SWALI: Je! Siku ipi ambayo Mfalme wa Babeli alimtoa vifungoni mfalme wa Israeli(Yekonia/Yehoyakini). Je! Ni ile tarehe 25 ambayo tunaisoma kwenye Yeremia, au ile ya tarehe 27 tunayoisoma kwenye kitabu cha 2Wafalme..Na Je! biblia imekosea uandishi?
JIBU: Tusome..
2Wafalme 25:27 “Ikawa katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yekonia mfalme wa Yuda ,katika mwezi wa kumi na mbili ,SIKU YA ISHIRINI NA SABA YA MWEZI ,Evil-merodaki,mfalme wa Babeli ,katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake,akamwinua kichwa Yekonia,mfalme wa Yuda,akamtoa gerezani”.
Lakini Yeremia inasema..
Yeremia 52:31 “Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, SIKU YA ISHIRINI NA TANO YA MWEZI, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani. 32 Akasema naye maneno mazuri, akaweka kiti chake juu ya viti vya wafalme waliokuwa pamoja naye huko Babeli”.
Yeremia 52:31 “Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, SIKU YA ISHIRINI NA TANO YA MWEZI, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani.
32 Akasema naye maneno mazuri, akaweka kiti chake juu ya viti vya wafalme waliokuwa pamoja naye huko Babeli”.
Kwa ufupi kama tunavyoifahamu habari tunajua kuwa wana wa Israeli walimuasi Mungu sana mpaka ikafikia hatua ya wao kupelekwa tena utumwani Babeli kama walivyopelekwa zamani enzi za Misri.
Hivyo waliochukuliwa mateka, yaligawanywa katika makundi makuu matatu:
Kundi la kwanza ndio lile lililokuwa chini ya Mfalme, Yehoyakimu, ambalo Danieli alikuwa miongoni mwao.
Kundi la Pili, lilikuwa chini ya huyu Mfalme Yekonia/Yehoyakini, ambapo Nabii Ezekieli naye alikuwa ndani ya kundi hili.
Na kundi la tatu lilikuwa ni la mfalme Sedekia, ambaye huyu alionyesha kiburi kwa Nebukadneza ikamfanya mpaka atobolewe macho, na kusababibishia kundi kubwa sana la wa-Yuda kuchukuliwa utumwani.
Sasa Tukirudi kwa huyu Yekonia ambaye yeye alichuliwa katika awamu ya pili alipokuja kuchukuliwa yeye hakuleta ubishi kwa Mfalme wa Babeli badala yake alijisalimisha kwa amani yeye na familia yake, hivyo Evil-Mordekai hakumuua, na badala yake alimchukua na kumwekwa vifungoni Babeli,..Alikaa huko hadi ulipofika wakati wa mfalme wa Babeli kumuhurumia na kumtoa..
Jibu ni kwamba biblia haijajichanganya hapo, ikumbukwe kuwa hata leo hii mfano Raisi wa nchi akitoa tamko la wafungwa kadhaa kupokea msamaha, na hivyo wawe huru, haimaanishi kuwa ni siku hiyo hiyo wanatoka gerezani..Bila shaka kutakuwa na shughuli za makaratasi ambazo zitafuata baada ya hapo kwa kwa muda, aidha, kwa siku kadhaa, au wiki kadhaa, na ndipo baadaye wawe huru.
Vivyo hivyo ilivyokuwa kwa Yekonia, tarehe 25 yake ilikuwa ni kama tamko la yeye kuwa huru, na siku ya tarehe 27 ndio ikawa siku yake ya kuwa huru. Hivyo waandishi kutofautiana haimaanishi kuwa kuna hitilafu, kinyume chake ni kuwa wote wapo sawa. Mmoja aliichukua siku ya tamko, na mwingine akaichukua siku ya kuwekwa huru.
Ubarikiwe.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
NINAJUA MAWAZO NIKUWAZIAYO:
MNARA WA BABELI
TUPO KATIKA ZAMU YA NNE YA MWISHO.
USITUMAINISHWE NA MANENO YA UONGO.
DANIELI: Mlango wa 9
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Amina sana.