Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)

Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)

​​SWALI: Kulingana na Hesabu 9:11 Je! kuna sikukuu za pasaka mbili kwa mwaka?

Hesabu 9:11 “mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu;”


JIBU: Mungu aliwaagiza wana wa Israeli kila tarehe kumi na nne (4) ya mwezi wao wa kwanza, itakuwa ni sikukuu ya pasaka kwao, ambayo wataila kama kumbukumbu la siku ambayo Mungu aliwatoa katika nchi ya Misri katika nyumba ya utumwa.

Hivyo kila inapokaribia tarehe hiyo ya mwezi wa kwanza wayahudi wote walijitakasa na kukusanyika pamoja ili kuila pasaka hiyo..Na ilikuwa ni sheria na lazima.

Lakini tunaona hapo katika kitabu cha Hesabu kuna mwezi mwingine ambao ni wa pili, tarehe kama hiyo hiyo ya 14, wayahudi walikuwa wanakusanyika tena waile pasaka..

Swali ni Je kulikuwa na pasaka nyingine ya pili?

Jibu ni ndio Mungu aliruhusu iwepo pasaka nyingine ndogo.. Na ni kwanini aliruhusu, ni kwasababu kulikuwa na watu ambao kipindi cha sikukuu ya kwanza hawakuweza kufika kwa wakati kutokana na umbali wa safari…na wengine walikuwa wamenajisika kwa kushika maiti, ambayo iliwagharimu muda wa siku saba mpaka wawe safi(Hesabu 19:11)..Na sheria ilikuwa hauruhusiwi kwa namna yoyote kuingia katika kusanyiko lolote la watakatifu mpaka utakapokuwa safi kabisa. 

Kwahiyo kulikuwa na kundi kubwa la watu ambao walishindwa kuila sikukuu hiyo ya pasaka kwa kwasababu hizo zilizoorodheshwa.

Hivyo kwa makundi kama haya ya watu, walipewa nafasi yao ya kipekee na Mungu ili kusudi kwamba sikukuu hii isiwapite kabisa katika mwaka huo.

Tusome..

Hesabu 9:10-12

[10]Nena na wana wa Israeli, kuwaambia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, ye yote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka kwa BWANA;

[11]mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu;

[12]wasisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika.

Hiyo ndio sababu ya kuwepo kwa sikukuu nyingine ndogo ya pasaka..iliyofanyika mwezi mmoja baadaye.

Lakini Je hadi sasa tunayo maagizo kama haya ya kuzishika sikukuu za pasaka?

Katika agano jipya hatusheherekei tena sikukuu za pasaka kwa jinsi ya mwili, bali kwa jinsi ya Roho tukikumbuka kuwa pasaka wetu Yesu Kristo tayari alishachinjwa zamani..

Hivyo wakati wote tupo katika pasaka yake.

Lakini leo hii wengine wanaifananisha siku hii na siku ya Valentino (Valentine’s day)..yaana siku ya wapendanao duniani kama wanavyosema ambayo huwa inaadhimishwa kila tarehe 14 mwezi wa 2 duniani kote..Jambo ambalo halihusiani kabisa na Sikukuu hii ya Bwana. 

Kwanza mwezi wa pili wa kiyahudi sio sawa na mwezi wetu wa pili wa kalenda ya Gregory..

Pili Upendo uliotangazwa na Valentino.Hauhusiani kabisa na Upendo uliotangazwa na Yehova Mungu wetu katika maandiko yake matakatifu.

Hivyo hatupaswi kuyalinganisha mambo ya kimbinguni na sherehe za kidunia. Sisi kama wakristo hatusheherekei Valentine’s day. Ni sikukuu ya kipagani. Tunaisheherekea pasaka ya Bwana kila siku katika Roho.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?

Mwandamo wa mwezi/Mwezi mpya Ni nini kibiblia?

Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

UNYAKUO.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments