Nini Maana ya Hosana?

Nini Maana ya Hosana?

Hosana ni neno la kiyahudi lenye maana ya “OKOA”. Neno hili limeonekana mara ya kwanza kwenye biblia kipindi wakati Bwana Yesu anaingia Yerusalemu, ambapo wenyeji walimpokea kwa furaha, wakimwimbia na kumtukuza Mungu kwa shangwe nyingi..

Yohana 12: 12 “Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu;

13  wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, HOSANA! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!”

Habari hiyo hiyo unaweza kuisoma tena katika Mathayo 21:9, Mathayo 21:15, na Marko 11:9-10.

Sasa swali la kujiuliza ni kwanini, Hao watu watumie hilo Neno “Hosana” na si Neno lingine lolote…labda “karibu Ee Masihi..karibu ee Masihi”..badala yake wanamkaribisha kwa kumwambia “Hosana” yaani “okoa..okoa”.

Ikumbukwe kuwa Wayahudi (yaani Waisraeli), wakati Bwana Yesu yupo duniani walikuwa wapo chini ya utawala wa kirumi.. Wakati huo dola ya kirumi ndiyo iliyokuwa inatawala dunia nzima chini ya Mfalme Kaisari aliyeko Rumi.

Kwahivyo wakati Kristo yupo duniani, Israeli ilikuwa ni koloni la hawa warumi, Ndio maana utaona pia waliomsulubisha Bwana ni askari wa kirumi. Hivyo waisraeli wote walikuwa wanalazimishwa kumpa Kodi Kaisari, na walikuwa wanamtumikia. Na kwasababu walikuwa wanayajua maandiko kwamba ipo siku Masihi (yaani Kristo), atakuja na kuwaokoa na utumwa wote na maadui zote..kama maandiko yanavyosema…katika Zekaria

Zekaria 14: 3 “Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita”.

Hivyo Wayahudi wote walikuwa wanaitazamia hiyo siku ambayo Masihi atakuja kuwaokoa kwa mkono mkuu. Na baadhi waliokuwa wamemwamini Yesu kama ndiye Masihi huyo kafika, hivyo wakabeba matawi ya mitende na kumshangilia na kumfurahia alipoingia Yerusalemu, huku wakimwimbia..Hosana… hosana..au okokoa…okoa!

Na wanafunzi wake pia walitazamia wakati huo ndio ulikuwa umefika au umekaribia wa wakovu, wakati wa Masihi kuwapigania na kuwarudishia ufalme..wasiwe tena koloni la Taifa lingine. Ndio maana utaona kipindi kifupi tu baada ya kufufuka kwake, walimwuliza hilo swali..

Matendo 1:6  “Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?

7  Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.

8  Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

9  Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao”.

Hivyo ule haukuwa wakati wa Masihi kuwaokoa Israeli, dhidi ya utawala unaowatumikisha. Iliwapasa kwanza wakahubiri injili kwa watu wa mataifa yote kwanza, na injili itakapokwisha kuhubiriwa na watu kuokolewa, Ndipo huo wokovu mkuu kwa Israeli uje.

Hivyo utafika wakati ambapo Kristo atashuka kutoka mbinguni kwa nguvu nyingi, naye atawapigania Israeli na kuwaokoa, wakati huo injili itakuwa imeshamalizika kuhubiriwa kwa mataifa yote na unyakuo utakuwa umeshapita, na ndio utakuwa mwanzo wa utawala wa Miaka 1000 ya Yesu Kristo hapa duniani, ambapo utakuwa utawala wa Amani, na atatawala akiwa pale Yerusalemu, Israeli Pamoja na watakatifu wake aliowanyakua.

Je! Wakati huo utakuwepo Pamoja na Kristo katika utawala huo, au utakuwa jehanamu?. Maisha yako ndio jibu lako.

Kama hujaokoka Mlango wa Neema upo wazi sasa, ila hautakuwa hivyo siku zote..Ukimpokea leo Kristo, utafanyika kiumbe kipya na utakuwa na uhakika wa kuzirithi ahadi za Mungu walizoandaliwa wote wampendao.

Kama umeamua leo kumpa Kristo Maisha yako basi fuatilisha sala hii ya toba hapa >> SALA YA TOBA.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.

Je! Bwana Yesu alitumwa kwa Waisraeli tu peke yao?

SABATO TATU NI NINI?

TAZAMA, MWISRAELI KWELI KWELI, HAMNA HILA NDANI YAKE!

JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.

MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Bahatigloire
Bahatigloire
10 months ago

Na ninani aliye waokowa

bahati gloire
bahati gloire
10 months ago

Asante sana kwa neno lakini kuna kitu si elewe umesema kama yesu kristo alipanda mbiguni bila kuwaokowa wana wa israeli je tangu leo wangali ndani ya kipindi cha colonia? Na kama hawako tena je waliokolewa muda gani? Naomba unieleweshe mtumishi wa mungu