MALAIKA WAPELELEZI WA HUKUMU WANAPITA SASA.

MALAIKA WAPELELEZI WA HUKUMU WANAPITA SASA.

Kabla Mungu hajaleta maangamizi katika dunia, huwa anawatuma kwanza malaika zake wapelelezi kwenda kuhakiki hicho kilichomfikia kuwa ni kweli au La, na ikithibitika kuwa ni kweli basi hatua inayofuata saa hiyo hiyo  ni wale malaika kutekeleza hukumu ya Mungu juu ya watu hao au Mji huo. Kwananini anawaagiza malaika hawa kwanza kupeleleza, je ni kwasababu yeye mwenyewe hajui kiwango cha maasi na haki yaliyomo ulimwenguni?..jibu ni hapana!..anajua kila kitu pasipo hata kutegemea malaika zake, wala mwanadamu..lakini anafanya hivyo ili pawepo na mashahidi ya kile kinachoendelea…Kama biblia inavyosema “Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.(2Wakorintho 13:1)”

Ndicho kilichotokea kipindi kifupi kabla ya miji ya Sodoma na Gomora kuangamizwa. Mungu aliwatuma malaika zake wawili, kwenda kuipeleleza miji ile, na kama tunavyoifahamu habari, malaika wale walipofika jioni ile, wakakutana na Lutu, Lutu naye akawalazimisha kuingia nyumbani kwake, mwanzoni walikataa, lakini baadaye wakafika, na walipofika tu kumbe huku nyuma, walikuwepo pia wapelelezi wengine wanawafuatilia malaika wale, na hao si wengine zaidi ya watu wa miji ile..

Hivyo sio malaika tu waliokuwa wanapeleleza, na wao pia walikuwa wanapelelezwa, jambo ambalo linaendelea sasa katika roho..

Sasa walipoona hatma yao ni wapi, kuwa ni ile nyumba ya Lutu, hawakufanya chochote, bali walisubiri mpaka usiku ulipoingia  ndipo wakakusanyika wote wakaizingira ile nyumba ya Lutu na kumwambia Lutu, awatoe hao watu  ili wapate kulala nao..Embu fikiria hali yao ilivyokuwa mbaya..Sasa kama ukichunguza pale utaona, wale malaika hawakuchukua hatua yoyote kwanza, ni kama walikuwa wanawasikiliza walichokuwa wanamueleza Lutu pale nje, na mashindano yao pale mlangoni..Na baadaye ilipoonekana Lutu anashindwa, wakawa wanakaribia kuuvunja mlango, ndipo wakanyanyuka wakamvuta Lutu ndani, kisha wakawapiga upofu wale watu waliokuwepo pale mlangoni..

Hiyo ilisababisha ripoti yao ya upelelezi iwe imekamilika, kwamba Sodoma kumeoza na wao ni mashahidi, kilichobakia kwao ni kumuhimiza Lutu kwa haraka aondoke Sodoma kwa sababu miji ile wanakwenda kuiteketeza. (Soma Mwanzo 19 yote)

Ndugu yangu, dalili kubwa inayotutambulisha kuwa tunaishi katika wakati wa upelelezi wa malaika hawa, Sio kuzuka kwa vitendo vya Ushoga na usagaji tu peke yake, hapana, kwani hivyo vilikuwepo tangu zamani..lakini ni kuzuka kwa vitendo vya Ushoga na Usagaji katika nyumba ya Mungu…Tunavyoona leo hii ushoga unafungishwa katika nyumba ya Mungu, basi tujue hiyo ni dalili mbaya, ni sawa na kutaka kuzini na malaika wa Mungu walio katika kanisa lake..

Malaika hao wameshapita na wameshaona kile ambacho kilitokea wakati wa sodoma na Gomora ndicho kinachotokea na sasa hivi, hivyo wanachokifanya sasa ni kuwapiga watu upofu kwa kasi sana, ili wasione mlango wa neema tena ambao wenyewe wanauvunjia heshima, na kinachobakia kwa watu hao  ni maangamizi tu..

Unapojiona wewe ni mtazamaji wa Pornography, ujue kuwa wewe ni kundi moja na hawa wanaoufanya  ushoga nyumbani mwa Mungu, isipokuwa wewe tu ni mfuasi wa nyuma, lakini adhabu yenu ni moja,,..na hivi sasa unapigwa upofu, ambao hutakaa uuone mlango wa neema kamwe kama hutatubu. Ukiona unazini, na kwako wewe zinaa ni kama kitu cha kawaida na huku unajiita ni mkristo bado, ujue upofu unaendelea sasahivi duniani, ukiona unajihusisha na mambo yote ya kizinzi (iwe ni kujichua, au ulawiti) ujue upo katika kundi hilo la kupigwa upofu na malaika hawa wapelelezi wa Bwana.

Wanapopita na kuangalia makundi mengi ya watu, leo hii yapo kwenye simu zao mikononi, kutwa kuchwa ku-download video za pornography na kutazama video hizo, na miziki ya kidunia..ujue kuwa hao watu wanapigwa upofu, na malaika hao waliotumwa na Mungu kuipepeleza dunia, kabla ya kwenda kuangamizwa dunia hii kwa moto siku hizi za mwisho.

Wakati huu ni wakati wa hatari nyingi, ikimbie dhambi, unaweza kuona inavutia leo machoni pako, na ndivyo ilivyo dhambi siku zote ni ya kuvutia lakini mwisho wake ni majuto ya milele. Mungu tayari ameshakikasirikia kizazi hiki, kinachoichezea madhabahu yake mpaka kufikia hatua ya kufanya mambo ya ajabu kama hayo madhabahuni pake..Utasema ni hao sio mimi, kumbuka kile kikundi kichache kilichokuwa kinacheza mlangoni mwa Lutu ndicho kilichouwashia moto mji mzima wa Sodoma na Gomora..ikasababisha hata wengine walio mbali wasiojua chochote ambao wanafanya mambo kama hayo mwisho wao kufika. Kwahiyo uovu unapoendelea katika nyumba ya Mungu ni jambo la kuomboleza kwa wote.

Hivyo na sisi Bwana atusaidie tusiwe wamoja wapo, bali tuchukue hatua ya kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kabisa kumgeukia yeye, katika huu wakati mfupi wa kumalizia kabla ya unyakuo kupita. Kwasababu tusidhani kuwa yaliyowakuta wale, hawayawezi kutukuta na sisi.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

USINIPITE MWOKOZI

JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..

UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.

JIRANI YANGU NI NANI?

Je! Hamna nyumba za kulia na KUNYWEA?.Mstari huu unahalalisha unywaji wa pombe?

DANIELI: Mlango wa 8

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments