Jibu la swali hili linahitaji unakini mkubwa kwasababu lisipoeleweka vizuri ni rahisi kusema biblia ina ubaguzi wa kijinsia au biblia haimaanishi hivyo inavyomaanisha.
Hebu tusome mistari michache ifuatayo..
1Wakorintho 11:3 “Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. 4 Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake. 5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa. 6 Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe. 7 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. 8 Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume. 9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume. 10 Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na DALILI YA KUMILIKIWA KICHWANI, kwa ajili ya malaika”.
1Wakorintho 11:3 “Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.
4 Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.
5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.
6 Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
7 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.
8 Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.
9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.
10 Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na DALILI YA KUMILIKIWA KICHWANI, kwa ajili ya malaika”.
Katika mistari hii Mtume Paulo aliindika kwa uongozo wa Roho Mtakatifu ili kufikisha ujumbe kwa kanisa lote la Mungu kwa wote watakaosoma waraka huo, na waraka huo haukuwahusu wakorintho tu kama wengi wanavyotafsiri..bali ililihusu kanisa la Kristo kwa ujumla, ikiwemo na sisi watu wa nyakati hizi za mwisho.
Sasa kama ukisoma mistari hiyo utaona, Imejikita sana katika Eneo la KICHWA…Na imezungumzia vichwa vitatu…1) kichwa cha Kristo, 2) Kichwa cha Mwanamume 3) Kichwa cha mwanamke…
Tukianza na kichwa cha Kwanza, ambacho ni cha Kristo, biblia imekitaja kuwa ni Mungu mwenyewe…maana yake aliyekuwa na mamlaka juu ya Kristo ni Mungu peke yake, ambaye ndiye Baba yake..
Na pili kichwa cha Mwanamume ni Kristo..maana yake ni kwamba..Kristo ndiye mwenye mamlaka juu ya kila mwanamume…
Na tatu kichwa cha kila mwanamke ni mwanamume…Maana yake ni kwamba mwenye mamlaka juu ya mwanamke ni mwanamume…Na mamlaka hayo mwanamume alipewa na Mungu pale Edeni (Mwanzo 3:16)
Sasa kwasababu mwanamume ndiye kichwa cha Mwanamke…basi mwanamke ni lazima aonyeshe dalili au ishara ya kumilikiwa katika kichwa chake…na ishara hiyo sio nyingine zaidi ya kufunika kichwa…Ni kama vile ulivyo utaratibu wa mwanamke kuvishwa shela linalofunika mpaka kichwa wakati wa harusi au anapovishwa pete, ni kuonyesha ishara ya kumilikiwa na mwingine…Ndivyo hivyo hivyo kila mwanamke anapaswa afunike kichwa anapokuwa kanisani kuonyesha ishara ya unyenyekevu, na ya kumilikiwa na wanaume ambao ndio vichwa vyao.
Sasa wengi wakisikia hili neno kutawaliwa/kumilikiwa wanachukia na linawakwaza!..wanadhani wameambiwa waabudu wanaume, (kumbuka anayestahili kuabudiwa ni Bwana wetu mmoja tu Yesu Kristo)!..Lakini katikati yetu wanadamu Mungu katuweka chini ya milki ya watu wengine,ili kufikisha ujumbe Fulani wa rohoni. Kwamfano Mtoto yoyote yule awe wa kiume au wakike anapokuwa mdogo anakuwa yupo chini ya milki ya wazazi wake, kwa faida yake huyo mtoto…Sasa mtoto akichukia kumilikiwa na wazazi wake atakuwa ni mgonjwa, kwasababu Mungu akitaka kumlisha au kumbariki ni lazima atumie wazazi wake/walezi wake kumbariki huyo mtoto. Na ndio hivyo hivyo, katika roho wanawake wote ni milki ya wanaume, ndivyo Mungu alivyopenda iwe hivyo, hakuna awezaye kubadilisha, na hiyo pia ni kwa faida ya wanawake..
Mwanamke yoyote anayekataa kutawaliwa au kumilikiwa na mwanamume akidhani atakuwa anamwabudu, anajimaliza mwenyewe!…ukitaka mambo yako yaende sawa kubali kumilikiwa, lakini ukitaka laana kataa kumilikiwa!…Vivyo hivyo unapokuwa kanisani mwanamke ukitaka ufaidike na ibada yako FUNIKA KICHWA CHAKO!, kama ishara ya kumilikiwa!…na tena biblia hapo kwenye mstari wa 10 inasema wazi kabisa kwamba “kwaajili ya malaika funika kichwa chako”….Maana yake ni kwamba malaika wa Bwana wanaopita kanisani kwaajili ya kuwahudumia watakatifu kulingana na Waebrania 1:14, wanapopita na kukuta kichwa chako kipo wazi, na tena umeweka wigi, au rasta hawawezi kukuhudumia…
Na ndio kazi ya shetani kuyafanya yale mambo madogo yaonekane sio maana sana, ili watu wasipate Baraka kutoka kwa Mungu..
Funika kichwa mwanamke wa kikristo uwapo ibadani, hilo ni Neno la Mungu na lipo katika agano jipya na si la kale, Usilidharau Neno la Mungu kwa kiburi cha kupandikiziwa na shetani, usikubali shetani akichezee kichwa chako..kumbuka ndio utukufu wako upo hapo, biblia inasema hivyo.
Kama maneno haya unafikiri ni ya uongo, hebu fanya utafiti siku moja, kisafishe kichwa chako, vaa vizuri, funika kichwa chako kwa kitambaa/kilemba, halafu nenda kanisani..utaona utofauti wa siku hiyo na siku nyingine, ndipo utakapojua kuwa Neno la Mungu sio uwongo…Utaona hata maneno yanayotoka katika kichwa chako yanakuwa na nguvu na uweza, hata uombaji wako utakuwa tofauti,,utatembea na jeshi la malaika wa mbinguni. Vilevile jambo hilo linaambatana na kujisitiri, ukiwa ni mwanamke wa kuvaa ovyo ovyo tu kila mahali, kamwe hutakaa uuone utukufu wa Mungu haijalishi utasema wewe umeokoka kiasi gani.
Hilo ni Neno la Mungu.
Bwana akubariki.
Mada Nyinginezo:
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
NAO WALIOKUWA WAMEKUSUDIWA UZIMA WA MILELE WAKAAMINI.
NI NANI ALIYEWALOGA?
USIMZIMISHE ROHO.
NI NINI TUNAJIFUNZA JUU YA MT. DENIS WA UFARANSA?
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Mwanamke amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya MAVAZI,iweje tena tuzungumzie vitambaa kama kifuniko?
Huo ulikuwa ni mbadala wa kitambaa,Sasa wanawake wa Africa nywele Walizonazo kama mbadala vni zipi????kama hawataanza kukosoa uumbaji wa Mungu Kwa kuzigeuza ziwe kama za wazungu au mara wazisuke wakati imekatazwa.
Hapana maandiko hayajasema wazifanye ziwe kama za wazungu.. bali waziache ziwe ndefu kwa kiwango cha kutosha…
Kwakwel inabidi wanawake tuishi kama biblia inavyo tutaka tuishi ili hakika tuurithi ufalme wa Mungu