UPAKO NI NINI?

UPAKO NI NINI?

Upako ni nini?

Upako wa Roho Mtakatifu au  kwa kiingereza (anointing of the Holy spirit). Ni neno lenye tafsiri pana kidogo. Linaloweza kumaanisha Nguvu au uwezo wa kipekee mtu anaoupekea kutoka kwa Roho Mtakatifu.. kumsaidia  kufanya jambo Fulani kirahisi zaidi,. au kufanya jambo ambalo hapo mwanzo alikuwa hawezi kulifanya.

Kibiblia zamani, mtu kabla hajatawadhwa kuwa mfalme alikuwa anatiwa mafuta,.. kiashirio cha mafuta yaliyomwagwa ndani ya roho yake kama baraka kutoka kwa Mungu ya kumsaidia yeye kuwa mtawala..(2Wafalme 9:6)

Vilevile watumishi wa Mungu kama makuhani, na manabii, nao pia walikuwa wanatiwa mafuta,.. kabla ya kuanza kutumika katika kazi ya Mungu.(Kutoka 29:7, )

Upako katika agano jipya:

Lakini katika agano jipya, vipo pia vigezo vya kutiwa mafuta,.. na vigezo hivyo havitegemei kunyunyiziwa mafuta ya aina yoyote ndani ya mtu,.. Bali kinyume chake ni kwa kuyatenda maagizo ya Mungu..

Tunamwona mtu mmoja katika biblia ambaye Mungu alimtia mafuta(upako) mengi zaidi ya watu wote waliowahi kuishi chini ya jua.. na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO,.. yeye mafuta yale yote aliyotiwa yalikuja juu yake kwa sababu moja tu..nayo ni hii: alipenda haki, na kuchukia maasi.

Waebrania 1:8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele;. Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.

Unaona Kristo, alipenda haki na kuchukia maasi, na ndio maana alitiwa mafuta kushinda sisi wote.

Tuwe kama yeye:

Vilevile na sisi tukiwa watu wa namna hiyo kama yeye wa kupenda haki na kuchukia maasi.. basi tuwe na uhakika kuwa Mungu naye atatutia mafuta mengi kupita kiasi katika maisha yetu na katika kumtumikia yeye..tutakuwa na upako wa kupita kiasi.

Tofauti na inavyodhaniwa na wengi leo hii, kwamba ukitaka upako,.. ni kwenda kufunga  kuomba sana  milimani, au kwenda kuwekewa mikono na mtumishi huyu au mtumishi Yule,.. hiyo sio sahihi..Ni vizuri tukifanya hivyo lakini huku nyuma tunafanya yampendezayo Mungu..Lakini kama hatufanya hayo na huku tunatafuta mafuta ya Roho Mtakatifu basi tuwe na uhakika kazi tunayoifanya ni bure..

vigezo vya kuupokea upako:

Ni lazima kwanza tujazwe Roho, na Kujazwa Roho si kwa kunena kwa lugha,. bali ni kwa kulitii Neno la Mungu kama ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo,.. yaani kuwa watakatifu kama jina lake mwenyewe Roho Mtakatifu lilivyo..Ndipo hapo na yeye ataachilia mafuta yake(upako) ndani yetu.

Hivyo kama wewe bado huna Roho wa Mungu ndani yako, fahamu kuwa huwezi kufanya jambo lolote,.. huwezi kuyaelewa maandiko, huwezi kuishinda dhambi, wala huwezi kumtumikia Mungu..Vilevile huwezi kwenda mbinguni haijalishi unajitihada kiasi gani..

Warumi 8:9 “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.

Lakini ikiwa utapenda Bwana akupe kipawa hicho, basi fahamu kuwa kipawa hicho ni bure,,, na wala hakiihitaji kutumia nguvu kukipata..Jambo la kwanza unalopaswa kufanya ni kutubu kwanza kwa  kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako zote,, kisha ukishatubu sasa na kusema kuanzia leo, mimi na ulimwengu basi, na kuanza kumtazama Kristo,. na kutaka kujifunza Neno lake kwa bidii..Mungu akishaona umegeuka na kuacha uliyokuwa unayafanya basi atakusamehe,. na AMANI YA AJABU itaingia ndani yako..Na yeye atasimama kukusaidia kwa namna ambayo hujawahi kuiona katika maisha yako.

Tafuta ubatizo:

Kisha bila kupoteza muda nenda katafute mahali utakapobatizwa katika ubatizo sahihi.. wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa Jina la YESU KRISTO,. sawasawa na (Matendo 2:38) ili uukamilishe wokovu wako, na kumruhusu Roho Mtakatifu kuingia ndani yako, na kuweka makao yake milele ndani yako..

Ukishafanya hivyo kwa moyo wa dhati bila kigugumizi, basi fahamu kuwa Roho wa Kristo ameshaingia ndani yako,. muda mfupi baadaye atakushushia vipawa vyake., kwa jinsi apendavyo yeye, aidha lugha, aidha maono, aidha ndoto, aidha uinjilisti,au unabii n.k.. Wewe tu mwenyewe utaona badiliko ndani yako siku baada ya siku..atakuwa anakufundisha na kukuongoza katika njia ya kweli yote, kwasababu yale mafuta yake tayari ameshayamwaga ndani yako.

1Yohana 2: 27 “Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote., tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake”.

Hivyo atakufundisha, na kukupa upako halisi unaotoka kwake, na sio ule feki unaouzwa na manabii wa uongo katika chupa,. na vifungashio mabarabarani, upako unaotoka kuzimu, usioweza kuyageuza maisha yako.

Fanya hivyo, Na Bwana akusaidie katika kukamilisha hatua zote hizi.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Amen.

Mada Nyinginezo:

UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUZAA MATUNDA.

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

SIKU ILE NA SAA ILE.

Je! hizi roho saba za Mungu ni zipi? na je zinatofautiana na Roho Mtakatifu?

ALIKUWAKO NAYE HAYUKO, NAYE YU TAYARI KUPANDA KUTOKA KUZIMU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Lazaro mwakajela Mwafrika
Lazaro mwakajela Mwafrika
1 year ago

Na ishara hizi zitaongozana nao watanena kwa ruga watatoa pepo watapooza wagonjwa na kufufuawafu hapo kunena kwa ruga ni ishara ya roho mtakatifu

Peter Benny
Peter Benny
3 years ago

Naomba kuwa natumiwa masomo zaidi kwa njia ya email au hata ikiwezekana kwa njia ya what’s App kwa namba hii +255629836929 naamini ntazidi kujengwa KIROHO

Haron
5 months ago
Reply to  Admin

Pia mm

Peter Benny
Peter Benny
3 years ago

Napendezwa sana na haya masomo na yananibariki na kunipa ufaham mkubwa zaidi juu ya mambo ya ufalme wa MUNGU