Nini tofauti ya Mtumwa, Mjakazi na kijakazi?

Nini tofauti ya Mtumwa, Mjakazi na kijakazi?

      1. MTUMWA

Mtumwa ni mfanyakazi wa jinsia ya kiume. Kawaida ya mtumwa, anakuwa anatawaliwa uhuru wake na maamuzi yake kwa asilimia kubwa na yule anayemtumikisha au aliyemwajiri. Hivyo mwanaume yeyote anayetumika chini ya bwana wake kwa namna hiyo anaitwa MTUMWA.

Sisi tuliokoka tunakuwa ni watumwa wa Bwana Yesu (2Timetheo 2:24)..na wote ambao hawajamwamini Bwana Yesu, wanakuwa ni watumwa wa dhambi.

Yohana 8:33 “Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?

34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, KILA ATENDAYE DHAMBI NI MTUMWA WA DHAMBI.

35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.

36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”.

2. MJAKAZI.

Mjakazi ni mtumwa wa kike, sifa zile zile  alizonazo mtumwa wa kiumbe, ndizo hizo hizo alizonazo mjakakazi.

Mfano wa aliyekuwa Mjakazi katika biblia ni Hajiri.

Mwanzo 16:1 “Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, JINA LAKE HAJIRI”.

 3. KIJAKAZI.

Kijakazi ni Mjakazi wa hadhi ya chini Zaidi. Ni sawa na kutumia neno “kitoto” badala ya “mtoto”..ndivyo ilivyo kwa “Kijakazi” na “Mjakazi”..Mfano wa vijakazi katika biblia ni BILHA NA ZILPA.

Mwanzo 35:25 “Wana wa Bilha, KIJAKAZI WA RAHELI, ni Dani na Naftali.

26 Wana wa Zilpa, KIJAKAZI WA LEA, ni Gadi na Asheri”.

Biblia inatushauri tusiwe “watumwa wa wanadamu”, bali wa Bwana.

1Wakorintho 7:23 “Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu”.

Vile vile tusiwe watumwa wa dhambi ambao ndio Mbaya Zaidi.. Dhambi inapomtumikisha mtu, mshahara wake ni MAUTI!!. Heri mwadamu akiisha kutumikisha atakulipa fedha, au mali..lakini dhambi inakulipa Mauti.

Warumi 6:23 “Kwa maana MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Sasa ili kuondokana na utumwa wa dhambi, tunafanyaje?

Bwana Yesu alisema maneno yafuatayo..

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Jitie Nira ya Bwana Yesu, ufanyike mtumwa wake, kwasababu Mshahara wake ni UZIMA WA MILELE!!!.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA FILEMONI.

MJUE SANA YESU KRISTO.

LEO WOKOVU UMEFIKA NYUMBANI HUMU

Tofauti kati ya maandiko na Neno ni ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Lucas mhula
Lucas mhula
2 years ago

Amen