Swali: Kwanini Mungu aliwapeleka wana wa Israeli Misri kwa miaka 400, Ni kosa gani kubwa walilolifanya mpaka Mungu kuwauza kwa Farao miaka yote hiyo?
Jibu: Hakuna kosa lolote walilolifanya mpaka kufikia hatua hiyo ya kupelekwa Misri katika nyumba ya utumwa. Bali Mungu aliruhusu iwe hivyo, kwa makusudi maalumu. Ni kama tu Yusufu alivyoenda kuuzwa kwa Misri kwa Potifa, maandiko hayaonyeshi kuwa Yusufu alifanya kosa lolote lililompelekea kwenda kuuzwa kama mtumwa kwa Potifa, lakini maandiko yanaonyesha kuwa Mungu alimpeleka Misri kwa lengo la kuwaokoa watu wengi siku za mbeleni, tunalisoma hilo katika Mwanzo 45:4-8
Mwanzo 45:4 “Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. 5 Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; MAANA MUNGU ALINIPELEKA MBELE YENU KUHIFADHI MAISHA YA WATU. 6 MAANA MIAKA HII MIWILI NJAA IMEKUWA KATIKA NCHI, NA IKO TENA MIAKA MITANO ISIYO NA KULIMA WALA KUVUNA. 7 MUNGU ALINIPELEKA MBELE YENU KUWAHIFADHIA MASAZO KATIKA NCHI, NA KUWAOKOA NINYI KWA WOKOVU MKUU. 8 Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri”.
Mwanzo 45:4 “Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri.
5 Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; MAANA MUNGU ALINIPELEKA MBELE YENU KUHIFADHI MAISHA YA WATU.
6 MAANA MIAKA HII MIWILI NJAA IMEKUWA KATIKA NCHI, NA IKO TENA MIAKA MITANO ISIYO NA KULIMA WALA KUVUNA.
7 MUNGU ALINIPELEKA MBELE YENU KUWAHIFADHIA MASAZO KATIKA NCHI, NA KUWAOKOA NINYI KWA WOKOVU MKUU.
8 Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri”.
Hali kadhalika Mungu aliwapeleka wana wa Israeli Misri na kuwafanya kuwa watumwa, kwa malengo makuu mawili.. ambayo yanafanana na yale ya Yusufu.
1.MUNGU KUTANGAZA UKUU WAKE.
Kupitia wokovu wa Israeli kutoka Misri kwa mapigo yale 10 aliyompiga nayo Farao, na kwa kupitia ishara za ajabu alizozofanya jangwani kama kushusha Mana, kuleta Kware, kudhihirisha Nguzo ya Wingu na Moto n.k, ulimwengu umeweza kumjua Mungu wa Ibrahimu kuwa ni Mungu mkuu na wa haki na mwenye nguvu nyingi na maajabu mengi.
Kwahiyo ijapokuwa Israeli waliteswa Misri lakini maisha yao baadaye yalikuja kuwa mahubiri makubwa sana kwa ulimwengu kumjua Mungu wa kweli, pengine wasingepitia hiyo njia ya mateso tusingemjua Mungu kwa kiwango hicho.
2. KUTANGAZA NJIA YA WOKOVU
Lengo la pili la wana wa Israeli kupitia yale maisha ni kutangaza njia ya Wokovu. Maisha yao kuanzia Misri mpaka Kaanani, ni ufunuo kamili wa maisha ya Wokovu kutoka Dhambini(Misri), kueleka mbinguni (Kaanani) mji wa raha.
Tunapomwamini Bwana Yesu na kutubu dhambi zetu, katika roho ni kama tumetoka Misri..na hivyo Kristo anatuweka huru mbali na vifungo vyote vya dhambi, kwasababu maandiko yanasema “atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi (Yohana 8:34)”.
Hii inatufundisha nini?.. Si kila mateso tunayoyapitia yanatokana na makosa tuliyoyafanya?.. Yusufu hakuna kosa alilolifanya mpaka kufikia kuuzwa Misri kwa Potifa na hata kufungwa gerezani, vile vile wana wa Israeli hakuna kosa walilolifanya mpaka kufikia kuwa watumwa kwa muda ule, bali Mungu aliruhusu hayo yatokee ili mwisho wake aonyeshe utukufu wake!..
Kwahiyo hatutakiwi kukata tamaa tunapopitia shida, maadamu tuna uhakika tupo sawa na Mungu (yaani tunaishi maisha yanayompendeza yeye), vile vile tunapopitia magonjwa ya muda mrefu hatupaswi kukata tamaa wala kulaumu, bali tunapaswa kushukuru na kuendelea kuomba na kuishi maisha yanayompendeza, kwasababu Mungu anataka kufanya maisha yetu kuwa ushuhuda..
Hata Kristo maisha yake yalikuwa ni ya ushuhuda, alikuwa kama namna ya mtumwa (Wafilipi 2:7-8), lakini alijua mwisho wake utakavyokuja kuwa, na sisi hatuna budi kuwa watu wa namna hiyo hiyo, kwasababu mwisho wetu utakuwa mzuri hata kama mwanzo wetu umekuwa mbaya na wa kukatisha tamaa, maadamu tupo katika Neno lake na amri zake, basi hatuna haja ya kuwa na hofu, ni suala la muda tu.
Maran atha!.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI.
MAJARIBU 10 WANA WA ISRAELI WALIYOMJARIBU MUNGU.
JIHADHARI NA MKUTANO WA WATU WALIOCHANGANYIKANA.
Bwana aliposema “sikuja kutangua torati bali kuitimiliza” alikuwa anamaanisha nini?
Nini tofauti ya Mtumwa, Mjakazi na kijakazi?
Rudi nyumbani
Print this post
Kuna watu wanasema kosa kubwa lililo wapeleka Israel misri linatokana na Baba Ibrahim kwakuto kuchunga Sadaka na kunguru wakakula ndipo Mungu akaamuwa kuwaweka utumwani kama adhabu kwa ibrahimu jee ni jweli
Hapana si kweli ndugu…
Ameen ubarikiwe ndugu