Matoazi na Matari ni nini? (Kutoka 15:20)

Matoazi na Matari ni nini? (Kutoka 15:20)

SWALI: Shalom, Naomba kuuliza maana ya MATOAZI kama vyombo vya muziki ni chombo gani? Asante sana


JIBU:

Matoazi, na  Matari ni jamii moja,, Hizi ni za ala za muziki, ambazo zilitumika kwa matukio tofauti tofauti , aidha kusifu, kuimba, kusherehekea, kukaribisha, kupongeza na wakati mwingine kwenye miendo ya  vitani.. zikiimbwa huwa zinashikiliwa na mkono mmoja na mkono mwingine unatumika kupiga toazi au tari kwa utashi, na kupigwa kwake ni lazima kuambatane na kucheza. Tazama picha.

Ili kuelewa kinadharia zaidi, unaweza kutazama video hizi chache Youtube, uone jinsi upigwaji wake ulivyo.

https://www.youtube.com/watch?v=4UJT9sM_ABo

https://www.youtube.com/watch?v=xbhk5yYgUxI

Katika biblia tunaona, wakati ule Daudi alipokuwa analileta sanduku la Bwana, Yerusalemu, yeye na Israeli wote walikusanyika na kumchezea Mungu kwa nguvu zao zote, na moja ya kifaa cha muziki walichokitumia kumwimbia Mungu kwa nguvu zile z kilikuwa ni Matoazi

2Samweli 6:5 “Daudi na nyumba yote ya Israeli wakacheza mbele za Bwana kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa kayamba, na kwa matoazi”.

Hata alipowaweka Walawi kwa kazi mbalimbali za kikuhani, wale aliowaweka katika zamu za uimbaji, wote walibeba matoazi yao, kwa ajili ya kumwimbia Mungu.

1Nyakati 15:15 Na wana wa Walawi wakalichukua sanduku la Mungu mabegani mwao kwa miti yake, kama vile Musa alivyoamuru, sawasawa na neno la Bwana.

16 Kisha Daudi akamwambia mkuu wa Walawi, kwamba awaagize ndugu zao waimbaji, pamoja na vyombo vyao vya kupigia ngoma, vinanda, na vinubi, na matoazi, wavipige na kupaza sauti kwa furaha.

Soma pia 1Nyakati 13:8, 16:42, 25:1. 2Nyakati 29:25

miriamu na matari

Tunamwona tena Miriamu, dada yake Musa, siku ile, Mungu alipowapigania na kuwaangamiza maadui zao wamisri katika bahari ya Shamu, biblia inatuambia Miriamu pamoja na wanawake wengine waliondoka na kumchezea Mungu sana, na ala walizotumia yalikuwa ni haya Matari.

Kutoka 15:20 “Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza”.

Tunamwaona Yeftha naye alipotoka vitani, kwa ushindi, binti yake akatokea ili kumlaki kwa kumchezea, na kifaa alichokitumia kilikuwa ni haya Matari.

Waamuzi 11:34 “Kisha Yeftha akafika Mispa nyumbani kwake, na tazama, binti yake akamtokea kumlaki, na matari na machezo; naye alikuwa ni mwanawe pekee; hakuwa na mwingine, mwana wala binti, ila yeye”.

Je hata sasa na sisi tunaruhusiwa kumchezea Mungu kwa matari?

Ndio Mungu anapaswa afurahiwe, kwa midundo tofauti tofauti na ala tofauti tofauti za muziki, ikiwa akina Miriamu, na Daudi, na wana wa Israeli wote walimchezea Mungu kwa nguvu zao zote, hata sisi tunapaswa tufanye hivyo na zaidi, kwa mambo makuu Mungu  anayotutendea kila siku na zaidi sana kwa kutupa zawadi ya mwanawe mpendwa YESU KRISTO ili atuokoe.

Lakini jambo la kuzingatia ni kuwa uchezaji wetu haupaswi kufanana na ule wa watu wa kidunia, wala uimbaji wetu haupaswi kufanana na ule wa watu wa kidunia, Vinginevyo sifa zetu zitabadilika na kuwa kufuru mbele za Mungu. Hilo ni la kulizingatia sana. Tuchezapo tucheze kwa jinsi Mungu atakavyotuajilia, lakini sio kumchezea Mungu kwaito, na mfano wa staili za kidunia ambazo hazimpendezi Mungu.

ZABURI 150

1 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.

2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;

4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;

5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?.

Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)

USIPIGE MATEKE MCHOKOO!

NA BAADA YA LILE TONGE, SHETANI AKAMWINGIA.

KWANINI KRISTO AFE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
lucas mhula
lucas mhula
2 years ago

Amen🙏🙏🙏

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Ameeeen Mtumishi, Mungu zaidi kuwabariki,najifunza mambo mengi ya kiroho .