Shalom, karibu tujifunze maandiko.
Katika maisha kumbuka kumtolea Mungu, kamwe usilisahau jambo hilo, uwe ni mchungaji, mwalimu, nabii, au muumini wa kawaida au yeyote Yule…maadamu tayari umeshamkabidhi Yesu maisha yako, kamwe usisahau kumtolea Mungu…Wengi wanakidharau hichi kipengele…ni kweli kabisa hatuwezi kumpa Mungu chochote kile kwasababu vyote vinatoka kwake…lakini utoaji wetu una nafasi kubwa sana katika moyo wa Mungu. Kutoa ni ishara ya kuonyesha unajali, unapenda na unathamini.. haijalishi hicho unachokitoa ni kidogo kiasi gani lakini kina nafasi kubwa sana katika moyo wa Yule unayemtolea.
Hebu tafakari mwanao anatoka shule anakuletea zawadi ndogo tu ya kalamu anakwambia mama/baba nimepita pale nimeona kalamu nzuri nimeinunua itakufaa kwa kazi zako…ukizingatia hiyo hela aliyonunulia ni wewe ndio uliyempa…Bila shaka kitendo hicho kitakugusa sana moyo…badala ya kuichukua ile kalamu kwa furaha kwamba umepata kitu kutoka kwa mwanao, badala yake utaichukua kwa moyo mwingine…itakutafakarisha sana, zaidi itakupa nafasi ya kumjua mwanao vyema, na kumpenda na kumwamini…na zaidi ya yote kutafuta kumlipa hata mara kumi ya kile alichokufanyia wewe.
Na ndio hivyo hivyo tunapokuwa na moyo wa kumtolea Mungu…fedha ile, au sadaka ile au chochote kile unachompa…kwake haendi kukitafsiri kama fedha, bali anakitafsiri kama moyo wa upendo, wa kumjali na wa kumheshimu..Utajisikiaje Mungu ajihisi unampenda??..bila shaka ni jambo zuri. Na lina thawabu sana.
Na pia kumtolea Mungu sio jambo la kukumbushwa…na wala hatulazimishwi na Mungu kumtolea yeye… “Kutoa ni kitu ambacho kinatoka ndani ya mtu baada ya kujua umuhimu wa kufanya hivyo”..
Na sehemu sahihi ya kumtolea Mungu ni mahali linapofundishwa Neno lake (ndio tafsiri ya sadaka)..Na Mungu wetu hazikusanyi sadaka hizo na kuzihifadhi mbinguni,…sadaka hizo zinatumika kwa kuiendeleza kazi yake kwa kutumia watumishi wake..Hivyo unapotoa kiwango Fulani cha fedha kama sadaka yako, fedha hiyo inakwenda kwa watumishi wa Mungu na hao ndio wanaoipangia bajeti kwa hekima ya Roho…Lakini kumbuka pia Mungu ananjia nyingi za kuifanya kazi yake iendelee kuwepo…hivyo wewe au mimi sio jiwe kuu la pembeni kwamba tusipomtolea basi atakwama!…ana njia zaidi ya milioni moja kulisimamisha kusudi lake pasipo hata mtu yeyote kutoa chochote.
Esta 4:10 “Ndipo Esta akasema na Hathaki, akamtuma tena kwa Mordekai, kusema, 11 Watumwa wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu ye yote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini. 12 Basi wakamwambia Mordekai maneno ya Esta. 13 Naye Mordekai akawaagiza wampelekee Esta jibu la kusema, Wewe usijidhanie kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote. 14 Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; WALAKINI NI NANI AJUAYE KAMA WEWE HUKUUJIA UFALME KWA AJILI YA WAKATI KAMA HUO? ”
Esta 4:10 “Ndipo Esta akasema na Hathaki, akamtuma tena kwa Mordekai, kusema,
11 Watumwa wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu ye yote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini.
12 Basi wakamwambia Mordekai maneno ya Esta.
13 Naye Mordekai akawaagiza wampelekee Esta jibu la kusema, Wewe usijidhanie kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote.
14 Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; WALAKINI NI NANI AJUAYE KAMA WEWE HUKUUJIA UFALME KWA AJILI YA WAKATI KAMA HUO? ”
Unaona hapo? Malkia Esta alidhani yeye asipoongea chochote ndio wayahudi watakufa..lakini Mordekai anamjibu na kumwambia asijidhanie kuwa asipozungumza chochote ndio wayahudi watakufa kinyume chake Mungu anaweza kufungua njia nyingine ya wokovu na wayahudi wote wakapona na yeye akafa katika huo umalkia wake…Lakini alipojinyenyekeza ndipo Mungu akamtumia yeye (Esta) kuwa wokovu kwa Israeli..Lakini angekaa kimya, Mungu angefungua wokovu kwa njia nyingine.
Ndivyo hivyo hivyo na sisi tunapojinyenyekeza na kumtolea Mungu,..basi sisi tunafanyika kuwa sehemu ya yeye kulikamilisha kusudi lake, tunafanyika sehemu ya yeye kuifanya kazi yake iendelee….Badala ya kumtumia mtu Fulani anakutumia wewe…Kama Mordekai alivyomwambia Esta “WALAKINI NI NANI AJUAYE KAMA WEWE HUKUUJIA UFALME KWA AJILI YA WAKATI KAMA HUO? ”..Lakini kama hatutaki, wala hatulazimishi, kazi zake zitaendelea kama kawaida kwasababu atawatumia wengine na si sisi…na kuwabariki hao na si sisi.
Bwana atusaidie kuyajua hayo, na kuyafanyia kazi kwa vitendo na si kwa midomo tu.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
CHUKIZO LA UHARIBIFU
DAKIKA MOJA TU, INAKUFANYA UMWAMINI SHETANI?
NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,
USIHUSISHE HISIA KATIKA KUMTOLEA MUNGU.
ESTA: Mlango wa 4
EPUKA MUHURI WA SHETANI
RAFIKI WA KWELI NI YUPI?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Ubarikiwe ndugu
Amen..nawe pia