Pande zote twadhikika, bali hatusongwi;(2Wakorintho 4:8)

Pande zote twadhikika, bali hatusongwi;(2Wakorintho 4:8)

Unaweza kushushwa chini, lakini simama usivunjike moyo.

2Wakorintho 4:8  “Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; 9  twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi”

Kwa kuwa bado tupo duniani, dhiki, mateso, manyanyaso hayaepukiki katika baadhi ya vipindi, Kiongozi wetu Yesu alituweka wazi, kwamba “duniani mnayo dhiki, lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu”(Yohana 16:33)

Utaudhiwa na mume/mke/baba/mtoto, kwasababu ya imani, utapigwa bila sababu, utatishiwa kufukuzwa kazi, utakuwa na mashaka pande zote, mwingine hujui kesho utaamkaje, ule nini, magonjwa hayana mwisho..Lakini katika yote, bado neema ya Mungu itatushika na kutusaidia, hatutasongwa kiasi hicho mpaka kuicha imani, hatutakata tamaa, hata turudi nyuma, Bwana atakuwa upande wetu.

Mambo hayo ni ya kitambo tu, hata kama tutauawa, bado tunao uzima wa milele, hata kama tutapoteza kila kitu bado mwenye vitu vyote yupo ndani yetu. Tutadhikika pande zote, tutasongwa kila mahali lakini hatutakata tamaa. Tukumbuke tu,  Kila pito linasababu yake, lakini katika yote, tujue Bwana anatuwazia mawazo mema, tukishakwisha kukamilishwa tutatoka kama dhahabu.

Yakobo 1:2  “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3  mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4  Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno”.

Bado maandiko yanasema..

1Petro 1:6  “Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;

7  ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo”.

Bwana awe nawe.

Maombi yangu:

“Baba mwema, nakushukuru kwa neema ya wokovu uliyonipa, Najua kama sio wewe nisingefika hata hapa nilipo, nakuomba Mungu wangu unione katika dhiki zangu, uyaone machozi yangu, uniondoe katika mateso yangu. Lakini zaidi unipe nguvu ya kuweza kukabiliana na dhiki zote za ulimwenguni, nisirudi nyuma wala kukata tamaa. Nikutumikie wewe katika mazingira yote. Upendo wako usipunguke ndani yangu. Ninaomba nikiamini katika jina la Yesu Kristo. Amen”.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA.

UYATIE MACHOZI YANGU KATIKA CHUPA YAKO EE! BWANA.

Furaha ni nini?

Unyenyekevu ni nini?

JE! UTATOA HESABU YA NINI KATIKA SIKU ILE?

Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Paul Peter
Paul Peter
1 year ago

Mungu akubariki sana ndugu kazi yako ni kubwa unayoifanya masomo ambayo huwa nayasoma kwenye blog hii yamenitoa kiwango kimoja hadi kingine katika imani yangu