamini Yesu, tunatakiwa tufe pamoja naye na kufufuka pamoja naye na kuketi pamoja naye katika roho..

Na tunakufa na kufufuka pamoja na Kristo kwa njia ya Ubatizo..Utauliza hiyo inapatikana wapi kwenye biblia..?

Warumi 6:3ย  โ€œHamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?

4ย  BASI TULIZIKWA PAMOJA NAYE KWA NJIA YA UBATฤฐZO KATIKA MAUTI YAKE, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzimaโ€.

Ndio maana ubatizo sahihi ni wa muhimu sana, ni kitu kidogo cha dakika moja lakini shetani hakipendi milele. Atamfanya mtu apende kuogelea katika fukwe za bahari masaa hata matano, lakini hatamruhusu aingie kwenye maji hayo hayo abatizwe kwa dakika mbili tu, kwa jina la Yesu. Hataruhusu hilo kamwe!..atahakikisha anamletea huyo mtu mapepo ya kumshawishi, na kuona kile kitu hakina maana au ni kutumiza matakwa ya mwanadamu na si Mungu.

Kwasababu anajua mtu yule akiingia kwenye yale maji kwaajili ya ubatizo, na huku moyoni ametubu kabisa kwa kudhamiria kuziacha dhambi zake, anajua atakapoingia kwenye yale maji, basi maisha yake yatabadilika na kuketi karibu na Kristo katika ulimwengu wa roho, kwasababu atakuwa kafufuka pamoja na Kristo.. Jambo ambalo hawezi kuliruhusu hata kidogo.

Ndugu kama ni wewe mmojawao ambaye ulishawishika na shetani namna hiyo, leo hii mpinge, katafuta kubatizwa, ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu Kristo popote pale na kwa gharama zozote, usikubali kuendelea kubaki nyuma kiroho.

Ikiwa utahitaji kubatizwa, basi wasiliana nasi kwa namba hizo hapo chini, au tutafute inbox.

Pia kama hujampokea Yesu maishani mwako, hiyo ndio hatua ya kwanza unayotakiwa uifanye, KUMBUKA YESU NDIYE NJIA, KWELI NA UZIMA. Hakuna njia nyingine zaidi yake yeye. Hivyo mpokee leo moyoni mwako na katafute ubatizo sahihi, na utaona mabadiliko makubwa sana katika maisha yako.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

KWANINI NI YESU KRISTO WA NAZARETI?

YESU MPONYAJI.

RABI, UNAKAA WAPI?

WAKAKAA KWAKE SIKU ILE. NAYO ILIKUWA YAPATA SAA KUMI.

USINIE MAKUU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
lucas mhula
lucas mhula
2 years ago

Amen๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Hakika MUNGU ni mwema sana,kamtoa mwanae kwa ajili yetu