MAANA YA KRISTO/ JINA KRISTO LINA MAANA GANI?

MAANA YA KRISTO/ JINA KRISTO LINA MAANA GANI?

Neno Kristo, na Masihi ni kitu kimoja, isipokuwa kwa lugha ya Kiebrania linatamkwa kama Masihi, lakini kwa lugha ya kigiriki linatamkwa kama Kristo.

Yohana 1:41 “Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo)”.

Hivyo Neno hili Kristo/Masihi linamaanisha mtiwa mafuta.

Mtiwa mafuta ni mtu yeyote aliyechaguliwa au aliyetengwa na Mungu kuwa wakfu kwa ajili ya kutimiza kusudi lake Fulani..Aidha na kuokoa, au kutawala, au kuchunga.

> Hivyo manabii wote unaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi au Kristo kwa Mungu, kwa lengo la kuitabiria Israeli, na kuwaelekeza maagizo yatokayo kwa Mungu.

1Nyakati 16:22 “Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu”.

> Makuhani wote tunaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi au maKristo wa Bwana wakifanya kazi ya upatanisho wa dhambi za watu na makosa yao.

> Waamuzi wote unaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi wa Bwana waliotiwa mafuta kwa lengo la kuwakomboa wanadamu.Wakina Gideoni, Samsoni, Yeftha wote hao walikuwa ni masihi wa Bwana.

> Vilevile wafalme wote iwe ni wa wale waliotoka Israeli, au hawajatoka Israeli tunaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi wa Bwana kwa ajili ya kuwaongoza watu wake.

1Samweli 24:5 “Lakini halafu, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli.

6 Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA,neno hili,kuunyosha mkono wangu juu yake,kwa maana yeye ni masihi wa BWANA”.

 

Isaya 45:1 “Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake,ambaye nimemshika mkono wake wa kuume,ili kutiisha mataifa mbele yake,name nitalegeza viuno vya wafalme;ili kufungua milango mbele yake,hata malango hayatafungwa.

2 Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma”;

Lakini hao wote walikuwa ni kivuli cha MASIHI/KRISTO MKUU NA HALISI atakayekuja, ambaye alitiwa mafuta mengi sana yasiyoelezeka kuliko wote, biblia inasema hivyo, na huyo si mwingine zaidi ya YESU.

Waebrania 1:8 “Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi; KWA HIYO MUNGU, MUNGU WAKO, AMEKUTIA MAFUTA, MAFUTA YA SHANGWE KUPITA WENZIO”.

Na ndio maana haitwi tu Yesu peke yake, bali anaitwa YESU KRISTO.

Yesu Kristo ametiwa mafuta ya mengi sana ya kuwakomboa wanadamu. Yeye anayo mafuta yote ya kikuhani ndani yake, anayo mafuta ya kifalme ndani yake, anayo mafuta ya kinabii ndani yake, anayo mafuta ya kichungaji ndani yake.. Yaani kwa ufupi mafuta yote ya karama za Mungu yapo ndani yake.

Hivyo mtu akimwamini Yesu, basi amepata kila kitu, ikiwemo ukombozi wa roho yake.

Lakini tahadhari ni kuwa biblia imetabiri kuwa siku za mwisho kutatokea makristo wengi wa uongo ili kuwadanganya watu wengi.

Mathayo 24:24 “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele”.

Kumbuka anasema watatokea makristo, hasemi ma-yesu, ikiwa na maana kuwa watakuwa ni watiwa mafuta lakini ni watiwa mafuta ya uongo, watakuwa wanaweza kweli wakawaombea watu kwa jina la Yesu na wakapona lakini injili yao ni injili potofu isiyoweza kumwokoa yeye, wala hao anaowaongoza.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema..

Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.

Hivyo je! Swali na  wewe umechukuliwa na hili wimbi la makristo wa uongo?

Tunaishi katika wakati mgumu na wa hatari kuliko yote katika historia, hivyo kama maisha yako yapo mbali na Kristo basi ujue upo hatarini sana kupotezwa.

Kwanini usimpe Kristo leo maisha yako ayabadilishe, kisha yeye mwenyewe akupe Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kuijua kweli yote ya kimaandiko, ambaye atakaa ndani yako kukulinda mitego yote ya ibilisi?. Kama leo upo tayari kufanya hivyo, na unasema sitaki tena maisha ya dhambi nataka Yesu aniokoe awe peke yake masihi ndani yangu. Basi fungua link hii kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

UPAKO NI NINI?

KUWA MWAMINIFU KWA MANENO YAKO MWENYEWE,

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

Yakobo alikuwa na watoto wangapi?

REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
VICTOR MKONY
VICTOR MKONY
10 months ago

Nahitaji ujumbe wa neno la Mungu kila siku kwenye email yangu hii

Deograsius Fungama, 0765181084
Deograsius Fungama, 0765181084
2 years ago

SOMO zuri sana