Je! Mtume Paulo alikuwa ni Mrumi, myahudi au raia wa Tarso? Nachanganyikiwa kusoma pale Paulo anajitaja kama raia wa Rumi tena wa kuzaliwa wakati yeye ni myahudi?…
JIBU: Tukisoma katika matendo tunaona Mtume Paulo akijitambulisha kama yeye ni mwenyeji wa Tarso mji wa Kilkia..
Matendo 21:39 “Paulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge. Nakuomba, nipe ruhusa niseme na wenyeji hawa.
Kama tunavyoweza kusoma hapo ni wazi kuwa mtume Paulo hakuzaliwa Israeli wala Rumi(Italia) Bali alizaliwa mji wa Tarso sehemu ijulikanayo kama Kilikia ambao kwasasa ungekuwepo maeneo ya kusini kidogo mwa Uturuki”.
Hivyo uraia wake wa Rumi aliutolea wapi?
Ifahamike kuwa enzi zile Mtu kuwa Mrumi ulikuwa ni mtu wa daraja la juu sana kuliko raia mwingine wowote chini ya jua, na pia ulikuwa na haki kuliko watu wengine. Kwasababu enzi hizo Ngome ya Rumi ndio iliyokuwa inatawala dunia, hivyo ukiwa raia wa Rumi ulikuwa na raia wa daraja la juu sana.
Kwanza ilikuwa hauruhusiwi kupigwa au kufungwa bila kushtakiwa, tofauti na raia wa mataifa mengine..Kitendo cha kumpiga tu raia waki-Rumi bila kumshitaki adhabu yake ilikuwa kali sana iadha kifungo au kifo wakati mwingine.
Pili raia wa Rumi alikuwa na uwezo wa kukata rufaa, ikiwa hajaridhika na mashtaka aliyohukumiwa nayo, anao uwezo wa kukata rufaa. Tofauti na raia wengine hukumu ikitolewa imetolewa, kama ni kufa utakufa tu, kama adhabu basi utaadhibiwa tu! hakuna cha rufaa. Na hiyo ndio iliyokuwa inawafanya mitume wengi, na watakatifu wengi wauawe wakati wa kanisa la kwanza kwasababu hawakuwa warumi.
Vilevile kwa Rufaa hiyo anao uwezo wa kufikisha mashitaka yake hata kwa kaisari mtawala mkuu mwenyewe kule makao makuu Rumi, ana akasikilizwa na kupewa haki yake.
Na katika nyaraka zao za historia ya Rumi inayonyesha kuwa raia wa Rumi alikuwa anapewa vipaumbele vya kwanza kuingia mikataba mingi ya kisheria pasipo kuwa na vizuizi vingi tofauti na wale wengine..
Hivyo enzi zile kuwa raia wa Rumi ilikuwa ni bahati sana,ni Zaidi ya sasahivi labda mtu kupata uraia wa mataifa makubwa yaliyo endelea.
Vilevile uraia huo ulikuwa unapatikana aidha kwa kuzaliwa au kwa fedha nyingi..Soma.
Matendo 22:27 “Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo. 28 Jemadari akajibu, Mimi nalipata wenyeji huu kwa mali nyingi. Paulo akasema, Na mimi ni Mrumi wa kuzaliwa”.
Matendo 22:27 “Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo.
28 Jemadari akajibu, Mimi nalipata wenyeji huu kwa mali nyingi. Paulo akasema, Na mimi ni Mrumi wa kuzaliwa”.
Sasa tukirudi katika swali Paulo alitolea wapi Uraia wa Rumi wa kuzaliwa angali yeye hakuwa Mrumi wala hakuzaliwa katika taifa la Rumi(Italia) wakati ule?
Biblia inatupa mwanga juu ya mji wa Tarso Paulo aliozaliwa kwamba ulikuwa ni mji USIOKUWA MNYONGE..
Matendo 21:39 “Paulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge. Nakuomba, nipe ruhusa niseme na wenyeji hawa”.
Unaona mji huo wa Taso ambao ulikuwa Upo Kilkia ni mji ambao haukuwa kama miji mingine iliyokuwa chini ya ngome ya kirumi, bali huu ulifanywa kuwa Huru, japo biblia haielezi ni kwasababu gani uliachwa huru, lakini ni mji ambao raia wao waliachwa huru kuchagua uraia wao wenyewe (Ndio maana ya kutokuwa mnyonge)…Na ndipo huko huko Paulo alijipatia uraia wa Rumi wa kuzaliwa.
Jambo lingile la kujifunza ni kuwa japo mtume Paulo alikuwa na uraia wa Rumi na kwamba alikuwa na haki zote za kukataa mashtaka yoyote ya mapigo na vifungo yaliyomkuta, lakini aliruhusu wakati mwingine kupigwa hadi kutoka damu na kutupwa gerezani.. Na mwishoni ndio anajitambulisha kwa waliomshitaki, kuwa yeye ni Mrumi, nao wanaogopa sana.. (Soma Matendo 16:16-40)
Lakini kwa kufanya vile utaona alipata faida mara mbili, kwanza alijiongezea thawabu kwa Mungu kwasababu alipigwa kwa ajili ya ushuhuda wa Kristo, na pili, alimwokoa yule askari wa magereza na familia yake yote.
Hivyo na sisi wakati mwingine tunaweza tukawa na nguvu za kuzuia mashtaka yetu aidha kwa vyeo vyetu au kwa ukubwa wetu, au kwa mamlaka yetu, au kwa kujua kwetu sheria lakini hatupaswi kufanya hivyo kila wakati, isipokuwa tu pale inapopasa tukiwa na sababu maalumu kama ilivyokuwa kwa Paulo wakati walipotaka kumshtaki wampige tena wamuue alipokwenda Yerusalemu, lakini alikataa na kusema mimi ni Mrumi, na akakata rufaa ya kwenda Rumi, si kwa lengo la kwenda kujitetea bali kwa lengo la kwenda kuwafikishia injili watu wa Rumi.(Soma Matendo 22-26 )
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Je! Mtume Paulo alimwabudu malaika aliyetembea naye?
Mtume Paulo alioa?
Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema katika 1Wakorintho 15:31″…NIKAKUFA KILA SIKU?
SIRI YA KUFANIKIWA KWA MTUME PAULO.
Kwanini Mungu anasema “Afanyaye malaika zake kuwa pepo”?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Amen
Bwana akubariki kwa NENO,nimejifunza vizuri!
Amen uzidi kubarikiwa nawe pia!
Ahsante MUNGU awabariki kwa kazi njema ya imani
Amen atubariki sote..
Amen atubariki sote…
Amos Mumia