NAMI NITAMPA ILE NYOTA YA ASUBUHI.

NAMI NITAMPA ILE NYOTA YA ASUBUHI.

Ufunuo  2:26 “Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.

28 Nami NITAMPA ILE NYOTA YA ASUBUHI”.

Je unaijua nyota ya ASUBUHI nini?

Hii si nyingine  zaidi ya YESU KRISTO mwenyewe.

Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile NYOTA YENYE KUNG’AA YA ASUBUHI”.

Ahadi ya kuishi na YESU milele ni ahadi kuu sana, ni furaha isiyo na kifani kuishi na YESU milele.

Ni furaha isiyo na kifani kumtazama milele yeye aliyemwaga damu yake pale msalabani kwaajili yetu sisi tusiostahili.

Lakini ni hasara kubwa sana kukosa kuwa na YESU milele. Ndio maana katika kitabu hiko cha Ufunuo Bwana  YESU mwenyewe anasema yeye ashindaye atampa “Ile nyota ya asubuhi”.

Maana yake yeye atakayeshinda atakaa na YESU milele.

Je umempokea YESU?.. Je una uhakika kwamba atakaporudi utakwenda naye mawinguni na kukaa naye milele?.

1 Wathesalonike 4:17 “Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo TUTAKUWA PAMOJA NA BWANA MILELE”.

Kama bado mpe leo YESU maisha yako kwa kutubu na kubatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu.

Shalom.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply