KUWA MWAMINIFU KWA MANENO YAKO MWENYEWE,

KUWA MWAMINIFU KWA MANENO YAKO MWENYEWE,

Kuwa mwaminifu kwa maneno yako mwenyewe, ni muhimu sana!.


Jina la Bwana wetu Yesu libarikiwe. Karibu tujifunze biblia.

Mwinjilisti mmoja alichukuliwa katika maono mbinguni akakutana na Bwana Yesu, alionyeshwa mambo mengi yatakayotokea baada ya Maisha haya, kwa wema na waovu, lakini Pamoja na hayo kuna mambo mengine aliambiwa ambayo naamini leo tukiyatafakari yatatusaidia.

Na jambo mojawapo aliloambiwa lilikuwa ni kuhusu “uaminifu”…kulingana na maelezo yake, anasema Bwana Yesu alimwambia haya maneno;

Neno langu ni nguvu inayoshikilia vitu vyote. Kwa kiwango ambacho unavyoamini Neno langu ni kweli, ndivyo unavyoweza kufanya vitu vyote. Wale ambao wanaamini kwamba maneno Yangu ni kweli, basi watakuwa pia wakweli kwa maneno yao wenyewe, Ni asili yangu kuwa kweli, na uumbaji huliamini Neno Langu kwa sababu mimi ni mwaminifu na kwake.

Wale ambao ni kama mimi, pia huwa ni wakweli kwa maneno yao wenyewe. Neno lao ni hakika, na ahadi zao ni za kuaminika. ‘ndio’ yao inamaanisha ‘NDIO!’ na ‘hapana’ yao inamaanisha ‘HAPANA!’. Ikiwa maneno yako mwenyewe sio kweli, ni lazima pia utaanza kutilia shaka maneno Yangu, kwa sababu udanganyifu uko moyoni mwako. Ikiwa wewe sio mwaminifu kwa maneno yako mwenyewe, ni kwa sababu bado hujanijua kabisa mimi ni nani, mimi ni mwaminifu kwa maneno yangu. Ili kuwa na imani, lazima uwe mwaminifu kwa maneno yako. Nimekuita utembee kwa imani kwa sababu mimi ni mwaminifu. Hiyo ni asili yangu”.

**mwisho**

Ndugu moja ya tatizo kubwa linalowakabili wakristo wengi wa sasa, ni kukosa UAMINIFU. Na uaminifu unaanza kwa mtu kukosa uaminifu kwa mambo yake mwenyewe kwanza. Kwamfano mtu baada ya kumpa Yesu Maisha yake, akaahidi kwamba hatasengenya tena, hatatukana, hataiba, hatafanya hichi au kile anaahidi pia atamtumikia Mungu, au atakuwa mtu wa kumtolea Mungu sana n.k..lakini baada ya muda kupita anaanza kwenda kinyume na kile alichokisema au alichokipanga. Ndugu hiyo ni hatari sana.

Maneno hayo ya mwinjilisti huyo aliyoambiwa na Bwana, nayaamini asilimia mia kuwa ni kweli. Hata katika hali ya kawaida kama huwezi kuwa mwaminifu kwa mali yako mwenyewe ni Dhahiri kuwa haiwezekani kuwa mwaminifu kwa mali ya mwingine. Kama kiatu chako mwenyewe hukitunzi wala hukijali utakijali vipi kiatu cha mwingine aliyekuazima ukivae kwa muda tu!. Uaminifu wa mtu unaanza kwa kile alichonacho yeye mwenyewe, ndipo aweze kuwa mwaminifu kwa kitu cha mwingine.

Kadhalika huwezi kuwa mwaminifu kwa Maneno ya Mungu, kama sio mwaminifu kwa maneno yako mwenyewe.

Katika Luka 16:10 Bwana Yesu alisema maneno haya..

“Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia”.

Hivyo tujifunze kuyashika maneno yetu wenyewe..Ndipo tutakapoona Neno la Mungu likiwa na nguvu juu ya maisha yetu… Ukisema sitaki hichi au kile!, au nataka hichi!..basi kishikilie hicho kweli kweli usiwe na mawazo mawili mawili… Hiyo nguvu ya Maamuzi ndio chanzo cha nguvu zako za kiroho. Hata likitokea jambo mbele yako, na ukanukuu mstari Fulani kwenye biblia kwa Imani, basi jambo lile ulilolitamka kufuatia mstari huo uliounukuu, litatimia kama ulivyolisema kwasababu wewe pia huwa ni mkweli katika maneno yako…Hivyo Mungu atahakikisha na yeye analifanya neno lake kuwa kweli juu yako. Lakini tusipokuwa wakweli kwenye maneno yetu, basi kuna uwezekano pia neno la Mungu lisiwe kweli juu yetu. Tunaweza tukalinukuu sana na tusiona matokeo yoyote.. kwasababu sisi wenyewe sio waaminifu.

Bwana atusaidie, na atubariki.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Je! Ni ipi tarehe sahihi Evil-merodaki alimtoa Yekonia gerezani?

 

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

ZABURI 91, NI ZABURI YENYE NGUVU NYINGI.

SABATO TATU NI NINI?

Je! Mtume Paulo alikuwa ni Mrumi, Myahudi au raia wa Tarso?

JE! PAKA KULIA USIKU NI ISHARA YA UCHAWI?

NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,

Hakuna mtu anenaye katika Roho,kusema Yesu amelaaniwa

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments