Kwanini Amelaaniwa aangikwaye msalabani?
Kutundikwa msalaba au kwa jina lingine kutundikwa mtini, ilikuwa ni adhabu iliyotekelezwa kwa watu wenye makosa ya hali ya juu sana.
Adhabu hii ilikuwa sio tu ilikuwa inatekelezwa na watu wa mataifa mengine kama wengi wanavyodhani ni Warumi tu, hapana bali pia ilikuwa inatekelezwa na Israeli pia.
Ni adhabu yenye mateso mengi sana, na vilevile ni adhabu ya aibu. Waliokuwa wanatundikwa msabani walikuwa sana sana ni wauaji. Makosa ambayo yalikuwa yanathibitisha kuwa wamelaaniwa na Mungu.
Kumbukumbu 21:22 “Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti; 23 mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi wako”.
Kumbukumbu 21:22 “Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti;
23 mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi wako”.
Utasoma sehemu nyingi, katika biblia mifano ya watu waliangikwa msalabani. (Mwanzo 40:18-19, Esta 2:22-23, Esta 7:10)
Jambo hilo hilo tunaliona mpaka katika kipindi cha karibu na agano jipya, katika ule ufalme wa Rumi, wafungwa wote waliokuwa na kesi kubwa za mauaji au wizi, n.k. Adhabu yao ilikuwa ni kuangikwa/kutundikwa msalabani ukiwa hai.
Lakini cha ajabu ni kwamba, adhabu zilizokuwa zinawahusu watu waliolaaniwa, zilimkuta mtu ambaye hakuwahi kutenda dhambi hata moja..Na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO
Wagalatia 3:13 “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, AMELAANIWA KILA MTU AANGIKWAYE JUU YA MTI; 14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani”.
Wagalatia 3:13 “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, AMELAANIWA KILA MTU AANGIKWAYE JUU YA MTI;
14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani”.
Lakini ni kwanini yamkute hayo yote?
Je ni ilikuwa ni bahati mbaya tu? Au Mungu alishindwa kumzuia? Jibu ni la, ilitokea vile kwa makusudi kabisa, ili ile hati ya mashitaka ya waliolaaniwa ifutwe juu yetu, aliibeba yeye ile hati ya laana, na ndio maana pale ambapo Baraba muuaji alipopaswa auawe, Yesu aliuawa badala yake, pale ambapo wewe mzinzi ungepaswa uhukumiwe milele kwa makosa yako, Yesu aliichukua laana hiyo siku ile msalabani, pale ambapo wewe uliye na dhambi ambazo nyingine ni aibu kuzitaja, Yesu alizichukua, hatia zote kwako.
Lakini hizo haziwezi kufutika juu yako, hivi hivi tu, bali ni mpaka uende kuzisalimisha msalabani.
Na ndio maana unahitaji kumpokea Yesu maishani mwako, vinginevyo hati ya mashitaka ya dhambi zako zitaendelea kubakia juu yako hadi siku ya mwisho, na utahukumiwa kama mkosaji.
Lakini ikiwa leo upo tayari kumpokea Yesu maishani mwako, basi leo leo atazifuta dhambi zako bure kabisa, haijalishi wewe ni mwenye dhambi kiasi gani.
Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. 5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
Hivyo kama upo tayari leo kumpa Yesu maisha yako, basi uamuzi huo ni wa busara, hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali Share na wengine, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au katika namba hii hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?
Nifanye nini ili niwe na uhakika nikifa naenda mbinguni?
MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.
USINIPITE MWOKOZI Lyrics
Rudi Nyumbani:
Print this post