Aina za dhambi

Aina za dhambi

Aina za dhambi ni zipi?


Dhambi zimegawanyika katika makundi makuu manne:

  1. Dhambi za makusudi,
  2. Dhambi zisizo za makusudi
  3. Dhambi za kutotimiza wajibu
  4. Dhambi za kutokujua.

1) Dhambi za Makusudi:

Hizi ni dhambi ambazo mtu anajua kabisa biblia imekataza kuzifanya lakini yeye anakwenda kuzitenda hivyo hivyo . Mfano wa dhambi hizi ni kama uzinzi, wizi, uuaji, aubuduji sanamu, ushirikina,  rushwa n.k.

Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana”.

Hesabu 15:30 “Lakini mtu afanyaye neno lo lote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.

31 Kwa sababu amelidharau neno la Bwana, na kuyavunja maagizo yake; mtu huyo atakatiliwa mbali, uovu wake utakuwa juu yake”.

2) Dhambi za kutotimiza wajibu:

Hizi ni dhambi ambazo mtu anafanya kwa kupuuzia wajibu wake au majukumu yake yeye kama mtu wa Mungu. Hizi zimegawanyika katika mafungu matatu;

  • Wajibu wa kuwaombea wengine:

1Samweli 12:23 “Walakini mimi, hasha! NISIMTENDE BWANA DHAMBI KWA KUACHA KUWAOMBEA NINYI; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka”

  •  Wajibu wa kuwahubiria wengine habari njema:

Ezekieli 3:18 “Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.

19 Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.

20 Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikiweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu wake, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.

21 Bali ukimwonya mwenye haki, kwamba yule mwenye haki asitende dhambi, tena ikiwa yeye hatendi dhambi, hakika ataishi, kwa sababu alikubali kuonywa; nawe umejiokoa roho yako”.

  • Wajibu wa kuwasaidia wengine:

Siku ile ya Mwisho, Kristo atakapokuja biblia inasema atawatenganisha kondoo na mbuzi. Kondoo ni wale watu ambao walitimiza wajibu wao wa kuwasaidia watakatifu waliohudumu katika kazi ya Mungu wakiwa hapa duniani, na mbuzi ni wale ambao walipuuzia na kudharau, hawakujua wajibu wao, wa kutoa vitu Mungu alivyowabariki kuwasaidia watenda kazi wa Mungu.

Mathayo 25:31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;

33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.

34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;

36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?

38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?

40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;

43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.

3) Dhambi za kutokukusudia:

Mfano wa dhambi hizi ni kama; Mtu amepandwa na hasira, sasa kutokana na hasira zile   ukampiga mwenzake  na kumuua, lakini lengo lake lilikuwa sio kumuua, au kumpiga n.k. Hiyo ni aina ya dhambi ambayo mtu akifanya anapaswa akatubu, asipotubu, ni kosa litakalompeleka motoni.

Walawi 4:1 “Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

2 Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu ye yote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lo lote ambalo Bwana amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lo lote la maneno hayo;

3 kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa Bwana ng’ombe mume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.

4 Naye atamleta huyo ng’ombe na kumweka mlangoni pa hiyo hema ya kukutania, mbele za Bwana; naye ataweka mkono wake kichwani mwake ng’ombe, na kumchinja huyo ng’ombe mbele za Bwana.

5 Kisha huyo kuhani aliyetiwa mafuta atatwaa baadhi ya damu ya huyo ng’ombe, na kuileta ndani ya hiyo hema ya kukutania;

4) Dhambi za kutokujua:

Ni dhambi ambazo mtu anafanya kwa kutokujua kama anachofanya ni kosa au la.

Luka 12:48 “Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi”.

Utajiuliza ni kwanini, mtu wa namna hii aadhibiwe? Jibu ni kwamba kutojua sheria, haimaanishi kuwa sheria haitakuhukumu, ni kama tu ilivyo katika sheria za kidunia, mtu akivunja sheria kwa kisingizio cha kutoijua sheria haimfanyi mtu huyo asishitakiwe. Huwezi kwenda kumbaka mtoto mchanga, na ukasema sikujua kama sheria inakataza kitendo hicho, na adhabu yake ni kali hivyo, uachwe huru.. Unaona ni wajibu wako kuijua sheria. Ndivyo ilivyo katika sheria za Mungu.

Mtu mwovu siku ile hawezi kujitetea kwa chochote, ikiwa leo hii itaendelea na uovu wake, haijalishi atasema simjui Mungu kwa namna gani.

Bwana atusaidie tuzikwepe dhambi hizo zote kwa neema yake. Hakika tutashinda ikiwa tutadumu tu katika neema ya Roho Mtakatifu.

Je umeokoka? Je! Unajua kuwa hizi ni nyakati za mwisho, na hukumu ya kiti cheupe che enzi cha mwanakondoo ipo karibuni?  Kama upo nje ya wokovu unangoja nini, embu leo fanya uamuzi mwema wa kumgeukia muumba wako. Kumbuka biblia inatuambia;

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Ikiwa upo tayari kutubu dhambi zako na kumpokea Bwana leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kupata maelekezo muhimu ya kufanya. >>>  SALA YA TOBA

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya “kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi?”

KWANINI NI LAZIMA TUFE KWA HABARI YA DHAMBI?.

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

AKIJUA YA KUWA ANA WAKATI MCHACHE TU”.

Nini Maana ya Hosana?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments