Hakuna mtu anenaye katika Roho,kusema Yesu amelaaniwa

Hakuna mtu anenaye katika Roho,kusema Yesu amelaaniwa

SWALI: Mstari huu una maana gani?

1 wakorinto 12:3 “Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”

JIBU: Maana yake ni kwamba hakuna mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu anayeweza kusema Yesu amelaaniwa, hilo haliwezekani kwasababu mpaka ameshaingia ndani katika Roho hawezi kumwona Yesu kwa namna hiyo….Na vile vile hakuna mtu ambaye hajajazwa Roho Mtakatifu anayeweza kusema Yesu ni Bwana…Ni lazima yeye naye awe katika Roho Mtakatifu kwanza ndio awe na ufunuo huo wa kusema Yesu Ni Bwana,

Vinginevyo atakuwa anatamka kwa mdomo tu, kwamba Yesu ni mwokozi wangu, au Yesu ni Bwana wangu, au Yesu ni njia lakini isiwe imetoka ndani ya moyo wake…akawa anasema kishabiki tu!..au kidini tu au kwa kuiga tu!…wakati ndani ya moyo wake hajapata ufunuo kamili au hajamwelewa Yesu kabisa!…ambao ufunuo huo wa kumwelewa Yesu, unatoka kwa Roho Mtakatifu mwenyewe. Ndio maana hapo anasema pasipo Roho Mtakatifu mtu hawezi kusema Yesu ni Bwana, kutoka ndani ya vilindi vya moyo wake!!…

Na sio hilo tu!…Pia mtu ambaye hana Roho Mtakatifu biblia inasema huyo sio wa Mungu..

Warumi 8:9 “…Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.”

Kwanini sio wake?…Kwasababu huwezi kusema unamjua Mungu wakati kile kinachokufanya wewe umjue yeye hakipo ndani yako….(na hicho kinachotufanya tumjue yeye, na kutufunulia maandiko ni Roho Mtakatifu)…Kamwe hatuwezi sisi kumjua Mungu wala kumwelewa wala kumfuata yeye kwa nguvu zetu, tunamhitaji Roho Mtakatifu huyo ndiye anayetuvuta na kutusogeza kwa Mungu na kutufunulia Yesu ni nani..(Yohana 6:44, Yohana 15:16).

Hivyo ni muhimu sana kuwa na Roho Mtakatifu kwasababu huyo ndio MUHURI wa Mungu kwa mtu, Kama vile alama ya mnyama ilivyo(666), vivyo hivyo alama ya Mungu au muhuri wa Mungu ni Roho Mtakatifu ndani ya mtu (soma Waefeso 1:13, Waefeso 4:30 na 2Wakorintho 1:22).

Maran atha!

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

Je! Mwanamke anapaswa afunikwe kichwa anapokuwa ibadani?

Kwanini Bwana alirejea Tiro na Sidoni kwa mfano wa Sodoma?

Je ni kweli huwezi kuijua karama yako mpaka uwekewe mikono na wazee?

Wewe u nabii yule akajibu la!..swali huyu ‘nabii yule’ ni nani?

USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments