REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.

REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tuyatafakari maandiko pamoja.

Katika maisha, hakikisha unarekebisha vitu vinne. 1) Kazi unayoifanya 2) Kabila unalotoka 3) Nchi unayotoka 4) Mahali unapotoka.

Haya ni mambo makuu manne ambayo ni nguzo katika kuyajenga au kuyaharibu maisha. Na kimojawapo kisipokaa sawa mbele za Mungu, basi kitakuletea tufani kubwa katika maisha.

Hebu tuisome kidogo habari ifuatayo..

Yona 1:7 “Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona.

8 Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani?

9 Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu.

10 Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha.

11 Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka“

Walipoanza kwenye nchi, aliwaambia yeye ni Mwebrania..hivyo wakajua moja kwa moja ni mtu wa Taifa la Israeli,ametokea katika mojawapo ya miji ya kule, alipoendelea mbele kidogo, kwenye shughuli anayoifanya akasema yeye anamcha Mungu (yaani maana yake ni mtumishi wa Mungu), anayehudumu katika shamba la Mungu, na kwamba ameikimbia kazi ya Mungu, ndipo walipoelewa tatizo lipo hapo, wakaogopa na kutafuta suluhisho kabla mambo hayajazidi kuharibika.

Sasa endapo Yona ingekuwa hajaikimbia kazi ya Mungu na baharini imewachafukia vile, basi tatizo ni lazima lingekuwa aidha kwenye kabila analotokea, na kama sio kwenye kabila basi kungekuwa na tatizo kwenye nchi anayotokea..au mahali anapotokea.

Hivyo Nataka uone leo kwamba kazi yako unayoifanya inaweza kuwa chanzo cha Tufani na misukosuko, hakikisha kazi unayoifanya yoyote ile aidha ya mikono, iwe inampendeza Mungu kwa viwango vyote, uwe mwaminifu katika kazi yako na pia jiepushe na hila na wizi. Vilevile kama unafanya kazi ya Mungu hakikisha hukwepi majukumu yako kama mtumishi, wala huifanyi kwa ulegevu vinginevyo utakumbana na tufani kama iliyokuta Yona.. Na mkristo yoyote ni lazima awe na jukumu katika kazi ya Mungu. Hivyo jihakiki sana.

Yeremia 48:10 “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu”

Vile vile kabila unalotoka linaweza kuwa chanzo cha matatizo. Makabila mengi yana mila na desturi zilizo kinyume na Neno la Mungu, makabila mengi yana matambiko na ushirikina, jiepushe na hayo yote baada ya kuokoka. Zipo mila nyingine ambazo ni aibu hata kuzisema hapa..Hizo zote ni rahisi kukusababisha tufani katika maisha yako, na hasira ya Mungu kuwaka juu yako. Jiepushe na hizo mila…Sisemi kwamba ujiepushe na ndugu zako au wazazi wako wanaofanya hizo mila!, na uwachukie na kuwasema Hapana!..endelea kubaki na ndugu zako, waheshimu,wapende, watunze, waombee, na ishi nao kwa furaha zote na kushirikiana nao kwa mambo mengine yote mazuri wanayoyafanya lakini usishiriki mila hizo zilizo kinyume na neno la Mungu.

Pia nchi unayotokea au mahali ulipo panaweza kuwa chanzo cha tufani katika maisha yako..Hivyo ni wajibu wa kushiriki mambo mazuri yanayoendelea katika nchi yako, na kuyakataa yale mabaya yote, Nchi inaweza kuhalalisha ndoa za jinsia moja kisheria kabisa!, nchi inaweza kuhalalisha uvutaji wa bangi, nchi inaweza kuhalalisha utoaji mimba, nchi inaweza kuhalalisha ndoa za wanadamu na wanyama n.k.

Nchi ya namna hiyo tayari ipo chini ya laana na hasira ya Mungu na watu wake ni hivyo hivyo..Hivyo ni wajibu wa wewe uliyeokoka unayeishi ndani ya nchi kama hiyo, kujitenga kwa kutofanya hayo mambo au kukubaliana nayo, ili usiwe miongoni mwa wanaomwudhi Bwana Mungu. Na kujitenga sio kutoongea nao, au kutofanya nao kazi kwenye kampuni moja!..hapana..bali kujiepusha na njia zao, mfano wa Danieli, Meshaki, Shedraka na Abednego jinsi walivyoishi katikati ya taifa la Babeli lakini hawakushiriki matendo ya watu wa Babeli, na walifanikiwa sana katikati ya Taifa lile ovu.

Bwana atusaidie na Bwana atubariki

Na mwisho kabisa kama umejaliwa kupata watoto, au unampango wa kuwa na watoto..kumbuka kuwalea katika njia inayowapasa, angali wakiwa wadogo, kwasababu wakiwa wakubwa hawataiacha biblia inasema hivyo, Na pia wewe mwenyewe kama hujaokoka!. Mlango wa Neema upo wazi, usiidharau injili hata kidogo inayohubiriwa kwako bure! Bila kutozwa chochote… Hata vitu vingi vinavyoishiaga kutolewa bure mara nyingi huwa ni vya gharama sana na vya muhimu sana, kwasababu kama vingeuzwa basi hakuna mtu angeweza kununua..

Hata madawa yanayotolewa bure! Mengi ni ya gharama ya juu sana, yananunuliwa ghali sana aidha na serikali au mashirika binafsi lakini yanakuja kutolewa bure tu kwa watu ili kuokoa maisha!. Na wokovu ni wa gharama sana na wa muhimu kwa kila mtu, ndio maana tunapewa bure!, hivyo usiudharau, Laiti tungetozwa fedha ili kuupata, basi hakuna ambaye angeweza kuununua, hata dunia nzima tungekusanya nguvu zetu zote, tusingeweza kununua wokovu wa mtu mmoja tu! Licha ya watu wa dunia nzima. Mpokee Yesu leo kama hujampokea, na ukabatizwe na kupokea Roho Mtakatifu. Kwa usalama wa maisha yako.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

YONA: Mlango 1

YONA: Mlango wa 2

JINA LA MUNGU NI LIPI?

USIPOKUWA MWAMINIFU, NAFASI YAKO ITACHUKULIWA.

KUMCHA MUNGU NI NINI? NA MTU ANAMCHAJE MUNGU?

JE NI LAZIMA MKRISTO AOE/AOLEWE?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

KAMA ZILIVYOKUWA SIKU ZA NUHU NA ZA LUTU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments