Je! Mtume Paulo alimwabudu malaika aliyetembea naye?

Je! Mtume Paulo alimwabudu malaika aliyetembea naye?

SWALI: Je! Mtume Paulo alikuwa anamwabudu malaika wake aliyekuwa anatembea naye kama tunavyosoma katika Matendo 27:23?

JIBU: Tuusome huo mstari..

Matendo 27:23 “Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami,”

Mstari huu ukisomwa kwa haraka haraka ni rahisi kutafsiri kwamba Mtume Paulo alimaanisha kusema kwamba anamwabudu Malaika wake..Lakini ukiurudia tena taratibu utaona kwamba hapo Mtume Paulo hakumaanisha kuwa anamwabudu Malaika bali ni Mungu..

Sasa tunaweza kuiweka vizuri sentensi hiyo kama ifuatavyo; “Kwa maana usiku wa leo Malaika wa Mungu alinijia”…..sasa swali ni Mungu yupi?…ndio anaendelea kusema…Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye…

Hivyo ukirudia kusoma kwa namna hiyo huo mstari utapata tafsiri kamili.

Hivyo Pamoja na hayo tunazidi kujifunza kwamba tunapaswa kuzidi kuyachunguza maandiko, ili tupate kulielewa Neno la Mungu kama yeye Mungu wetu anavyotaka tulielewe..kwasababu ipo mistari mingi na Habari nyingi katika maandiko matakatifu ambazo wakati mwingine ni ngumu kuzielewa lakini tunapokaa chini na kutaka kumwuliza Roho Mtakatifu yeye ni mwaminifu na atatufulia, kwasababu tusipopata tafsiri kamili kwa msaada wa Roho Mtakatifu shetani anaweza kuitumia mistari hiyo hiyo kutukosesha na kutuhalalisha uovu wake…kama alivyoitumia baadhi ya mistari kuwadanganya watu kuhalalisha ulevi, zinaa, ndoa za mitara na hata ameshautumia mstari huu kwa baadhi ya watu kuhalalisha ibada za kuabudu malaika na ibada za sanamu.

Bwana atusaidie na kutubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?

Je! Shetani alitolea wapi uovu?

Je ni wakina nani ambao hawataonja mauti mpaka siku ya kuja Bwana?

Ulinzi wa daima (eternal security) Je! ni neno la kimaandiko?

Kwanini Musa alipewa mbao mbili za mawe na sio moja au zaidi

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments